Mambo ya Muhimu ya kuzingatia katika Kutrade Financial instruments

Mambo ya Muhimu ya kuzingatia katika Kutrade Financial instruments

Nyumbalao

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
494
Reaction score
522
Wana jamvi nami nimeona niweke two cents zangu kuhusu swala lilochukua moto kwa siku za karibuni haswa swala hili la forex na options.
Mambo muhimu sana ya kuzingatia, nayaweka hapa chini nikiwa trader niliyotrade kwa miaka zaidi ya kumi na nimetrade trade 11,371 na katika hizo nimepata faida trade 8,880 (78.09%) na nimepata loss trade 2,491 (21.91%) kwahiyo haya ninayoyaweka hapa sio vitu vya vitabuni wala sio getting rich scheme ni mambo ambayo nimepractice kwa kipindi naona naweza kuyasemea kidogo sana.

1. Tafuta kujijua wewe ni trader/investor wa aina gani wewe ni mtu wa muda mrefu muda mfupi na jinsi ambavyo unaweza kufanya mambo yako. Mfano ukipata loss unajisikiaje unachukulia kama ni mwisho wa dunia au unaangalia kama nikuprune msitu wako ili uzae zaidi baadaye.

2. Tafuta sana elimu kwenye eneo hilo usiende tu kwa emotions na kusikia tumia dakika 15 mpaka 30 kila siku kuingia ndani kwenye hili jambo kama unataka kuingia kwenye stocks tafuta detail ya kampuni kwa undani kama unataka forex anza na chache jua Fundamental then uje kwenye Technical najua watu wengi wanakimbilia kwenye Technical na hasa hiyo price actions bila kuwa na hata clue ya Fundamental ni makosa kufanya hivyo. Maana fundamental inakupa kuangalia picha kubwa kama sasa mfano fundamental ya dollar ni strong ukilinganisha na currency nyingine. Ila kwenye dakika zako 5 na 15 inawezekana kukawa na fursa inayosema vinginevyo ila haitakupa faida sana kama ukienda na fursa inayokubaliana na fundamental.

3.Tafuta broker anayeeleweka na aliyesajiliwa na hasa kwenye nchi ambazo nazo tuna mahusiano mazuri na nchi yetu ni rahisi kufuatilia. Na hata mimi kuna preference zangu za broker katika safari yangu hii nimeshatumia brokers zaidi ya watano. Lakini tafuta anayekufaa fanya utafiti maana kila mmoja anaweza kuwa na faida na hasara zake angalia kama inafit malengo yako fanya kazi.

4.Tafuta mentor hakuna haja sana ya kutengeneza barabara kwenye njia wakati kuna watu wameshailima. Na unaweza kutafuta watu waliokwesha kufanya unachokitaka kufanya ukawafuata ila vilevile unaweza kutengeza group la watu unaoanza ukapeana kuspecialize kwenye instruments chache na kushare.

5. Fuata system yako ya kutrade kama inakupa faida zaidi ya asilimia 70% ukiwa na systems au utaratibu unaoweza kukupa faida kwa zaidi ya asilimia 70% kwa trade atleast 500. Ufuate huo na fuata huo kila wakati. Discipline ni jambo la msingi mno katika kutrade kuliko ninavyoweza kulielezea jua kwamba jitahidi kufungua duka lako yaani biashara yako muda huo huo kila siku. Jipangie muda wa kufanya hili jambo kila siku utaona mafanikio yake.

6. Epuka over trading watu wengi wanatrade wanatrade kwa mwingi sana kuliko wanavyoweza kuimili na hatimaye wanalazimisha trades ambazo baadaye zinawaumiza tafuta balance. Opportunity haziishi kama leo hazijaja kesho zitatokea jifunze kuwa na kiasi. Hili ni gumu ila ukilizoea unaenda nalo tuu bila shida ila ni gumu sio rahisi lazima ukubali.

7. Epuka kuchukua kiasi kikubwa cha trade kuliko uwezo wako. Jitahidi kuchukua position yenye kurange 1-2% ya akaunti yako na muda wowete usiruhusu hasara ya zaidi ya 5% ya akaunti yako kwahiyo stop loss ni muhimu sana itumie.

8.Kubali kuchukua kile ambacho soko linakupa. Hakuna mtu yeyote anaweza kushindana na soko kwahiyo soko likikupa hasara ichukue kwa shukrani ikikupa faida hivyo hivyo. Jua unavyoingia kwenye trade yeyote ile kuna matokeo mawili hasara au faida. Sasa ingia kwenye position yenye nafasi kubwa ya kukupa faida na sio vinginevyo ikikupa hasara nayo ichukue mapema na sio unasubiri mpaka inakuw kubwa sana. Hii ni ngumu ila ukijiufunza kufanya hivyo utabaki na account yako na itakuwa kubwa tu.

Mwisho trading sio kazi ya kila mtu na kwa ukweli sio wote watakaona mafanikio lakini ukikubali kujifunza na kupractise bila kukata tamaa utaona faida yake. Nawasii wote kuwa trading ziko huku duniani toka zamani na kama kaliba yako unaona haikufai kaa mbali maana wote hatuwezi kuwa trader ni lazima tugawane kazi na hiyo sio kwamba wewe sio kamili wewe umezawadiwa hivyo. Itumie talanta yako kuudumia jamii na we utalipwa. Kwa ufupi sana huwa tunalipwa kwa matatizo tunayoyatatua kwenye jamii zetu.
Nawatakia siku njema na yenye baraka tele.
 

Attachments

  • EURUSDDaily pictures.png
    EURUSDDaily pictures.png
    7.5 KB · Views: 100
Moja wa broker wazuri ambao unaweza kudeposit hela at your convenient nakuanza kazi mapema ni hawa hapa TemplerFX | Promo Karibu ujifunze na ueleweshe naungana na post hapo juu trading ina risk sio unakuja kuprint hela. Unatakiwa uwe educated na kuchukua calculated risk
 
Nilikuwa naangalia nyuma na katika kazi zangu hizi za ushauri naamini nilitoa ushauri kuntu sana kwenye maada husika kwa wakati huo wale wote walioufuatilia tafadhali sema jambo. Kwa wale waliopuza nao namba nipate maoni najua inawezekana kwenye kipindi ushauri huu unatoka ulikuwa uko so busy kujua nini kinaendelea ila ni zamu ya kuangalia tena wapi ulianguka na kuanza upya. Kwa wanataka kupractice link hii hapa unaweza kujifunza jambo moja mbili Templer FX Trader
 
kweli ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote na ushauri mzuri nao utabaki hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom