Mambo yanayoisibu SAUT Mwanza

Mambo yanayoisibu SAUT Mwanza

A

Anonymous

Guest
To: President, Bishop Wolfgang Pisa, OFM

Tanzania Episcopal Conference (TEC)

Kurasini Centre

P.O Box 2133

Dar es Salaam.

7 January 2025

Mhashamu Baba Askofu Pisa,

YAH: MAMBO YANAYOISIBU SAUT MWANZA.​

Tumsifu Yesu Kristo.

Kwanza nikupe hongera kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa TEC.

Mimi ni mdau wa SAUT Mwanza ambae nimekaa na kufanya kazi SAUT tangu inaanza na pia nimesoma hapa. Kwa hiyo ninapoandika hii barua naandika kwa uchungu kwa sababu naona mbele ya hiki chuo kuna giza sana na hakuna anaeonekana kujali. Kama usipoangalia wewe kama Mkuu wa SAUT, chuo chako ambacho zamani kilikuwa kinasifika kitakufa. Hivyo basi nimeona kama mkatoliki mkereketwa niongee na wewe kidogo kimaandishi.

Ninashukuru sana kuwa siko kwenye nafasi yoyote hapa chuoni kwa hiyo ninaangalia na kusikiliza malalamiko nikiwa nimekaa pembeni sasa naona yanazidi. Watu wengi wanajiuliza hivi hawa maaskofu na mapadre hawaoni uozo huu ulioko hapa chuoni au kuna nini? Au ni njama mahususi za kuhakikisha kwamba uongozi wa sasa, ili watu wapate cha kuongea? Watu wengi sasa tunamkumbuka Kitima enzi zake mtu ulikuwa unajisikia kuitwa mfanyakazi wa SAUT. Sio sasa.

Sasa ni vilio tu na malalamiko. Kila mtu anaapply kazi hata kama ni ya chini yake ili mradi tu aondoke SAUT! Kwa kweli hamuwatendei haki wanafunzi wanaojiunga hapa pamoja na walimu wa hapa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu kuliko chuo chochote duniani! Yaani ni kama vile yatima wasio na watu wa kuwasemea. Wakati Mwenyekiti wa Council akizidi kunenepa walimu wa SAUT ambao wengi wao wana wanafunzi zaidi ya mia tano wanakonda na wana dhiki za kupitiliza. Hivi kosa la walimu hawa ni nini? Kuipenda SAUT?

Walimu wenye wanafunzi zaidi ya mia tatu waliahidiwa kulipwa hela kidogo ya motisha kwa kazi kubwa wanayofanya, lakini matokeo yake hawajalipwa hata senti tano. Hivi ukiangalia kwa undani unafikiri hawa walimu wanasahihisha inavyotakiwa kweli au wanaweka tu marks. Motisha iko wapi kwa kazi kubwa wanayoifanya? Badala ya walimu hawa kusifiwa kwa kazi wanazofanya, wanasifiwa wasichana ambao wako ofisi ya makamu mkuu wa chuo au ni rafiki wa karibu wa PA wa makamu mkuu wa chuo. Makamu Mkuu wa chuo anamsifia sana Personal Assistant (PA) wake kuwa anamshauri vizuri na anafanya kazi sana, kila akikaa ana kazi ya kumsifia huyo dada, mpaka watu wanajiuliza huyu mzee kapewa nini? Kwa kweli anaudhi. Tungetegemea awasifie wafanyakazi wote wanaofanya vizuri. Mbona hafanyi hivyo.

Juzi juzi, PA wa Mkuu wa Chuo alikwenda nje ya nchi na watu wengine wawili, watu wakajiuliza amekwenda kufanya nini? Hata hatujamwona kutoa report yoyote. Kichekesho kingine, kuna M-Ethiopia ambae ndio kila mtu anasema anaendesha chuo na anakiharibu, eti yeye alikataliwa visa kwenda kwenye hiyo safari, nadhani akatetewa na Makamu mkuu wa Chuo akapata viza, wakati wenzie wanarudi, yeye ndio akaenda hiyo safari, kufanya nini?

Mhashamu baba Askofu hao ndio wanaokula hela za chuo kirahisi, ila walimu ambao ndio wanafanya kazi kubwa wakiomba hela za safari wananyimwa! Kuna watu huwa wanaenda TCU kwa sababu wanakiwakilisha chuo kwenye workshop Fulani au training, wakati mwingine wanaomba pesa wananyimwa!! Wakati wameenda kwa ajili ya Chuo!

