Mambo ya msingi yaliyowasukuma Lisu na Mbowe kuwania Uenyekiti Taifa wa CHADEMA

Mambo ya msingi yaliyowasukuma Lisu na Mbowe kuwania Uenyekiti Taifa wa CHADEMA

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Great Thinkers,
Nimerejea hotuba za wagombea wawili wa nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA, Haya ndiyo mambo ya msingi ambayo kila mgombea ameyatabainisha kama sababu zilizomsukuma kuwania nafasi hiyo. Kwa ambao ni wapambe ama wapiga kampeni wa kambi hizi, mnaweza kuja na uchambuzi wenu iwapo mgombea wenu hakusema haya ninayoyaweka hapa chini

Ikumbukwe kwamba, kampeni bado zinaendelea huko viungani. Tumeshuhudia namna ThinkTanks wa CCM mitandaoni wakijionesha wazi wazi upande ambao chama chao kinamuunga mkono

Tundu Antipas Lisu
  1. Ukomo wa madaraka kwa Kiongozi wa chama
  2. Uwazi katika mapato na matumizi
  3. Upatikanaji wa wawakilishi wa chama mfano Viti maalumu na ngazi zingine zifuate utaratibu
  4. Uwepo ukomo wa kupata nafasi za viti maalumu yaan time limit
  5. Katiba ya chama kubadilishwa
  6. Kutokomeza Rushwa ndani ya chama

Freeman Aikaeli Mbowe
  1. Nimekitoa chama mbali sana na mi ndo nimebakia najua in and out
  2. Siwezi kuondoka nikaacha chama katika mvurugano wa namna hii,
  3. Bado Nina nguvu sana naweza fanya kazi na vikao nane kwa siku “Ebo give me a break” sijachoka
  4. Sijatimiza Umri aliostaafu nao mtei wa miaka 68, Mpaka nitimize
  5. Maridhiano yana umuhimu katika siasa ntaendelea kuyatumia inapobidi
  6. 6. Nimekaa gerezani sababu ya chama."
 
Back
Top Bottom