Mambo ya pesa MBONGO Kwa kilingala
Leo nilisikiliza asubuhi kipindi cha Pachanga time TBC FM. Kulikuwa na uchambuzi wa Wimbo wa TP OK Jazz unaoitwa Mbongo uliotungwa na mwanamuziki mahiri Simaro. Mambo yaliyonivutia katika uchambuzi wa wimbo huo ni yafuatayo; Pesa mama yako ni nani? Mama yako alizaa watoto wawili, wa kwanza pesa wa pili ni mwanamke. Nani aligundua pesa? Ukienda kwa mganga kutafuta utajiri - pesa na yeye anakuomba pesa, halafu ukimwangalia mganga mwenyewe ni masikini atawezaje kukupatia pesa? Ukienda hospitali kutibiwa watakuomba pesa. Ukifa ili uzikwe inahitajika pesa. Pesa inapatikana kwa njia nyingi; kuna wanaopata pesa kwa kurithiukiwafuata utapotea kuna wanaopata pesa kwa uchawi ukiwafuata utamaliza kuroga ndugu zako ubaki peke yako. kuna wanaopata pesa kwa wizi ukiwafuata utafungwa. Pesa oh pesa. Mbongo oh mbongo. Hongera Mbazigwa na Shimanga Asosa kwa kazi nzuri kutukumbusha miziki ya Bakulutu