Mambo ya Muungano kwenye Rasimu ya Katiba

Mambo ya Muungano kwenye Rasimu ya Katiba

Mtaanza lini kujadili katiba ya tanganyika?
 
Nakubaliana na wewe kuwa tuisome rasimu ya katiba kwa makini na tuichambue maana ikishapita huwa ni kazi sana kuirekebisha katiba. Maoni yangu ni haya:
A) MUHIMILI WA MAHAKAMA UMEWEKWA CHINI YA RAIS:
Kuna mahakama 2, mahakama ya juu na mahakama ya rufani:
146.-(1) Bila ya kuathiri masharti yoyote yaliyotangulia katika
Sehemu hii, kutakuwa na Muundo wa Mahakama katika Jamhuri ya
Muungano utakaokuwa kama ifuatavyo:
(a) Mahakama ya Juu; na
(b) Mahakama ya Rufani.
147.-(1)Kutakuwa na Mahakama ya Juu ya Jamhuri ya
Muungano au kwa kifupi itaitwa “Mahakama ya Juu” ambayo itakuwa
na:
(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa Rais wa Mahakama ya Juu;
(b) Naibu Jaji Mkuu ambaye atakuwa Makamu wa Rais wa
Mahakama ya Juu; na
(c) Majaji wengine wa Mahakama ya Juu wasiopungua saba.

Uteuzi wa jaji mkuu uko hivi:
151.-(1) Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa
majina ya watu watatu yaliyopendekezwa na Tume ya Utumishi wa
Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni kwa
ajili ya kuthibitishwa na Bunge.
(2) Jaji Mkuu ndiye atakuwa Mkuu wa Mhimili wa Mahakama
katika Jamhuri ya Muungano.

Uteuzi wa naibu Jaji mkuu uko hivi:
152.-(1) Naibu Jaji Mkuu atateuliwa na Rais kutoka miongoni
mwa majina ya watu watatu yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi
wa Mahakama na kabla ya kuapishwa jina lake litawasilishwa Bungeni
kwa ajili ya kuthibitishwa na Bunge.

Uteuzi wa majaji wengine saba wa kuunda Mahakama ya juu uko hivi:
153.-(1) Majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa na Rais kutoka
miongoni mwa majina yatakayopendekezwa na Tume ya Utumishi wa
Mahakama na wataapishwa na Rais.
Uteuzi wa mwenyekiti wa mahakama ya rufani, na majaji wa mahakama hiyo unafuata mlolongo huohuo rejea vifungu vya 162 na 163

Hiyo Tume ya utumishi wa mahakama inaundwa ifuatavyo:

172.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo
itaundwa na wajumbe tisa watakaoteuliwa na Rais kama ifutavyo:

(a) Jaji Mkuu ambaye atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano;
(c) Jaji mmoja wa Mahakama ya Juu;
(d) Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani;
(e) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanzania Bara;
(f) Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar;
(g) Wakuu Wawili wa vitivo vya sheria kutoka vyuo vikuu, mmoja
kutoka Tanzania Bara na moja kutoka Zanzibar
watakaopendekezwa na Jaji Mkuu; na
(h) Mtendaji Mkuu wa Mahakama ambaye atakuwa Katibu wa
Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Wajumbe a,b.c.d, na h ni wateule wa Rais; yaani watano kati ya tisa, bado hata hao wa namba g watapendekezwa na jaji mkuu ambaye ni mteule wa Rais!

Na kitu kingine ni kuwa Rais anaweza kutengua masharti ya katiba yanayohusu uteuzi wa watu wa muhimili huu, hasa sharti la muda (uzoefu),
Kifingu cha 153 “……na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi.
basi Rais anaweza kutengua sharti la kuwa na sifa kwa muda usiopungua
miaka kumi, na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa
Mahakama, kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu.”
Hapa Rais anapewa uwezo wa kutengua masharti ya katiba. Kumbuka hii ni katiba ya wananchi wote lakini Rais napewa uwezo wa kutengua uamuzi wa wananchi!

