Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Jana liianzisha hii topic wakubwa wakaifunga naona leo nguvu ya umma inafanya kazi imeanzishwa tena.
 
Hivi bado watu wanaenda kwa kakobe
 
imani yako itakuponya ila kama una imani haba usiende kwa babu plez ni wastage of time.
 
Originally Posted by Masanja
Hizi zote ni ishara za watu waliokata tamaa na maisha! We fail to invest in better infrastructures, health services, education, roads...etc for our children..na tunaanza kukimbilia Loliondo kutafuta dawa za kututibu ukimwi na kansa! Ama kweli! Umasikini ni kitu kibaya. Lakini ni kibaya zaidi kama ni umasikini wa fikra. I only wish tungekwenda Loliondo kukomboa mbuga yetu aliyogawiwa yule mwaraabu...perhaps angetupa kodi zaidi tukajenga ile barabara ya Arusha-Loliondo!

Kama mnabisha kwamba watanzania tumekata tamaa na maisha angalia vitu kama DECI vilipoingia hata wakubwa wa serikalini waliiba kodi zetu wakaenda 'kupanda mbegu' sijui leo DECI iko wapi...mifano ni mingi jamani

Ushauri wangu kwa watanzania wenzangu: Mafanikio hayana short cut. Huwezi kupata utajiri simply kwa kwenda kwa mganga! work hard and bit of 'luck' money will come. Ni kupenda hivi vitu vya mkato mkato ndo tunazidi kuwa masikini. Unalala..usiku asubuhi unataka uendeshe Lexus! Unless uibe utaipata wapi? Mwanafunzi anashindwa kusoma shule anataka mganga amsaidie kufaulu mtihani! Tunawanyima haki wanachi wetu na kupeleka hela zote uswisi huku wachache wakiishi maisha ya peponi...harafu unakuta hao hao wanasimama kwenye majukwaa wakitwambia twende kanisani kuombea amani ya nchi! Kuna watu wanatufanya tuone kwamba umasikini ni mapenzi ya Mungu kitu ambacho si kweli. Kikwete anaona kabisa DOWANS wanatuibia na wale wahusika kashindwa kuwawajibisha...they have swindled billions in our name....Kikwete huyo huyo anasimama mbele ya TV anatwambia kwamba matatizo ya umeme yanatokana na kazi ya 'Mungu' kwa sababu mvua haipatikani. Twende kanisani/msikitini tukaombe mvua inyeshe tupate umeme!

I Masanja, I refuse to believe in this! Hardwork, determination and discipline will liberate you! I say and I do! Amen!

Wewe unaelewa unajibu kuhusu nini? Watu wanaenda kupata matibabu kwa maradhi ambayo bado yanasumbua tiba yake. Wewe umeng'ang'ana na uvivu wa watu kufanya kazi. Au wewe ndio umekasirika kwa kuwa hiyo sio dawa ya kuleta utajiri? Elewa mada inayozungumziwa.
 
Ni kweli kwamba mgonjwa yeyote pamoja na wanaomjali hujaribu kupata tiba yoyote na kwa namna yoyote ili kutibu gonjwa linalomsumbua mgonjwa na jamii yake. Hata kama uwezo wa tiba hiyo haijathibitishwa, bado itatumika tu. Desparation inaweza kumfikisha mtu mzima na akili zake katika situations za ajabu kama simulizi za huko Loliondo.

Wiki mbili zimepita sasa tangu ndugu yangu mmoja yalipomkuta mikasa katika hospitali kubwa tu, Dar es Salaam. Katika hospitali ya kwanza alipewa rundo la mividonge baada ya kudundwa pia sindano nne za kuzuia maumivu na kutapika. Maabara wakasema iko malaria mbili.
Ilipobidi kwenda kwingine baada ya mgonjwa kuzidiwa, na pale wataalamu wakafanya mavipimo yao na kugundua malaria moja pamoja na kitu ingine, ati labda utumbo umejikunja!!! Very contradictory. Hospitali ya tatu (in 36 hours) hata kabla ya kufanya vipimo wakataka kumdundika QUININE 9 based on lab report ya wengine! Baada ya kukataa hayo na kusisitiza vipimo kamili, mgonjwa akakutwa hana malaria hata chembe moja ila alihitaji kuongezewa maji mwilini, kwa maana ilikuwa case ya dehydration!!! Huduma mbovu kama hizi haziwezi kuwa pendeleo la mgonjwa yeyote. Na hii ndo hali halisi unless upo uwezo wa kwend kwa makaburu pale Trauma Centre.

Ya Loliondo yawezekana kabisa kuwa siyo kipimo cha watu kujazwa UJINGA bali ni kile cha watu kukata tamaa na huduma mbovu katika nyanja mbalimabali.
Rundo la watu wanaomiminika kwa matumaini kwenda Loliondo si tukio la kwaida hata kidogo. Nini mindset ya watu wote hao kufuata NENO tu?
Je inawezekana ku-speculate kwamba ni matokeo ya kukata tamaa baada ya miaka 50 ya ubabaishaji wa mijizi ya MAFIA waliomo ndani ya CCM? Leo hii yule Babu mchungaji akiibukia kunadi sera za CDM kama dawa ya matatizo mengine ataitwa mhaini?

hii mada ina mantiki, haiwezekani watu wasafiri kutoka sehemu mbalimbali kukimbilia dawa ya mtu huyu, hii inaonesha dhahiri watu wamekata tamaa na huduma mbovu zitolewazo katika hospitali zetu
 
Gari mali ya Shirika la Umma ndani ya Loliondo, hatuna hakika hii gari ilikuwa na mahusiano gani na uwepo wake kule. Shirika linalomiliki hili gari linatakiwa kutoa maelezo. Pesa za walala hoi zinatumika kulihudumia hili gari lakini hiyo pesa haikupaswa kutumika kama inavyoonekana pichani. We need maelezo.