Unafikiri hao viongozi watakuwa wana motisha gani ya kukifanyia chuo kazi? Kuna wakati juzi juzi Rais alikua anasafiri kwenda nje na wanataaluma kutoka idara za Kiswahili za vyuo mbali mbali. Ilikuwa safari ya kwenda Cuba kukuza Kiswahili na kujenga mahusiano na kutafutia wahadhiri wetu tonge waende wakafundishe huko. SUongozi wa AUT walimnyima hela mkuu wa idara ya Kiswahili! Jamani, kuna bahati nyingine bora kuliko kusafiri na Rais wa nchi! Tunashindwa na vyuo vidogo wao walituma wawakilishi! Halafu watu wanaenda Poland, kutafuta nini??

Kuna huyu M-Ethiopia wenu mlimuweka hapo. Huyu bwana yuko hapa kuharibu chuo. Yaani amehakikisha kwamba anajipenyeza mpaka amewekwa kwenye nafasi ambayo imetungwa ili mradi tu awe juu. Hela zote za SAUT ziko chini yake.

Kama hakupendi atahakikisha anakunyanyasa na kukutungia uongo mpaka kama sio mvumilivu unahama chuo. Maprofesa wanahama kwa sababu yake (Bilame, Tibategeza, Mbasa, Beda, wote hao maprofessor wazuri tu, n.k!) na wangekuwa wengi tu kama wengine wasingekuwa wabishi kuondoka. Anakutungia uongo na ubaya wenyewe hata akikutungia uongo uulizwi unashtukia tu unapata adhabu mpaka unahama.

Yeye hana nia nzuri na chuo yuko hapa kukiua. Muulize mfanyakazi yoyote wa SAUT atakwambia. Akiona tu kuna mhadhiri mahiri basi yeye atampania huyo mpaka amvunje vunje. Muulize DVCAA, DVCAF. Amehakikisha anawashusha wamekuwa wadogooo. Vitu wa academics Makamu wako anamuuliza yeye badala ya DVCAA.

Mkikaa kwenye kikao (hata Seneti) mkitoa maamuzi yeye anakwenda nyuma nyuma anamfanya Makamu mkuu wa Chuo anabadilisha mnabaki mnashangaa tu. Nimeshasikia viongizi wakiuliza sasa tunakaa Vikao vya nini? Father Nkwera kidogo alikuwa anajitahidi kulinda hadhi ya vikao lakini siku hizi utakuta watu hata wasiostaili kuingia senate wanaingia ili wapate posho.

Kuna msichana wa kikenya ana cheo cha Director wa international sijui kitu gani. Ukiuliza ofisi yake iko wapi huioni? Safari zote za nje anakwenda yeye peke yake, halafu makamu wako anamsifia kuwa anafanya kazi nzuri, sijui ni ipi na vigezo vya wanaofanya kazi nzuri sijui ni vipi? Tafadhali Mhashamu Baba Askofu rudisha hadhi ya chuo hiki. Kuna wafanyakazi wengine hawajalipwa gratuity hata moja, ukitaka kujua wanaofaidi ni wapi itisha list ya waliolipwa na ambao hawajalipwa, utakuwa huko administration wamelipana wote hata huyo m-ethiopia na rafiki zake, wakati huo huo kuna wafanyakazi hawajalipwa hata mara moja, kwa kisingizio cha mikopo, sasa wataishije kama hawajalipwa graituity zao si lazima wakope, basi wanakomeshwa hapo. Ila wao huko juu wamelipana wote.

Sasa hichi ni chuo chA DINI kweli? Kuna walimu wanafundisha weekend, jumamosi na jumapili wakati watu wengine kama huyo m-ethiopia wako nyumbani, kulipwa nao nasikia imekuwa shida wanalalamika sidhani kama wameshalipwa, kazi wamefanya lakini M-ethiopia hataki kuwalipa anawapa sababu mbalimbali ili wakate tamaa. Wakati wa graduation picha zinazopigwa na kupostiwa ni za hao viongozi tu na wala sio wahadhiri ambao wanafanya kazi kubwa mpaka hao wanafunzi wanahitimu. Sasa hali kama ni hiyo walimu wataacha kuuza mitihani na notes? Wataacha kukimbia? Wataacha kukitukana chuo kila wanapopata fursa?

