Mambo ya kwa Babu LOLIONDO



watafiti wenyewe wamesalimu amri kwa babu wa loliondo.
 
mmhh
hizi stori za lolliondo zimekuwa nyingi sana humu JF
na hata sielewei ..

kuna mtu ambaye anaweza kunielewesha ni nini kinaendelea huko???

tafadhali usinijibu kama huna nia ya kunijulisha
AD.....

Huko Loliondo kumetokea 'Babu' ekchuare ni Mchungaaji mstaafu wa KKKT ambaya anadai mawasiliano vere dairekti with Muumba. Basi Muumba akamuonesha (onyesha?) kuwa aina fulani (specie) ya acacia tree ina dawa kwa ajili ya yale magonjwa yasiyotibika. Akaanza kazi yake mwaka jana mwishoni around Oct. kitu kama hiyo.
Na ndicho anachofanya, kutoa kikombe kimoja cha maji yenye 'sumu' hiyo. Na imekuwa gumzo, all roads leads to Loliondo! Sikushauri uende ila nenda, boooonge la advencha!
 
Yote yanatokea kwa sababu imani haina shule, tuwaache wenye imani watwangwe vikombe. Sisi ambao hatuna imani kama tupo, tukauke!
 
Hutaamini hata nikikwambia, nilifika huko jana asubuhi saa 12 na gari niliyokuwemo ilikuwa ipo umbali wa approx. 3km toka alipotoa dawa Babu.

Kwa hizo 3km itakuchukua siku ngapi mpaka kupata dawa?
 

Many serious diseases that men are prone to, like cancer, diabetes & high blood pressure, don't cause any symptoms. Regular checkups can help diagnose these early.



It is a fact of life that most men do not bother to make an appointment to see their physicians unless they have serious symptoms (feelings of ill health). Getting a regular check up is not something that comes naturally to most men.



In fact, most men feel reluctant when sick to even admit that they are feeling ill, and only consult a doctor when they feel they have no alternative (or only if their spouse drags them to the doctor).



Unfortunately, most of the serious ailments that can shorten men's lives do not cause any symptoms until the late stages of the disease – and in many instances, men unaware that they have a disease.
 

Duuhh haya
ni wangapi wametibiwa
na wakapona kabisa?
Maana mie naona hii ni imani potofu
na huyo babu ni muongo mtakatifu..
 
Habari wandugu. Jioni hii nimeongea na waheshimiwa madiwani wa2 wa hapa jijini Arusha wakiwa safarini kutokea Loliondo kupata kikombe. Wamenijuza kwamba kwa babu kumefurika tena kwani kuna takribani magari kama mia nane. Pia wakiwa njiani kurudi Arusha, ndani ya dk 45 waliweza kuhesabu magari 347 ambayo yanaelekea kwa babu. Wao walifika Loliondo siku ya juma nne na wamefamikiwa kunywa dawa leo asubuhi. Hivyo basi kama utakuwa unakwenda leo kama ukiwahi sana utakunywa dawa siku ya juma nne.

Sikuambii uache kwenda ila ukienda ujiandae kukaa siku hizo.
 
Jamani mimi siyo mdini, ila najaribu kujiuliza kama Babu wa Loliondo ndo angekuwa mwislamu je hii dawa ingetolewa kwa wakristo? je ingetolewa kwa masharti gani? mh udhu usingetuhusu kweli???? au tungelazimika wote tuingie misikitini? Mh!!! Makafiri wangepewa kweli kikombe????? LOL.

SIPATI PICHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.

Ila kwa Babu hakuana masharti bana, bohora twende, pagani twende, hindu twende, suni twende, chadema twende, cuf twende, ccm twende, waislamu twende, wakristo twende. Mungu akupe maisha marefu babu.
 
mbona kwenye majumba yetu tunawapangisha na viwanja tunawauzia maana hii dar kiasili ilikuwa inakaliwa na waislamu kama tungekuwa na khiyana msinge kuwa na viwanja wala nyumba za kupanga ktk hili jiji.
 
mbona kwenye majumba yetu tunawapangisha na viwanja tunawauzia maana hii dar kiasili ilikuwa inakaliwa na waislamu kama tungekuwa na khiyana msinge kuwa na viwanja wala nyumba za kupanga ktk hili jiji.

Let's be realistic
 
Kwa kipindi kifupi,Mchungaji mstaafu wa KKKKT ameweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na 'kutibu' magojwa sugu yaliyoshindikana hospitalini kwa kutumia 'dawa' itokanayo na kuchemsha mizizi na majani pamoja na imani.

Serikali 'imebariki' tiba hiyo kwa ama kukataa kuifungia isitumike kwa sababu haijathibitishwa kitaalam au kwa kutoa vyombo vya ulinzi kumlinda 'babu', dawa zake na wanaoenda pale kupata 'tiba'.

Sipingani na wale wanaoenda pale kupata huduma hii ya kiimani lakini wasiwasi wangu upo pale itakapo gundulika si tiba wala lolote,je serikali itachukua hatua gani.

Je kama ni tiba kweli ba watu wakapona,serikali itafanyaje kuhakikisha watu wengi zaidi wanaipata.

Kubwa zaidi ni je kwakuwa dawa hii ina nguvu kubwa ya kiimani kwa Mungu, siku mchungaji huyu akisema 'ameoteshwa' na Mungu kuwa wale wote walioenda kwake na kupata dawa kisha kupona wanatakiwa kurudi kwake wakiwa sh laki moja na asiyefanya hivyo atakufa ndani ya siku kadhaa, wewe na serikali mtafanyaje?

Najaribu kuona kitu kama hicho kinaweza kutokea, hii ni imani na fumbo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…