PICHA+MAGARI.JPG
 
well,kwani hata msanii wa ukweli si alienda huko?kwani hujui?alijidai ameenda kukagua nyayo za watu wa kale!sasa cha kushangaza mbona hakwenda siku zote hizo?mama wa msanii wa ukweli akajiona mjanja kuvaa ijabu ila wajanja wakamwona!watu kibaooooo huko
 
people are so desperate towards their own created problems, and because of desperation no one who is taking any critical analysis of the event. why cant we take time and analyse the event in logical way that other can get the concept and understand rather than pouring brabra all the way
 
kunywa dawa arifu ka iman ipo kwel hapo nimewakubal
 
kama rais wa nec mwenyewe anasema mfumuko wa bei za vyakula utategemea na kudra za mwenyezi mungu kuleta mvua sasa ni kwanini mtawaliwa asitegemee kudra za babu kupona
 
Wiki mbili zimepita sasa tangu ndugu yangu mmoja yalipomkuta mikasa katika hospitali kubwa tu, Dar es Salaam. Katika hospitali ya kwanza alipewa rundo la mividonge baada ya kudundwa pia sindano nne za kuzuia maumivu na kutapika. Maabara wakasema iko malaria mbili.
Ilipobidi kwenda kwingine baada ya mgonjwa kuzidiwa, na pale wataalamu wakafanya mavipimo yao na kugundua malaria moja pamoja na kitu ingine, ati labda utumbo umejikunja!!! Very contradictory. Hospitali ya tatu (in 36 hours) hata kabla ya kufanya vipimo wakataka kumdundika QUININE 9 based on lab report ya wengine! Baada ya kukataa hayo na kusisitiza vipimo kamili, mgonjwa akakutwa hana malaria hata chembe moja ila alihitaji kuongezewa maji mwilini, kwa maana ilikuwa case ya dehydration!!! Huduma mbovu kama hizi haziwezi kuwa pendeleo la mgonjwa yeyote.

utata wa watanzania wengi unakuja kwa kujidai ujuaji wa kila kitu!hawaheshimu profession.mgonjwa anaweza kukataa dawa kisa vipimo ni -ve bila kujua kwamba vipimo ni kipengele tu katika matibabu ya mgonjwa.nawashauri muwe mnauliza kwa nini mhudumu wa afya anakufanyia kitu flani na sio kujiamulia kivyakovyako.
'Ujuaji' huu unasababisha watu kuingizwa mkenge kama ule wa loliondo.
 
Naye (yule aliyekuwa Kipofu) akajibu: "Kama ni mwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu na sasa naona." I like it that way, but don't forget we're dealing with 'The Sword of Jesus' or in swahili: 'Panga la Yesu', sasa Yesu na Panga wapi na wapi? Au ni 'Mujaheedina wa Yesu'?
 
Amini usiamini sio kwamba wote wanaokwenda huko wako desparate coz ya huduma mbaya za hospitali zetu.

Sio vizuri kutaja majina lakini wamekwenda viongozi wakubwa wa nchi hii ambao hutibiwa nje kwa kodi zetu. Jamaa wamechagua
kwenda Loliondo baada ya USA, UK, India, Canada etc believe it. Inasemekana huyo mchungaji dawa yake inatibu hata magonjwa
sugu yasiyotibika kwa modern medicine kama UKIMWI, KISUKARI, Hupertension, Cancer etc. Wiazara ya afya sasa hivi imetuma
watalaamu wa National Institute for Medical Reserach (NIMR) kwenda kuifanyia utafiti dawa hiyo kwa kuanzia kwa ku-prove kama
kweli inaponyesha magonjwa hao.

It is really a serious thing kwa hapa Tanzania. Kuna wahindi kutoka India wapatao 200 wameombe VISA ya kuingia TZ kwaajili
ya kwenda Loliondo kupata hiyo miracle medicine, It is a medical panacea kama kweli inafanya kazi kama wanavyosema
wenyewe waliowahi kutibiwa na dawa hiyo.

Sasa hivi ukifika Loliondo kabla ya kumuona Mchungaji na kunywa hiyo dawa unaweza kuchukua kati ya weeks 3-4 kabla hajupata dawa.
Tatizo la dawa hiyo ni lazima uinywee hapo hapo ukiipeleka nje na hapo haiponeshi tena. Kuna wagonjwa kibao sasa wanatolewa mahospitalini
na kupelekwa Loliondo. Wengine wanakufa kabla ya kumuona na kunywa hiyo dawa kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa walioko kwenye
foleni ya kusubiri.

Bei yake TSH 500/= TU
 
Mimi sidhani kama kuna tatizo kama watu wanapona, na inaonekana kabisa kweli kuna nguvu ya Mungu..
 
mhu jamani michuzi kaweka eti karibia watu saba wameshakufa sababu wamepelekwa wakiwa mahututi,pia msongamano ni mkubwa kupita kiasi,mi naona serekali ingeingilia kati kusaidia watu na huyo mzee,sasa wiki mbili hujamuona babu na watu wanazidi kwenda si balaa hilo,Mungu ambariki huyo babu azidi kusaidia watu,mi naona watu kama wamechelewa kweli iyo dawa sio kwamba kwasasa itabidi idairudiwe ili iweze kutosha?aya we... ya Dunia mengi mara mabomu, mara babu roliondo,story haziishi.......
 
Back
Top Bottom