Hii inaacha nafasi ya Rais kumteua mtu kuwa Jaji wa mahakama ya juu au ya rufani ambaye hana uzoefu kwa kushauriana na tume ya utumishi ambayo ameiteua yeye mwenyewe!
Kwa kuruhusu kipengele hiki, Rais anapewa uwezo wa kutengua masharti ya katiba. Kumbuka hii ni katiba ya wananchi wote lakini Rais anapewa uwezo wa kutengua uamuzi wa wananchi

NAPENDEKEZA HII TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA IWE HURU NA RAIS ASIPEWE NAFASI YA KUTENGUA MASHARTI YA KATIBA. Kama ni lazima kutengua masharti basi wa kumruhusu kufanya hivyo si tume aliyoichagua mwenyewe bali Bunge ambalo limechaguliwa na wananchi kwa madhumuni ya kurekebisha katiba kwani katiba ni ya wananchi.

B) KUJAZA NAFASI WAZI ZA WABUNGE

Katika utangulizi wa Katiba ambao unaonyesha misingi yya Katiba ambayo imekubaliwa na wananchi, kuna kipengele kinasema:
“NA KWA KUWA, tunaamini kuwa misingi hiyo inaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye mfumo wa demokrasia na utawala bora ambayo Serikali yake inasimamiwa na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowawakilisha wananchi na Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na
kuhakikisha kuwa haki za binadamu zinalindwa na kudumishwa na kwamba wajibu wa
kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu”;
Hii inaonnyesha kuwa wananchi wanaamini katika bunge lenye wabunge wa kuchaguliwa na wanaowakilisha wananchi (yaani wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vya siasa au dini nk)

Pia kifungu cha 105 kinasaema :
105.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo:
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya
uchaguzi;
(b) Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni
mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge
kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa
Washirika wa Muungano.

Yaani kifungu hiki kinasisitiza kuwepo kwa wabunge waliochaguliwa na wananchi kuwakilisha majimbo (na hao watano tu walemavu wa kuteuliwa)

Pia kifungu cha 119 kinasisitiza wabunge wa majimbo wawe wa kuchaguliwa na wananchi:
“119.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi
watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na vile vile
masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa Katiba hii,
inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge.


SASA Kifungu cha 106 kinaua kabisa msingi ambao wananchi wanauamini
“116 (4) Endapo Mbunge anayetokana na chama cha siasa atapoteza sifa

za kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyokuwa ya Bunge kumaliza muda
wake, Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri, kwa mujibu wa masharti
yatakayowekwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, itamteua
na kumtangaza kuwa mbunge mtumwingine kutoka kwenye orodha ya
majina ya wagombea iliyowasilishwa na chama hicho kwa mujibu wa Ibara
ndogo ya (5)

Kwa maana ya kifungu hiki wananchi watawekewa mtu ambaye hawakumchagua kuwa mbunge wao. Suala kuwa chama husika kilimuweka katika orodha ya wagombea wake haina maana kuwa orodha hiyo ya chama ilichaguliwa na wananchi wote. Orodha hiyo inaandaliwa na chama husika kwa utaratibu wanaoujua wao ambao hauko kwenye katiba.
Je hii si kuvunja msingi iliotajwa kwenye utangulizi na kuwekewa msisitizo katika kifungu cha 105 na 119?
NAPENDEKEZA UWEPO UCHAGUZI MDOGO KUJAZA NAFASI WAZI. Tusikwepe gharama kwani hakika hiyo ni gharama ya demokrasia.

Suala hili likiachwa kama lilivyo kutajitokeza matatizo mengi kwenye uchaguzi mkuu kuzidi ilivyokuwa huko nyuma. Yaani chama kitaamua kutumia nguvu nyingi na mbinu zisizohalali ili kihakikishe kinapata kiti cha ubunge kikijua kuwa hata kama itathibitika kuwa mbinu mbaya zilitumika, chama kama chama hakitakuwa na cha kupoteza kwani kitaendelea kushikilia kiti chake.
Ni afadhali basi katiba ingesema kuwa aliyekuwa mshindi wa pili ndiye apewe hiyo nafasi hiyo kwani ana kura za wananchi, na pia itazuia nguvu na mbinu haramu kutumika wakati wa uchaguzi.


