Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Hili jambo limekaa kiimani zaidi,lakini watu si wanapona jamani,anyway wizara ya afya imeshaunda task force yenye technical personells,watachunguza kwa undani huduma ya babu kama ina viwango vinavyokidhi na itatuambia kama hii dawa ni curative kwa hiyo tusubiri saizi tutabishana kwa mitazamo ya kiimani zetu na ukweli hautapatikana.
 
Safi sana wewe ndiye unaewaza vyema
 
Kama watu wanapona it is ok.saa hii nauli ya laki na zaidi inatoka wapi jamani?kama watu wanapona it is gud
 
tukumbuke huyu sio mtu wa kwanza tanzania kutamka kitu kama hicho.. kuna yule dada wa Kanyigo miaka ya 1990s katikati, James Brwn, Mzee wa Tegeta na NDUKAI.. where are they.....

Alikuwepo pia ESTHER na dawa ya uzazi kwa wanawake...
 

wee acha kjidai unamfahamu Mungu acha ujuha bana! kwani kina Nuhu, Loti, si peke yao waliteuliwa? wee umeathirika na umangaribi naona!
 

nakuomba uzikashifu na ARv's na za pressure , kisukari dawa zoote za kimangaribi, seems wewe ni limbukeni, issue hapo ni kupona! unajua ARV's zinawafanyia nini watu? bora miti shamba isiyotiwa midawa kabisa? tena ipo maporini hata moshi wa magari haikuwahi pata! so tulia kama unaumwa nda huko, na hiyo issue ya breaking news futa kabisa upupu wako!
 
Unakumbuka yale aliyofanya Yesu je kila mtu aliweza kuyafanya. Pia soma kuhusu fimbo ya MUSA. Je kila mtu aliruhusiwa kuitumia na ikafanya kazi. Imani haitakiwi kuhojiwa kama ilivyo kwa sheria ni kuijua na kuifuata, ukipingana nayo utahukumiwa.
 
Kama watu wanapona it is ok.saa hii nauli ya laki na zaidi inatoka wapi jamani?kama watu wanapona it is gud

Kwa sababu ya increased demand,watu wengi wanakwenda kwa babu hadi magari ya abiria hayatoshi,saizi magari ya kampuni za utalii yanakodiwa,wanachukua advantage hiyo ingawa sio vyema.
 
Unakumbuka yale aliyofanya Yesu je kila mtu aliweza kuyafanya. Pia soma kuhusu fimbo ya MUSA. Je kila mtu aliruhusiwa kuitumia na ikafanya kazi. Imani haitakiwi kuhojiwa kama ilivyo kwa sheria ni kuijua na kuifuata, ukipingana nayo utahukumiwa.

Haya tusubiri kama two weeks tuone kinahoendelea.
 

Imekukalia rohoni! wacha ikunyonye hasa ukifikiria kule mbele huji kitatokea nini ukiwa nyani je babu alishaenda/........
 


Wewe bado mchanga kiroho na upeo wako wa Bible ni mdogo sana inawezekana una husuda binafsi au una sali kwa Kakobe.
nikuulize maswali yafuatayo ukinijibu basi argument zako ni sahii:

1. Walikuwepo Yesu wangapi? na kwa nini hawakuletwa wengi ?
2. Ni kwa nini only kwa jina la yesu unafika mbinguni au unapona au kuokoka na siyo kwa jina linginelo kama la Petro, Paul, Yohana au watume wengine?

Kama unasema dawa ya Mungu haina masharti kasome habari za naaman alipoambiwa akajizamishe mto Yordani mara saba ndo apone ukoma au soma habari za kipofu aliyepakwa matope akapona.

Mungu hana fomula anapotaka kumponya mtu kwani anaweza tumia mbinu yoyote kama aliyotumia jangwani kumwambia Musa amtundike nyoka wa shaba juu ya mti na atakayemwangalia ndiye atakaye pona. sasa jiulize je ni wote waliweza kumwangalia wakati walikuwa mahututi? jibu ni hapana kwani kuna wana wa israel walikuwa na hali mbaya na hawakuweza kumwangalia nyoka na wali kufa.
Unaweza kujiuliza kwa nini nyoka wa shaba wakati kuna dawa?. Hili swali litajibiwa kwa swali la kwa nini tu huyu Babu wa Loliondo, na kwa nini huo mti tu?

Wewe kama unahitaji kupona kanywe dawa acha ubishi ambao kwa sasa hautakusaidia na hili ndilo tatizo la watanzania mtabaki ku doubt kila kitu wakati wenzenu kutoka Kenya , Uganda, Rwanda na ulaya wanapona . Mungu ameangalia uadilifu hapa kwani wangepewa watu wengine hiyo dawa ingekuwa imefika milioni.
Mwache babu wa watu aendelee na kazi yake
 
hapo kwenye bold tu nimechoka!!



muhimu kupona iwe imetoka kwa mungu ama la unachojua ni uizima kwanza. Imani bora kabisa hii!!

pole sana ndg yangu, je ukipona sasa hutakufa??????????????? "there is no free meal" aliye nyuma ya huo uponyaji lazima atavuna anachopanda , watu wakiona mambo yalivyo ovyo duniani kwa sasa wanakiri dunia imekwisha lakini ukiwaeleza ishara za mwisho wa dunia kama lisemavyo neno la Mungu" siku za mwisho kutakuwa maajabu na ishara nyingi za uongo kutoka kwa roho ya mpinga kristo" somo hilo linakuwa gumu sana. Sikiliza mwisho wa huyo babu.
 

Rudia kusoma tena! Yule mtu alipoambiwa aseme kuwa ule uponyaji sio wa Mungu ila wa Ibilisi alisema "uwe wa Mungu ama la ninachojua nalikuwa mgonjwa na sasa nimepona" hii ndo imani kuu aliyokuwa nayo!
 
Hebu ngoja tuone, hivi kumbe Mfalme Naamani yeye hakupewa masharti? Sijui bana haya mambo mie, kikubwa matendo yangu tu, the rest are details

mkuu akuna mfalme naaman huyo alikuwa amiri jeshi mkuu
 
hahahah kakutuma kakobe nini? mwambie babu anaponya aende akanywe dawa na yeye
 
mimi ninachotaka angetibu tu kwa jina la mafumba ng'wana ngikili siyo kutumia jina la mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…