Kwenye vitivo/ndaki ndio usiseme. Viongozi hawana wanachofanya ni kukaa kwenye vikao na kula chakula na kupata posho, ila waulize wakueleze kuhusu ndaki zao, hawana habari. Kuna huyo mmoja ni msukuma na chapombe sana, ila bosi anajifanya kama hajui kuwa huyu mtu hafai. Anamlinda tu watu wamesema wamechoka. We siku njoo ghafla waite hao wakuu wa vitivo uone kama wanajua kuhusu vitivo vyao. Utashangaa sana yaani aibu hata kuwalinganisha na wakuu wa vitivo kutoka katika vyuo vingine.

Miundo mbinu mibovu iliyochoka sana nakushauri Mhashamu Baba Askofu siku ukija usiishie tu ofisini. Pita madarasani, ofisi za walimu, vyooni, hostels, utajionea maanake walimu wanalalamika hata projectors za kugombania na ni mbovu, hazina tija. Na wanafunzi waliopita hapo chuoni zamani wanakishangaa chuo jinsi kilivyo na mazingira mabovu kabisa.

Makamu wa Chuo nae anachangia katika kukiharibu chuo. Alimwamini sana huyo M-Ethiopia na akaacha kuwasikiliza wasaidizi wake wakuu. Kuna maamuzi ambayo yanapitishwa na Senate yeye anayabadilisha pindi tu akiambiwa na M-Ethiopia. Nasikia viongozi wengine wanalalamika sasa tunapotezewa muda kwenye mikutano miingi ya nini?

Aliamua kuhamisha kitengo cha admission kutoka kuwa chini ya mkuu wa taaluma wa chuo akakipeleka kwake. Sababu ni ipi? Hayo ndio matokeo ya kushauriwa na PA wake badala ya kushauriwa na watu wanaohusika. Pengine PA alimshauri kuwa “Mwamishe rafiki yangu umuweke chini yako ili aweze kuingia kwenye senate”. Hiyo ofisi nayo inatakiwa itazamwe upya ili iendane na hadhi yake. Nashauri ijulikane na iwe wazi nani anaingia kwenye Senate na nani haingii. Wajumbe kutoka vyuo shirikishi vya SAUT wanatushangaa sana. Na hili linaweza kumnalizwa kwa urahisi kwa kuangalia Rules ans regulations za Chuo.

Mtu anaitwa Director wa International Office wakati hata ofisi ya kufanyia kazi hana. Kila safari ya nje anaenda mwenyewe ila wenzie wakienda kanataka kujua. Kana kihelehele sana na bwana mkubwa anathubutu kukasimamisha mbele eti kanafanya kazi nzuri, ipi? Makama Mkuu wa Chuo kila ikitokea nafasi anamsimamisha PA wake eti anamshauri vizuri, vipi? Mbona chuo kinaoza? Where is the professionalisms? Kwa hiyo washauri wake anaowaamini ni PA wake na M-Ethiopia wengine wote wanaonekana hawafai? Projectors ni mbovu na hazitoshi kwa mahaitaji ya kufundisha. Ukiipata unakuta inaonyesha rangi ya njano. Chache sana hazizidi tano labda ndio nzima. Huyo M-Ethiopia anapelekewa maombi haya ya kununua bulb, projectors anakataa. Watu wanadai haki zao anakataa, wakati yeye safari zake zote akitaka anakwenda na anajilipa vizuri.

Mwenyekiti wa Baraza la chuo kwa kweli ameshachokwa sana. Hasaidii kitu. Yeye kila siku ni kufoka tu. M-ethiopia akishamjaza maneno basi anakuja amejitayarisha kwa vita. Kila hoja ya kukijenga chuo yeye anaipiga chini!! Mimi nawaonea huruma sana viongozi wengine wa chuo ambao wana mikutano kibao, utekelezaji zero. Huko Lavoure Centre mna mpango gani? Ukija chuoni usiku unakuta mlinzi yuko gizani, hakuna bulb kwenye jingo la taaluma. Hata bulbs zinawashinda? Karibu chuo kitapitwa na ofisi za mtaa!

