Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Aleluyah!

Nimekuwa nikitafakari sana kuhusu huyu Babu wa Loliondo na nguvu alizo nazo za kuweza kuponya maradhi mbali mbali ambayo ni sugu hapa duniani. NIkianza kutafakari neno la Mungu ambalo linasema siku za Mwisho watakuja Manabii wa uongo soma Mathayo sura yote ya 24.

Nimeona watumishi wengi wa Mungu ambao wamekuwa wakitumia Neno la Mungu kufunika matendo yao magumu na ya kichawi tukiambiwa kuwa hawa ni watu wa Mungu. Lakini baada ya Muda imedihirika kuwa ni nguvu za kishirikiana zimekuwa zikitumika. Utakumbuka kuwa Paulo alimtoa pepo mama mmoja ambaye alikuwa ni mjakazi wa mtu ambaye kwa kutumia hilo pepo lake la utambuzi alikuwa akitumika kuagua watu na Mabosi wakewalifaidika sana kimapato kwa kumtumia yeye ingawa yeye alikuwa hafaidiki zaidi ya kuwa mjakazi, na pale paulo alipolikemea na kutoka ikawa ndo mwisho wa mambo ya utabibu wake.

NI kweli nina uhakika kuwa Huyu alikuwa ni Mchungaji kule Imiti babati na leo hii amepewa nguvu za kuweza kutibu magunjwa kwa kutumia dawa ya mizizi. Sasa swali langu ni kitu gani kinachozuia yeye kufanya kazi sehemu nyingine yoyote nje ya eneo lake, je ni kwaninini hiyo dawa lazima akupe yeye kwa mkono wake mwenyewe?
Hii inanipa nafasi ya Kumtafakari pia Mtumishi mwingine aliye kuwa Mchungaji na baada ya kwenda Huko NIgeria na kurudi alirudi na upako wa ajabu sana amabo akikunyooshea mkono tu unaanguka na aliponyesha watu wengi sana lakini siku za hivi karibuni amepoteza umaarufu wote baada ya kujulikana kuwa natumia nguvu za giza kutekeleza hayo yote.

Leo hii natafakari jinsi watu wanavyo kwenda kwa wingi kutoka mikoa yote ya Tanzania na nje ya Tanzania sehemu ambayo haina miundo mbinu na si ajabu leo ukasikia magonjwa ya mlipuko huko Loliondo. Jana nimepewa taarifa kuna Msafara wa magari km 50 wanasubiri huduma hiyo.

Mimi sitaki kumkani huyu babu kwamba yeye ni wa Mungu lakini Neno la Mungu linasema tuzipime hizo roho.

rai yangu watu wa Mungu nisaidieni niweze fahamu ninyi ambao mmesha zipima hizo roho je ni kweli huyu ni mtu wa mungu na siyo anasaidiwa na Mizimu ya mahalia na ndiyo sababu hawezi amishia huduma yake sehemu nyingine? Na hivyo mizimu hii imekuja kwa Sura ya Malaika wa Nuru.

Nisaidieni kwani mimi ni mchanga kwenye Imani nahitaji msaada. Wasi wasi wangu isije kuwa tunakwenda kwa Mganga wa Kienyeji tukuifikiri ni mtu wa Mungu, yaani nalataka ni watu wajue kuwa ile ni nguvu ya Mungu au la ingawa inaponya.

Nawasilisha
Mungu awabarikLi sana!

