Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄
2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.
3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.
4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.
5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.
6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.
7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.
8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.
9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.
10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.
Ongezea la kwako hapo kama unalo.