Mambo ya msingi kujua kabla hujaingia kwenye forex trading

Mambo ya msingi kujua kabla hujaingia kwenye forex trading

sele255

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2016
Posts
205
Reaction score
262
MAMBO YA MSINGI KABLA YA KUINGIA KATIKA FOREX TRADING

Ajira ni changamoto na tatizo linalokuwa siku hadi siku.Miongoni mwa vijana na watu wengi wamejiingiza katika biashara ya forex.JE HII AJIRA INALIPA?.Jibu langu ni NDIO na vile vile HAPANA.

Kwa wasiojua maana ya Forex trading, hii ni biashara inayohusisha ubadilishani wa pea za shilingi mfano EUR/USD ,USD/TSH n.k .Utaratibu unaotumika ni kwamba unanunua shilingi fulani na kuiuza thamani yake inapoongezeka.Hii inachangia uchumi unabadilika badilika kila nukta.

Vijana wengi wameingia kwenye hii biashara kwa ushawishi wa kupata pesa kwa muda mfupi.Matokeo yake wengi wao wameishia kupoteza pesa zao.Ni kweli kabisha biashara ya forex inalipa ila tu ukiifanya kwa malengo na utaratibu.Tuzungumzie mambo ya msingi kabla ya kuanza kufanya forex trading.

1.ELIMU ELIMU ELIMU
Hii ndio sehemu ya msingi,pata elimu ya kutosha kuhusu forex.Baadhi ya vijana wamegeuza fursa kwa kuwafundisha elimu ya forex kwa kutoza pesa,elimu ambayo inatolewa bure kabisa.Kwa mtazamo wangu haifai kulipia mtu akufundishe forex,kuna vitabu vingi sana na online courses zinazofundisha forex trading.Kabla ya kuanza trading hakikisha umeelewa kila kitu kuhusu forex trading.

2.AKAUNTI YA MAJARIBIO
Baada ya kupata uelewa wa kutosha kuhusu forex, kinachofuata ni kutafuta trial account kwa kufanya majaribio.Ukiweza kutengeneza faida kwenye trial account ndio weka pesa uanze kufanya biashara.

3.CHAGUA BROKER WA UHAKIKA
Biashara zote za fx zinafanyika kupitia brokers. Hapa chagua broker wa uhakika ambaye anakidhi vigezo vyako.Ukichagua broker asiye wa uhakika lazima ujutie kujua forex trading. Angalia vitu kama anatoa leverage zipi? Je ana stop loss? Minimum deposit/withdrawal? Anatoa education about forex? Je ana social trading?.

4.MTAJI
Mwisho kabisa,forex trading inahitaji uwe na mtaji kuona faida.Unaweza anza na mtaji mdogo, ila kuona faida kubwa labda utumie leverage. Mtaji mkubwa kwenye forex ndio utaona matunda yake.

Ushauri wangu kwa vijana ,fx sio biashara ya kukariri na usitegemee anayekufundisha atakufanya upate faida kubwa.Suala ni kupambanua mawazo yako,soma vitabu ,pata ushauri na pia jaribu vitu vipya.Usipozingatia hayo forex itakuwa kama moto kwako.

Kwa habari na taarifa za ujasiriamali ,jiunge nasi kupitia telegram ,kupitia link hapo chini
UJASIRIAMALI
 
Nakubaliana na wewe vitu vingi hapo ulivyoorodhesha lakini hiyo ya kwanza Mmmh nina mashaka nayo, kwa sababu kwenye forex kusoma peke yake hakutoshi mkuu unaweza kusoma sana lakini usipopata mtu aliekuzidi ambae atakua kama guider wako au mentor utapata shida sana kutoboa kwenye hii business.

Unaweza kusoma sana vitabu na ukashidwa kutoa hiyo elimu kwenye kitabu ukaipeleka kwenyw chart kujua hapa nafanyaje. ni hayo tu lakini MENTOR MUHIMU la sivyo utaunguza mpaka uje kusema ni SCAM[emoji38] [emoji38] [emoji38] .
 