C) KUTANGAZA MALI KWA WATUMISHI WA UMMA
Kitu hiki ni kizuri na tumekuwa nacho kwa muda mrefu lakini hakionekani kuwashtua wahusika. Ni vyema basi katiba sasa ikakiwekea mkazo zaidi.
Katika kifungu cha16 kiongozi amelazimishwa kutangaza mali zake
“16.-(1) Kiongozi wa Umma atalazimika kutangaza, ndani ya
siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi,
mali na thamani zake na madeni yake katika Tume ya Maadili na
Uwajibikaji.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (1), Kiongozi
wa Umma atalazimika kutangaza mali zake na madeni:
(a) yake binafsi;
(b) ya mwenza wake wa ndoa; na
(c) watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane,
mara moja kila mwaka, au kadri itakavyoamuliwa na sheria.

Hii sehemu ya mwisho ndiyo inapoteza uzito wa suala hili. Kama kipengele hiki kitabaki kilivyo ni wazi Katiba imejiwekea mwanya wa kutungwa sheria itakayopoteza uzito wa Katiba, Ikimubukwe pia kuwa wabunge ni miongoni wa watakaotakiwa kutangaza mali na ndio haohao ambao watatunga sheria ya kujiwekea muda; je haitatokea conflict of interest? Kumbuka sheria inaweza kubadilishwabadilishwa wakati wowote. (leo iwe kila mwaka, kesho iwe kila miaka mitano, kesho kutwa iwe miaka miwili nk)
NAPENDEKEZA KATIBA YENYEWE IWEKE MUDA ILI KILA MHUSIKA AUFUATE, KUTANGAZA KILA MWAKA NI VIZURI ZAIDI. Nina uhakika kama mtu ameongeza mali halali ndani ya mwaka mmoja hawezi kushindwa kuzitaja.

Katika suala hili la utangazaji mali naona kama Spika anadhalilishwa katika kifungu cha 128

128 (4) Spika atatakiwa kuwasilisha kwa Rais nakala mbili za taarifa
rasmi ya maelezo ya mali yake, kadri itakavyokuwa, mali ya mke au mume
wake.
Kwa nini spika asiwasilishe taarifa hiyo kwenye tume ya maadili kama ilivyo kwa viongozi wengine? Hii si ni kumfanya aonekane yuko chini ya Rais? Je Rais yeye anawasilisha taarifa hizo kwa spika? Je kama spika hatawasilisha taarifa hizo kwa Rais, ina maana Rais ataweza kumchukulia hatua? Au tunadhani ni rahisi kwa tume ya maadili kumuuliza Rais kama spika ameshawasilisha orodha ya mali zake kwake au la!
Huu ni udhalilishaji wa muhimili mmoja dhidi ya mwingine.
NAPENDEKEZA SPIKA AWASILISHE ORODHA YA MALI ZAKE KWENYE TUME YA MAADILI NA KWA UTARATIBU SAWA NA WA VIONGOZI WOTE WA UMMA.