Sina maelezo ya kukusaidia zaidi ndugu yangu ingawa mie kama wewe nimeombea jambo hili ili kupata mafunuo zaidi usiku mmoja. Na Roho kwa namna ya ajabu usiku ule alinielekeza katika Zaburi 34 (please read na uamue). Unajua wanadamu tumeteseka sana na magonjwa ya kila aina na sasa baada ya Babu kutokea tunaona ndiyo pumziko limekuja kimsingi hakuna anayehoji sana kwani the driving force ni kupona na kuwa HURU. Ila neno linasema zijaribuni ROHO hiyo ndiyo caution yangu.
 
ndugu watu wanye matatizo wapo wengi sana, alafu watu wanabeza eti haiwezekani, hivi kuna kitu kinachomshinda YESU....?? matokeo yake hadi maustaadhi watu wangu wameenda kwa imani watapona na wamerudi kuwashuhudia wenzao, ukienda huko hadi helkopta za matajiri wa kiarabu zinaenda....Kama unamatatizo nenda acha ubishi usio na maana by the way yeye mchungaji a.k.a babu hana anachopungukiwa, hakutangaza magazetini wala redioni ila watu wenyewe wamekua wakiwashudia ndugu zao.....

to god b the GLORY

Maajabu ni kwamba, unakunywa kikombe kimoja cha tu cha dawa ambacho ndo kinagharimu Tshs. 500 tu....na mara moja dawa inaanza kufanya kazi. Uruhusiwi kunywa mara mbili..... KWELI DUNIA IMEPETA MKOMBOZI.... TUSUBIRI MPAKA WAZUNGU TOKA ULAYA WATAKUJA...NGOJA TUONEE.!!!!!!!!

Aleluyah!

Nimekuwa nikitafakari sana kuhusu huyu Babu wa Loliondo na nguvu alizo nazo za kuweza kuponya maradhi mbali mbali ambayo ni sugu hapa duniani. NIkianza kutafakari neno la Mungu ambalo linasema siku za Mwisho watakuja Manabii wa uongo soma Mathayo sura yote ya 24.

Nimeona watumishi wengi wa Mungu ambao wamekuwa wakitumia Neno la Mungu kufunika matendo yao magumu na ya kichawi tukiambiwa kuwa hawa ni watu wa Mungu. Lakini baada ya Muda imedihirika kuwa ni nguvu za kishirikiana zimekuwa zikitumika. Utakumbuka kuwa Paulo alimtoa pepo mama mmoja ambaye alikuwa ni mjakazi wa mtu ambaye kwa kutumia hilo pepo lake la utambuzi alikuwa akitumika kuagua watu na Mabosi wakewalifaidika sana kimapato kwa kumtumia yeye ingawa yeye alikuwa hafaidiki zaidi ya kuwa mjakazi, na pale paulo alipolikemea na kutoka ikawa ndo mwisho wa mambo ya utabibu wake.

NI kweli nina uhakika kuwa Huyu alikuwa ni Mchungaji kule Imiti babati na leo hii amepewa nguvu za kuweza kutibu magunjwa kwa kutumia dawa ya mizizi. Sasa swali langu ni kitu gani kinachozuia yeye kufanya kazi sehemu nyingine yoyote nje ya eneo lake, je ni kwaninini hiyo dawa lazima akupe yeye kwa mkono wake mwenyewe?
Hii inanipa nafasi ya Kumtafakari pia Mtumishi mwingine aliye kuwa Mchungaji na baada ya kwenda Huko NIgeria na kurudi alirudi na upako wa ajabu sana amabo akikunyooshea mkono tu unaanguka na aliponyesha watu wengi sana lakini siku za hivi karibuni amepoteza umaarufu wote baada ya kujulikana kuwa natumia nguvu za giza kutekeleza hayo yote.

Leo hii natafakari jinsi watu wanavyo kwenda kwa wingi kutoka mikoa yote ya Tanzania na nje ya Tanzania sehemu ambayo haina miundo mbinu na si ajabu leo ukasikia magonjwa ya mlipuko huko Loliondo. Jana nimepewa taarifa kuna Msafara wa magari km 50 wanasubiri huduma hiyo.

Mimi sitaki kumkani huyu babu kwamba yeye ni wa Mungu lakini Neno la Mungu linasema tuzipime hizo roho.

rai yangu watu wa Mungu nisaidieni niweze fahamu ninyi ambao mmesha zipima hizo roho je ni kweli huyu ni mtu wa mungu na siyo anasaidiwa na Mizimu ya mahalia na ndiyo sababu hawezi amishia huduma yake sehemu nyingine? Na hivyo mizimu hii imekuja kwa Sura ya Malaika wa Nuru.

