Mambo ya nyumbani(home affairs)

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
japo kila mtu yupo huru kuanzisha thread humu wakati wowote naomba tufanye kitu kimoja
hapa tutapost mambo mbalimbali madogo yanayotokea majumbani kwetu,mfano chakula,sabuni za kufulia,dawa nzuri ya mbu, una allergy gani.msosi mzuri etc

kwa kuanzia na story yangu ya kwanza
mimi nina issue moja yaani kwanza napenda sana kupika japo mimi sio mpishi bora nyumbani kwetu ,ila najitahidi. ila tatizo langu moja jikoni napenda kuonja nyamaa yaani kama napika nyama kilo ujue robo nitaila huko jikoni hilo jambo nadhani ndo limenifanya maisha yangu nisijue kitu wembamba nakumbuka kuna wakati nipo darasa la tano nilipimwa uzito nikawa na kilo 55. natamani kuacha tabia ya kuonja onja msosi ila siwezi .huwa nashangaa kuna mtu anaweza kupika eti mwanzo mwisho haonji hata chumvi .yaani mimi naweka chumvi hata mara kumi kidogo kidoogo maana sipendi chumvi nyingi kuharibia watu mood ya kula .sasa kila nikiweka chumvi naonja kiukweli kama ni wali kijiko nile kabisa nisikilizie .
hyo ni namba moja leteni story zenu na nyie tushauriane

mods naombeni mpeleke jukwaa husika nimeshindwa kujua niweke wapi samahanini
 
Kweli hujui kupika... Sasa fanya sabstute uwe unapika maharage... Nyama waachie wajuvi hapo nyumbani
 
Hapo kwenye kuonja onja hapo nilikua nikikaanga samaki kama ni wale wa vipande basi kiko changu cha kuonja,na nikipika naenda na kisosi na kijiko kabisa jikon ila sasa hivi napika bila kuonja mwanzo mwisho yan
 
pika mchunga au mgagani ili uonje vizuri sio nyama kila siku
 
Mi najua kupika ila sijui Vitu vingi napenda sana kujarib Vitu vipya,so Mara nying napika mwenyew, ningependa kua mpishi mzuri,coz naboreka[very very bored]sana nikikaa tu bila kazi naitaj kufanya shughuli at any time,I live alone due to circumstances,ila napenda mapish ya BBQ, kimche na samaki,..hasa Asian,..
 
Nilipokua mdogo nilikua natamani kuonja msosi jikoni hasa wali. Msichana wa kazi alitutesa kwenye kuonja mnabaki kulalamika ii dada si utupe tu na sie tu onje anatutimua na kutishia kusema kwa wazazi tumekaa karibu na moto. Baasi kwa hasira nikasema subiri nikikua nitakua naonja bakuli zima sikupi(utadhan atakuwepo,sijui yupo wapi kwa sasa) siku hizi nasahau kuonja nnachopika kasoro upishi wa kuku
Hasa maini na moyo vinaliwa jikoni eti naonja kama nyama zimeiva[emoji3] [emoji3]
 

Sawa,
 
ahahaaa sasa maini na moyo si yanaiva mapema .mimi huwa naonja paja zima
 
Hapo kwenye kuonja onja hapo nilikua nikikaanga samaki kama ni wale wa vipande basi kiko changu cha kuonja,na nikipika naenda na kisosi na kijiko kabisa jikon ila sasa hivi napika bila kuonja mwanzo mwisho yan
hongera mwenzetu
 
Darasa la tano 55kg
Sasa hivi kg ngap??

Kama ukipika chakula chenyewe unamaliza jikoni

Ni bora uwe unapika chai tu...
Nadhan hiyo haitapungua hata ml..1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…