D) KUPINGA UCHAGUZI WA RAIS
Hili ni suala zuri kwa maana ya kuondoa mashaka juu ya uchaguzi wa Rais, yaani Katiba inatoa nafasi ya kupingwa kwa matokeo kabla Rais hajaapishwa. Tuliona kule Kenya katika uchaguzi ulioleta vurugu jinsi Rais alivyoapishwa haraka haraka na kusababisha mauaji. Katika uchaguzi ulioofuata w a nchi hiyo hiyo tumeona namna matokea yalivyopingwa na baada ya uamuzi wa mahakama hakuna vurugu.
Suala hili zuri limeharibiwa na Katiba yenyewe katika kifungu cha 78(4):
“78. (4) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu
inaweza kutoa uamuzi bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo
zikatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya
kutoa uamuzi.”
Yaani mahakama ya juu inatoa maamuzi yawe ni ya kutengua uchaguzi au ya kuthibitisha uchaguzi na hailazimiki kuweka wazi sababu za kufanya hivyo hadi hapo itakapoona inafaa kuzitoa ndani ya siku 30! Tunatarajia nini kwa wananchi ambao watakuwa hawakurudhika na uamuzi huo wa mahakama ya juu? Kwa nini sababu ziwekwe kuwa siri? Yaani mtu anapinga matokeo, anawasilisha sababu zake na vielelezo lakini mwisho anaambiwa (kwa mfano) kuwa matokeo yanabaki yalivyo na hapewi sababu za kufanya hivyo!

Ukisoma utaratibu wa kumuapisha Rais, utagundua kuwa sababu za uamuzi wa mahakama zitatolewa baada ya Rais kuapishwa! Tunafanya hivyo ili iweje? Kwamba kwa kuwa Rais atakuwa ameshaapishwa basi atakuwa na rungu la kuwapiga walalamikaji!

HAKUNA SABABU ZA MSINGI ZA KUFICHA SABABU IWAPO MAHAKAMA NI HURU NA INA UHAKIKA IMETOA UAMUZI WA HAKI

E) MASUALA YA MUUNGANO
Hapa naomba ufafanuzi wa kifungu cha 62
“62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote
juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka
hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na
mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawakwa ajili ya ustawi ulio bora
kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
Labda kama nimeelewa vibaya, sioni kwa nini mshirika wa Muungano awe na mamlaka na haki zote kwa mambo yasiyo ya muungano? Mimi nadhani mambo yasiyo ya muungano ndiyo yanashughulikiwa na washirika wa muungano kila mmoja katika eneo lake. Kwa mfano maliasili siyo suala la muungano, je Mtanzania bara atakuwaje na mamlaka na haki zote juu ya mafuta yaliyo Zanzibar? Je Mzanzibari atakuwaje na mamlaka na haki zote juu ya ardhi ya Tanzania bara?
NAONA HILO NI KOSA LA KIUANDISHI (TYPING ERROR), NENO “yasiyo” lifutwe mara moja.

215. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya
Muunganovitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) maduhuli yatokanayo na taasisi za Muungano;
(c) mchango kutoka kwa Washirika wa Muungano; na
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano.
Huu mchango kutoka washirika wa muungano ungetajwa kwa uwiano na uwiano huo huo ndiyo utumike mahali popote panapohitaji uwiano kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Yaani isiwe mshirika mmoja anachangia asilimia 60 lakini penye uwiano anapata asilimia 75 nk.
 
Hili la serikali 3 litaacha muunano ukiwa hai? kama tuna serikari ya shirikishao la EAC kuna haja gani ya kuwa na serikari ya shirikisho ya Tanzania, je kuna madhara Zanzibar ikiachiwa iingie EAC kama Nchi inayojitegemea? Wanajanvi naomba mnijuvye.
 
Hili la serikali 3 litaacha muunano ukiwa hai? kama tuna serikari ya shirikishao la EAC kuna haja gani ya kuwa na serikari ya shirikisho ya Tanzania, je kuna madhara Zanzibar ikiachiwa iingie EAC kama Nchi inayojitegemea? Wanajanvi naomba mnijuvye.


Kila siku nasema na nakuunga mkono 150%!!

Kwa nini tanang'ang'ania Serikali 3 na Zanzibar wakati tuna uwanja mpana zaidi wa kujidai wa Afrika Mashariki??

Tanganyika tunaogopa nini??

Naona kama vile tumerogwa!
 
...uhai wa muungano upo kwenye serikali tatu pekee,nje ya hilo hakuna muungano. mpaka sasa wazanzibari wanaserikali yao, yapo mambo yasiyo ya muungano yataratibiwa na serikali gani bila tanganyika ? zanzibar ikijiunga eac kama nchi inamaana hakuna muungano tena maana itakuwa na identity kimataifa kama taifa huru. ukikubali muungano lazima kuna mambo utayaacha na ndio maana halisi ya muungano. kama kila nchi ikifanya mambo yake yenyewe hapo tena hakuna muungano....
 
