Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 3,135
- 3,392
Jipeni moyo tu ,ooh Hiyo ni damu ya yesu-mtishamba ni damu ya yesu. mauti inawakaribia taratibu poleni sana enyi wenye shingo ngumu.
Mnashindwa kumtafuta mungu wa kweli awafunulie ju ya hiyo huduma,mmekezana tu kibabu,jamani sio nguvu ya mungu,ni roho nyingine hiyo. watu wataanza kufa taratibuuuu!
Mauti hayatakuja kwa wanaopata dawa kwa babu tu. Hata wanaopata hospitalini na hata wasioumwa kabisa labda mimi na wewe, wote tutafikia umauti...
Lakini kwanini watu wamelivalia njuga jambo hili? Kuna anayelazimishwa kwenda?
Au wasioenda ndio wasafi sana kiroho?
Na nani ametupa mamlaka ya kuhukumu?
Je kuna muumini anayelewa kila kitu JINSI Mungu anavyojidhirisha na kutenda kazi zake?
Ni kweli imeandikwa kuwa Shetani anaweza kugeuza GIZA ionekane kama NURU, na je wewe unayefikiri upo kwenye NURU una uhakika gani kwamba hiyo NURU sio GIZA lililogeuzwa?
Mimi nafikiri kwa vile hakuna aliyeshurutishwa kwenda hamna haja ya kucharurana kiimani hapa jamvini. Wanaotaka kwenda waende, wasiotaka waendelee na taratibu zao za ibada na maombi mbalimbali, huku wakiwaombea walioenda na wasioenda.