Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Mambo ya kuzingatia uwapo safarini

Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
We siyo mstaarabu,ungenunua hata bigijii ili usiwe kero Kwa wengine
 
Hii ni muhimu mno. Nilikuwa nakwenda Morogoro na basi la Abood la mwisho kabisa kutoka Dar.

Nilipata siti ya mwanzo kabisa nyuma ya dereva. Nilikuta kuna binti tayari keshakaa jirani ya siti yangu. Kama ilivyo uungwana nikamsalimia. Binti alinishusha na kunipandisha akachuna.

Nilikuwa nimechoka na mambo yangu, sikumtilia maanani nikauchuna na simu yangu. Tulipofika chalinze nilinunua maji na korosho, kama ilivyo uungwana nimkamkaribisha, demu, kimya. Hapo hapo na yeye alinunua maji akatoa noti ya 10,000. Jamaa akamwambia hana chenji na bus linataka kuondoka. Nikamwambia jamaa (ni wale wanaouza ndani ya bus) ampe nikamlipa. Kwa aibu akatoa asante ya chini chini. Sikumjibu.

Kufika Morogoro sasa, kumbe ilikuwa anaenda kukutana na mwanaume. Jamaa kila akipigiwa simu hapokei na mwisho akazima simu kabisa. Nililijua hili maana alianza kupiga simu toka tupo Mikese.

Nilipakia spare kwenye boot, hivyo tulipofika Moro ilibidi niwe mpole mpaka mizigo ya wengine iishe. Ndio bi dada ikabidi ajilete kipole kuuliza kama mimi ni mwenyeji Morogoro. Nikamwambia si mwenyeji nimekuja mara moja nageuza kesho yake.

Ikabidi sasa usister duu aweke pembeni aanze kufunguka ukweli. Kuwa alikuja kukutana na bwana 'ake na ndie aliemtumia nauli.
Ilikuwa ana Sh. 10,000 tu mfukoni na hajui pa kwenda maana mshkaji kaingia chaka.

Ikabidi nimwambie asubiri nichukue mizigo yangu halafu nitaona cha kumsaidia. Uzuri mwenye spare ilikuwa anazipokelea hapo hapo Msamvu. Nikaenda kuchukua chumba lodge na mgeni wangu nyuma. Baada ya hapo hatukutongozana tena. Alijuwa wajibu wake na maringo alitupa pembeni tena.

Msela wake alikuja kumtafuta asubuhi tukiwa tunajiandaa kuondoka akiomba samahani kuwa simu ili stuck touch akashindwa kupokea. Itoshe kusema kuwa jamaa alitukanwa kila tusi la duniani, mimi na cha maringo wangu tukarudi dar na kuendeleza libeneke kwa miezi kadhaa mbele mpaka nilipoamua kumpotezea kutokana na demu kuwa na shida za kila siku kuliko hata mkimbizi wa Sudan.
Kama story ya kweli hivi.
 
Kuna siku nilikua nimelewa sana halafu kwenye bus nilipanda kama staff(dereva tunajuana,classmate wangu)....
Sasa ile naingia tu harufu ya konyagi ikasambaa bus lote..

Kuna mwanamke akaropoka"naona mmepakia pipa la komoni humu mnatukera"...kumbe naenda kukaa nae kwenye seat moja,,,nilisafiri kwa manyanyaso...

Mwisho dereva akaniita nikaenda kukaa nae pale mbele akaninunulia na konyagi nyengine...
Aisee we jamaa umetisha sana.😁
 
Itoshe kusema kuwa jamaa alitukanwa kila tusi la duniani, mimi na cha maringo wangu tukarudi dar na kuendeleza libeneke kwa miezi kadhaa mbele mpaka nilipoamua kumpotezea kutokana na demu kuwa na shida za kila siku kuliko ha
Eyooooo gwe jhubhaaaaaa....... mwana kondoo mrembo mringaji anamfuata kaka chinjachinja 🇨🇳, akachinjwe kwa hiari yake mwenyewe
 
1. Salimia unayemkuta kwenye siti maana hujui ya baadae. Inakera hukusalimia halafu baadae unaanza kuuliza "Eti hapa tumefika wapi?" 🙄🙄🙄

2. Kuwa mstaarabu unapoingia kwenye basi hasa kama tayari unajua siti yako haina haja ya kugombania mlangoni.

3. Sikiliza nyimbo na video za kwenye simu yako kwa kutumia earphones kwani kinachokufurahisha wewe kwa mwingine yawezekana ni kero.

4. Usiongee na simu kwa sauti kubwa hasa mambo yako binafsi kwani hakuna anayehitaji kujua mambo yako.

5. Kuwa mwangalifu unaposinzia epuka kumlalia jirani yako unaposinzia. Sambamba na hilo soma gazeti lako kwa uangalifu sio unalitandaza hadi linagusa pua ya mwenzako.

6. Usilazimishe kuchungulia dirishani kila mara wakati umekaa siti ya katikati, hiyo ni kero kwa aliyekaa dirishani.

7. Kama unasafiri na watoto wakatie siti yao isiwe kero kwa jirani yako. Unasafiri na watoto watatu kwenye siti moja ni kero kwa jirani yako na kwa watoto.

8. Usipake pafyumu kali za kukereketa wenzio. Sambamba na hilo piga mswaki vizuri ni kero kukaa na abiria anayenuka mdomo hasa anapokusemesha.

9. Msome abiria uliyekaa naye kama hapendi kusemeshwa usimsemeshe semeshe, mwache, wengine wana mambo yao kichwani, wengine wanaenda kwenye misiba, wengine wamefukuzwa na waume zao huko walikotoka, sio kila mtu anapenda kuongea safarini.

10. Kama unajijua una tatizo la kutapika safarini jiandae mapema kwa kuwa na vifaa vya kukusaidia kwenye hali hiyo.

Ongezea la kwako hapo kama unalo.
Usipende kutongoza tongoza hovyo ukiwa safarini.
 
Na hapo ulipo umefunga na ukifungulia tu straight kwenye nyagi kama kawaida.

Hapo namna tisa hapo inanikumbusha wasambaa kwenye mabasi yao wote wanapewa mifuko maalum kwa ajili ya kutapika.

It was a new experience for me ila washambaa wanafurahisha sana na mambo yao.
hahaha,wasambaa na Mambo yetu
 
Back
Top Bottom