Kila siku nasema na nakuunga mkono 150%!!

Kwa nini tanang'ang'ania Serikali 3 na Zanzibar wakati tuna uwanja mpana zaidi wa kujidai wa Afrika Mashariki??

Tanganyika tunaogopa nini??

Naona kama vile tumerogwa!


Serikali 3, tumeamua kuuvunja muunguno kiustaarabu ili tusiwatie aibu waasisi wa Muungano ya hayatui Mwl Juluis K. Nyerere na Hayati Karume
 
Sioni faida za muungano na kanchi kadogo ka Zanzibar yenye watu 1.3 milioni na ukubwa wa wilaya ya Kinondoni lakini wenye ushawishi mkubwa katika siasa za nchi yenye zaidi ya watu 43 milioni.Fikiria Zanzibar ina wabunge 60 katika bunge la JMT ambao wanalipwa na hazina ya Dar sawa sawa na mbunge wa Kigoma anayewakilisha zaidi ya watu 1 milioni.Hii ni nini kama si unyonyaji.
 
Exactly!
Wakati kabla ya uhuru Nyerere alikuwa tayari kusubiri Kenya na Uganda wawe huru kwanza ndo tuwe nchi moja!

Sasa tuna Jumuia ya EA.. na inavyoelekea Jumuia itakuja kuwa Muungano wa kisisasa!

Kwa nini Bara (44m) ijibane na Zanzibar (1m).. na kuwa serikali tatu!!! halafu tena ndo tujiunge wote na EA??

Why??

ushauri wangi Muungano uwe wa EA na siyo na Tanganyika na Zanzibar!

Hii itakuwa vyema kwa Visiwani na bara!

Visiwani wabebe mzigo wa kujiunga na EA na siyo kutumia mgongo wa bara!

Nikuulize??? Kwa nini kwa mfano Tz ijiunge na Uganda kwanza ndo ijiunge ndo tukishakuwa na uganda tujiunge na EA??
Kwa ni ni kila nchi isijiunge yenyewe?


...uhai wa muungano upo kwenye serikali tatu pekee,nje ya hilo hakuna muungano. mpaka sasa wazanzibari wanaserikali yao, yapo mambo yasiyo ya muungano yataratibiwa na serikali gani bila tanganyika ? zanzibar ikijiunga eac kama nchi inamaana hakuna muungano tena maana itakuwa na identity kimataifa kama taifa huru. ukikubali muungano lazima kuna mambo utayaacha na ndio maana halisi ya muungano. kama kila nchi ikifanya mambo yake yenyewe hapo tena hakuna muungano....
 
Sioni faida za muungano na kanchi kadogo ka Zanzibar yenye watu 1.3 milioni na ukubwa wa wilaya ya Kinondoni lakini wenye ushawishi mkubwa katika siasa za nchi yenye zaidi ya watu 43 milioni.Fikiria Zanzibar ina wabunge 60 katika bunge la JMT ambao wanalipwa na hazina ya Dar sawa sawa na mbunge wa Kigoma anayewakilisha zaidi ya watu 1 milioni.Hii ni nini kama si unyonyaji.

Usitafune maneno Ngongo bana. Huu ni upuuzi! Tuwaingize kwenye federation ya EAC kama mataifa jirani mengine. Haki atayopata Mrundi iwe ndo haki anapewa Zenji,full stop; and we role the effect back to 1964. Hawataki hilo, Tanzania iwe na serikali moja na haki anayopewa mtu wa nzenga ndo hiyohiyo anapewa mtu wa pemba. Huu upuuzi wa kusumbuana sumbuana vichwa ufike mwisho.
 
