Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.
 
Usiwe na mawazo ya kula tunda kimasihara
Wakati watu wakiwa wanakata tiketi wanaangalia majina. Siku moja nasafiri, kuangalia list ya abiria kwenye chat, nikaona jina Irene Emmanuel si nikajiweka pembeni yake. Kilichonipata ndio hiki sasa!!!!
Kumbe zigo lenyewe ndio hili, nilisafiri kwa kukalia nusu tako toka Dar hadi Kigoma.

1682042586459.png
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
 
Mimi nikiwa safarini sipendi kuongea ongea sana.
Mara nyingi nina headphones zangu nakula ngoma nilizodownload kwaajili ya Safari.
Wewe ndio wale mnafungulia ear phones zenu kwa sauti kubwa, halafu mnaja.ba bwiiiiiìiiiii kwa sauti mkiamini mtu wa pembeni hawezi sikia kwa sababu ya unene na ukubwa wa muziki, kumbe muziki unausikikiza peke yako
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
Si useme tu ulipiga viroba? Hata mimi hizo zilikuwa ndio zangu. Bia zinazingua jukojoa kwingi unakera watu
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
Kuna siku enzi hizo janki nasoma, natoka shule Tosamaganga naenda home Tanga. Basi ikafika Kitonga Comfort Hotel, nikala msosi wangu kisha nikachukua viroba kama nane hivi nikawa nafyonza mdogo mdogo.

Aisee nikazima. Nilitakiwa kushuka Chalinze niunge gari za kwenda Tanga, nikajikuta niko Mnazi Mmoja naamshwa nishuke, tumefika.
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" [emoji849][emoji849][emoji849]
Epuka kula ovyo ovyo hasa hasa vyakula kama ndizi mbivu, mahindi ya kupikwa, vyakula vyenye majimaji mengii, hii itakusaidia kuepukana na tatzo la kuharisha au kutapika njianii
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
Na hapo ulipo umefunga na ukifungulia tu straight kwenye nyagi kama kawaida.

Hapo namna tisa hapo inanikumbusha wasambaa kwenye mabasi yao wote wanapewa mifuko maalum kwa ajili ya kutapika.

It was a new experience for me ila washambaa wanafurahisha sana na mambo yao.
 
Back
Top Bottom