Natumai wote ni wazima wanaJF wenzangu.
Well najua mengi yamesemwa kuhusu loliondo. Ila mimi ushauri wangu ni mdogo tu. Tuhakikishe tunafanya medical checkup kabla ya kwenda loliondo, ili ujijue kama unatatizo ama huna. Maana watu wengi hawana tatizo lolote la kiafya lakini wanaenda tu, sasa hiyo inakuwa ni kama kupoteza muda na pia fedha ambazo zingetumika kwa mambo mengine ya kimaendeleo zaidi. Ni hayo tu. Pia naomba mniwie radhi iwapo nitakuwa nimekosea jukwaa maana nilikuwa siona category mbadala ya kuiweka hii. Jioni njema wanajamvi
watafiti wenyewe wamesalimu amri kwa babu wa loliondo.