Nisaidieni kwani mimi ni mchanga kwenye Imani nahitaji msaada. Wasi wasi wangu isije kuwa tunakwenda kwa Mganga wa Kienyeji tukuifikiri ni mtu wa Mungu, yaani nalataka ni watu wajue kuwa ile ni nguvu ya Mungu au la ingawa inaponya.

Nawasilisha
Mungu awabarikLi sana!

Amepewa kwa neema na anatoa kwaneema.

Yawezekana walengwa walikuwa ni majirani zake wa kipato cha chini...

Mungu amzidishie ili kila mtu aweze kuaford matibabu..
Big up babu!

kwa kusoma hizi replay zenu nashindwa hata kumalizia thread yote...... Coz sijapata kuona mawazo yaliokaa kushoto kama hayo hapo juu
 
Kwa hiyo wachawi wanashauriwa wasiende?.......kuna mzee mmoja hapa mtaani anasadikiwa kuwa ni mchawi sana na anampango wa kuelekea huko kwani ana kisukari tumshauri asiende?........................
Ila watu waache kucheza na babu jamani........................tumwogope mungu tafadhari!
 
we sema karama za Mungu haziuzwi, haziuzwi kwa hiyo shilingi mia tano 500, sasa sijui kinachoendelea hapo. mi yangu macho....nitaona hii issue inaishia wapi, kwasababu kama ni jambo la Mungu litaishia kuzuri, lakini kama ni jambo ambalo si la Mungu litaishia kubaya sana.
 
Kwa hiyo wachawi wanashauriwa wasiende?.......kuna mzee mmoja hapa mtaani anasadikiwa kuwa ni mchawi sana na anampango wa kuelekea huko kwani ana kisukari tumshauri asiende?........................
Ila watu waache kucheza na babu jamani........................tumwogope mungu tafadhari!

Heshima kwako Jile79,

Mkuu anaweza kwenda lakini mshauri kwanza aachane na uchawi vinginevyo anaweza kuumbuka sana.Naomba nisisitize kwamba kama umetupiwa kitu kibaya kwa Babu ni mahali pake haswa.
 
Mimi nina sumbuliwa na pressure ( hypertension) pamoja na kisukari ( type 2 Diabetes) kwa mwaka wa pili sasa! nimekunywa dawa za hospitalini na za kienyeji adi 'nimetosha' natamani sana kwenda kwa babu lakini 'kaburu' ananyima ruhusaa sasa nafikiria ku resign kazi ili niende kupata matibabu kwa babu ila nasita kidogo kwa maana sijapata uthibitisho wa mtu yoyote ninaye mjua aliye pona, hivyo kama kuna JF member yoyote aliyekuwa na tatizo kama langu akaenda kwa babu kupata kikombe akapona kabisaa naomba ata ani PM ili nianze 'Plan B' ya ku resign ndani ya wiki hii
 
Umeenda mbali sana, kumwekea sumu ili afe,.... hapana.

Mkuu wala sijasema watamwekea sumu ili afe yeye,, hapana,, sumu inaweza kuwekwa ili watu wafe iwe kama kibwetere na hivyo kum disqualify. Huo ni wasiwasi wangu tu,, ila naomba aweke ulinzi mkali kwenye dawa yake
 
Bango waliopona mkuu,
Babu kajificha loliondo ndani ndani.
Barabara ya kwenda kwake mbofu ile mbaya, wamemvumbua wagonjwa wa magonjwa sugu walio pona!
Na hao ndio bango la babu,
Babu hana cha kwenda ch 10 au star TV kama akna Ndodi yeye ni huko kijiji cha mbali

asavali umempa jibu sahihi
 
Watu, ambao wanaaminika kuwa na akili vichwani wanahoji kwanini auze dawa hiyo kama ni maono ya Mungu!!!...
Mi kwa hasira nitawaita hawa wote wa jamii hii kuwa ni WAPUMBAVU!...unategemea mtu huyu ataoperate namna gani kutoa dawa kwa watu wa dunia yote, then asipate hata mkate wa shs.500, na kisha afe kwa njaa?
Mbona wahubiri wanaojiita manabii, wapakwa mafuta, mitume na majina meengi ya kujitukuza, mbona wanapokea fedha nyingi sana za sadaka toka kwa waumini wao, kwanini wanamwonea wivu babu kuchangisha siing 500 tu?