Rasimu ya katiba mpya ina jambo la maana moja tu, kufufua Dola Takatifu la Tanganyika lililozikwa kwa hila za watawala miaka mitatu tangu likombolewe (1961-1964), Tukishapata Tanganyika yetu hayo ya Rasimu ya Tanzania hayatuhusu as sie ni ya Viongozi, Zanzibar kama vipi tukutane nao kombe la Kagame au challenge Cup!. Mchakato wa kuunda katiba ya Tanganyika unapaswa kukamilika kabla ya kuendelea na mchakato wa Rasimy ya katiba mpya ya Tanzania!
 
Waacheni wazanzibar weusi waliofanya mapinduzi wajiusahau kwaani wale waliokuwa wanafaidi mahusiano na mkoloni arabuni/sultan wa oman ndiyo wanataka muungano uvunjike yaani akina JUSA, shke Farid na nk. kwa kuwa wazenj hawataki muungano kama vile bara tunapata kitu hebu tuwape nchi yao, MCHAWI MPE MWANA ALEEE. tumechoka na kelele za wazenj. chakula tunalima sisi bara, nyama wananunua bara, biashara zote wapemba wamekamata kuanzia kariakoo mpaka uswazi. Nyie wazanzibar wenye asili Afrika kuweni makini na wanzanzibar wenye asili ya uajemi. JUSA, MAARIMU SEIF NA WENGINE.
 
Rasimu ya katiba mpya ina jambo la maana moja tu, kufufua Dola Takatifu la Tanganyika lililozikwa kwa hila za watawala miaka mitatu tangu likombolewe (1961-1964), Tukishapata Tanganyika yetu hayo ya Rasimu ya Tanzania hayatuhusu as sie ni ya Viongozi, Zanzibar kama vipi tukutane nao kombe la Kagame au challenge Cup!. Mchakato wa kuunda katiba ya Tanganyika unapaswa kukamilika kabla ya kuendelea na mchakato wa Rasimy ya katiba mpya ya Tanzania!

We Songoro, hiyo katiba ya Tanganyika mbona ipo!? Inaitaji tu editing kidogo hapa na pale basi.... Where is the problem.
 
Heri ujirani mwema kuliko udugu wa uhasama
Tunahitaji Tanganyika yenye mamlaka kamili na sio Tanzania bara .
 
Utakuwa muungano wa kuheshimiana zaidi. Tena baada ya upande fulani kukwama, which I am certain, nina uhakika tunaweza tukaishia kuwa na serekali moja
 
Utakuwa muungano wa kuheshimiana zaidi. Tena baada ya upande fulani kukwama, which I am certain, nina uhakika tunaweza tukaishia kuwa na serekali moja
Sawa mkuu tena wanaotaka muungano UFE kumbe ni hawa wanaong'ang'ania serikali MBILI.
 
Hili la serikali 3 litaacha muunano ukiwa hai? kama tuna serikari ya shirikishao la EAC kuna haja gani ya kuwa na serikari ya shirikisho ya Tanzania, je kuna madhara Zanzibar ikiachiwa iingie EAC kama Nchi inayojitegemea? Wanajanvi naomba mnijuvye.
Zanzibar si kuwa inataka kujiunga na hako kajumuiya kenu ka EAC ambako hakina cha maana kwa wananchi wa nchi jumuia, Zanzibar usiifananishe na timu zenu za Simba na Yanga (nadhani umenielewa), inahitaji mambo yaeleweke yapi Tanganyika inasimamia binafsi na si kwa mgongo wa muungano.
 
Kwa kukutahdharisha ni kuwa Muungano ulishavunjwa siku nyingi na wazanzibari wenyewe na kile tume ilichofanya ni kuhalarisha tu. Zanzibar kuna makamu wa kwanza na wa pili kwa katiba ipi ya jamuhuri! rais wa jamuhuri akiwa zanzibar kwa sherehe za kiserikali ni Rais wa zanzibar ndie anakagua gwaride la maaskari! sasa wewe hujui tu kuwa hizi ni tayari nchi mbili!!
 
Back
Top Bottom