Ni sawa Mkuu, ndio maana nikasema baada ya Elimu nenda kwenye account ya majaribio

Yaani ifikie kipindi usimame peke yako bila kutegemea mentor
 
1.ELIMU ELIMU ELIMU
Hii ndio sehemu ya msingi,pata elimu ya kutosha kuhusu forex...........,kuna vitabu vingi sana na online courses zinazofundisha forex trading.......
Naomba recomendation japo ya viatbu bora viwili tu. Nitavitafuta na kushare na wana JF wengine hapa jukwaani.
2.AKAUNTI YA MAJARIBIO
Baada ya kupata uelewa wa kutosha kuhusu forex, kinachofuata ni kutafuta trial account kwa kufanya majaribio.Ukiweza kutengeneza faida kwenye trial account ndio weka pesa uanze kufanya biashara.
Hapa vijana wengi wanakosa subira ya kutumia demo kwa muda mrefu, Inashauriwa angalau utumie demo si chini ya miezi mitatu, Na ndani ya huo uda angalau uwe umeweza kuikuza account yako angalau mara tatu.
3.CHAGUA BROKER WA UHAKIKA
Biashara zote za fx zinafanyika kupitia brokers. Hapa chagua broker wa uhakika ambaye anakidhi vigezo vyako.Ukichagua broker asiye wa uhakika lazima ujutie kujua forex trading. Angalia vitu kama anatoa leverage zipi? Je ana stop loss? Minimum deposit/withdrawal? Anatoa education about forex? Je ana social trading?.
Hapa wengi hawajui ni vigezo vipi hasa watumie katika kutafuta broker, Wengi huchagua broker kutokana na kusikia kwa flani au kutokana na tangazo fulani bila hata ya kuwa na vigezo stahiki vya kumfanya achague huyo broker aliyechagua.
Kwa nza inatakiwa mtu awe na ABCs za broker bora na achague vigezo vyake.
Pili anaweza tumia hii link: Forex Brokers Comparison kuweza kufanya chaguo sahihi la broker.
4.MTAJI
Mwisho kabisa,forex trading inahitaji uwe na mtaji kuona faida.Unaweza anza na mtaji mdogo, ila kuona faida kubwa labda utumie leverage. Mtaji mkubwa kwenye forex ndio utaona matunda yake.
Mtaji mkubwa au mdogo sio kigezo cha kupata mafanikio katika forex hilo moja.
Matunda ya FX yanatokana na umahili wako katika kutunza / kulinda mtaji wako, uwe mkubwa au mdogo. Hili ndio linawaliza wengi, Wanafikiria faida zaidi, badala ya kufikiria hasara (Calculated risk) kwa kila position anayo ingia, Hapo ndipo LOT size inatakiwa itumike vyema kulingana na account size yako.
Kwenye hii picha hapa chini angalia Lot size, Angalia Margin level, na angalia idadi ya position.
upload_2018-2-26_5-27-34.png

Ushauri wangu kwa vijana ,fx sio biashara ya kukariri na usitegemee anayekufundisha atakufanya upate faida kubwa.Suala ni kupambanua mawazo yako,soma vitabu ,pata ushauri na pia jaribu vitu vipya.Usipozingatia hayo forex itakuwa kama moto kwako.
Hakika ushauri mzuri.
 
Nakubaliana na wewe vitu vingi hapo ulivyoorodhesha lakini hiyo ya kwanza Mmmh nina mashaka nayo, kwa sababu kwenye forex kusoma peke yake hakutoshi mkuu unaweza kusoma sana lakini usipopata mtu aliekuzidi ambae atakua kama guider wako au mentor utapata shida sana kutoboa kwenye hii business.
Unaweza kusoma sana vitabu na ukashidwa kutoa hiyo elimu kwenye kitabu ukaipeleka kwenyw chart kujua hapa nafanyaje. ni hayo tu lakini MENTOR MUHIMU la sivyo utaunguza mpaka uje kusema ni SCAM[emoji38] [emoji38] [emoji38] .
Hapa ni uwezo wako tu mkuu. Usijitumie wewe kama reference ama si unit ya wengine. Kwa waliopiga msuli yatima advance kawaida sana
 
Kabisaa mimi mwenyewe nilianza bila mentor na Mambo yanaendaa tuu...
Soma somaa,,,open demo account practice it ukiona waanza pata faida with demo ..ingia real account....
 
Ingia Babypips.com

Hautakuwa na haja ya Kutafuta Mentor kabisaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hoja ilikuwa ni kitabu/ vitabu. Rejea mtiririko wa convo hapo juu.

Sio muda wote ni wa ku_trade

Ule muda unasubiria setup basi unakuwa unapata mawili matatu toka kwenye kitabu /vitabu.
 
Hoja ilikuwa ni kitabu/ vitabu. Rejea mtiririko wa convo hapo juu.

Sio muda wote ni wa ku_trade

Ule muda unasubiria setup basi unakuwa unapata mawili matatu toka kwenye kitabu /vitabu.
Noted
 
Back
Top Bottom