Sasa mtu atatoa huduma hiyo BURE, kwa muda gani, maana huduma hii inaonekana itakuwa ya kudumu!
Walalamishi hawa wamepoteza heshima mbele ya jamii, maana wanaonekana wamejaa wivu sana kwa babu!

Wataendelea kusema sana, lakini dawa inatolewa, inaponya, na mwishowe wenyewe watashuka kwenye madhabahu zao na kwenda kutibiwa!

Mkuu umenigusa!
Mtu yuko bize masaa yote halimi, hafugi, haimbi atakula nini!?
tena hta hiyo 500 hachukui yoote, anapata 200tu. Duniani wapingaji(makafiri) hawakosekani..achana nao...
Yule mzee ni wa kuombewa,...........hivi kuna mtu amesema anatamani sana kwenda kwa babu lakini hana sh500!! watu bwana!
 
Kwa nyomi lile unafikiri watamtakia mema babu????????? yule mzee balaaa...halafu hata hawajibu..:bump2:
 
namfaham sana . ndio wanamzika sasa hivi .
 
Hawa sasa nado wapinga kristo wenyewe hao,watapotosha umma kwa faida zao wenyewe............huyu ni mojawapo
 
Mkuu hiyo ndiyo naisikia toka kwako....ila nimesikia mengi ya ajabu toka kwa babu wa loliondo..kama vile walioiba furishi la mahela yake kuvamiwa na kundi la nyani wakakimbia hadi kujisalimisha kwa babu nasikia yeye akawasmehe ila polisai wakawang'ang'nia...
Lapili ni polisi aliepokea rushwa toka kwa mama mmoja shs50,000/= mchungaji akamshtukia, akamwambia arudishe, polisi akakana, mara polisi akajisikia kikohozi akakohoa ile 50,000/= ikatoka...
Kifupi ukienda kwa babu jitahidi uwe mtu mwema la sivyo yata kukuta mabaya mno!
 
naamini watz wengi tunaendeshwa na matukio, yani pamoja na changamoto nyingi sana tulizo nazo tayar watu wamesahau wame-concentrate kwenye tukio la Loliondo huku bado mgawo wa umeme ukiendelea kutukamua, ya Dowans bado ni kizungumkuti, katiba mpya serikali wamehodhi hoja na watu wamekaa kimya, maisha yanazid kuwa magumu bidhaa ni bei juu mno................................watz tusiendeshwe na matukio yasiyo ya msingi tukasahau hoja zinalolitafuna taifa
afya kwanza mambo mengine badae
 
Mkuu hiyo ndiyo naisikia toka kwako....ila nimesikia mengi ya ajabu toka kwa babu wa loliondo..kama vile walioiba furishi la mahela yake kuvamiwa na kundi la nyani wakakimbia hadi kujisalimisha kwa babu nasikia yeye akawasmehe ila polisai wakawang'ang'nia...
Lapili ni polisi aliepokea rushwa toka kwa mama mmoja shs50,000/= mchungaji akamshtukia, akamwambia arudishe, polisi akakana, mara polisi akajisikia kikohozi akakohoa ile 50,000/= ikatoka...
Kifupi ukienda kwa babu jitahidi uwe mtu mwema la sivyo yata kukuta mabaya mno!

Hapo kwenye red fafanua please Ilitokea wapi??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
 
We vipi kweli afya kwanza bwana!!! utafaidi vipi umeme wakati una kaukimwimwi kamekulaza chali?
 
Back
Top Bottom