Tatizo lilianzia tulipoanza kuchukuliwa utumwani. Jamii zilisambaratika na tulipoteza viongozi, uwongozi, elimu na ujuzi.
Wakolini walipokuja kututawala pia tuliishia kufanya kazi za kitumwa. Kazi za ujuzi walizofundishwa weusi ni uwalimu, uuguzi, upadre nk. Tulipopata Uhuru hatukuwa na uwezo wa kujitawala. Wakati wanatupa Uhuru walijua tu tutakwama.
Tungeweka malengo ya kuwajengea vijana kujifunza utawala wakati mkoloni anatawala, lakini hili mkoloni asingelikubali kwani angeshindwa kututawala kwa ukoloni mamboleo.