Tafadhali fanya kitu kuhusu hichi chuo chetu kilichotulea. Kwa hali hii ilivyo,kitakufia na ukizingatia serikali inajenga vyuo vingine 14. Kazi ipo. Amkeni kutoka usingizini SAUT. Na muanze kuwajali wahadhiri wenu, wao hawana mahali pa kula bure na wanafamilia za kutunza.

Pole kwa hii barua ila nimekaa naangalia mambo yanavyokwenda roho inaniuma. SAUT ni chuo change kimenisomesha na kunipa kazi. Nataka kuona hadhi yake inarudi. Sikutaka kupeleka kopi ya hii barua sehemu nyingine husika ila nikaona kwanza nikuletee wewe najua utafanya marekebisho ili chuo kiendelee kukua. Wasaidie pia wanafunzi wa certificate na diploma. Hao ndio wamesahauliwa na walimu wengi wanaowafundisha hawana hata sifa za kuwa wahadhiri! Walipataje kazi hawa? Au ni kwa sababu wanafanya kazi SAUT? Angalia hii isikiponze chuo. Kuwe na mkakati mzuri wa kupata wahadhiri wazuri na wahadhiri wakiahidiwa kufanya kazi na kulipwa basi hizo ahadi zitekelezwe sio kuwafanya wajinga mnawafunja morali.

Wako katika ujenzi wa Jiji la Mungu

Mdau mkereketwa.

CC: Secretary General of TEC: Fr, Charles Kitima, Minister of Education, Chairman TCU.
 
Aliyeandika Iyo Barua ni PETER KAFUMU, DVCAA Na CREUTUS,
pale Chuo kuna vita ya madaraka, kuna genge la watu Wanataka madaraka Kwa hali na mali, wameamua kuwachafua wenzao ili wao wachukue madraka yao, kabla ya huu utawala wa sasa kuingia madarakani chuo kilikua kinaenda kufa kabisa kilikua hakilipi mishahara ata kwa miezi mitatu walimu wanadai tu, walimu hawakua promoted kwa 10 wote walikua assistance lecturers tu, majengo yalikua yale yale ya mwaka 47, ila toka uongozi huu uingie walimu wanalipwa kwa wakati, idadi ya wanafunzi kusajiliwa imeongezeka, kuna majengo yameongezeka, chuo kimejengewa uzio ambao maduka ambayo yanatumika kama kitega uchumi cha chuo, na mengineyo mazuri, shida iliyopo pale chuo kwamba nafasi zote kubwa wanataka zishikwe na mapadri tu, iligenge la watu watatu ndio lina injinia Ili jambo.
 
To.President ,Bishop Wolfgang Pisa
Tanzania Episcopal Conference(TEC)
Kurasini Center
P.O.BOX 2133
Dar Es Salaam.
12/1/2025
YAH:TUNAOMBA UINGILIE KATI SAUT MWANZA.
Kwako Mkuu wa chuo ,pole na majukumu,nimeangalia andikokwenye jukwaa la jamii forums kuhusu chuo cha Saut,nimeamua kufatilia Sakata hilo kwa ukaribu kama mpenzi wachuo maana nimesoma hapo miaka kadhaa iliyopita kwanza nikabaini kuna mgogoro wa kiuongozi kuna kundi linahitajiumakamu mkuu wa chuo na cheo cha financial controller ambacho kuna mtu ametajwa kama mtu wa Ethiopia ,
Nimesikitishwa na watu wazima hawa wasiyokuwa na adabuhata kidogo kufikia hatua yakumuita askofu ambaye nimwenyekiti wa counsel ya chuo kuwa anajinenepea hidhi nidharau na utovu mkubwa sana wa kimaadili kwa kundi hililinalosaka Madaraka kwa nguvu na mapadre kuwemonimefedheheka sana .
Mh Raisi wa TEC Chuo hichi cha saut kabla ya uongozi huu waBalozi mwaka 2018 kilikuwa kikiongozwa na padri nadhaniwewe unajua chuo watumishi hata mshahara tu ulishindikanampaka miezi mitatu hujalipwa walimu walikata tamaa kabisa ilatangu uongozi huu uingie madeni yote yalilipwa na mishaharainalipwa kwa wakati ya kila mwezi.
Walimu hawakuwahi kuwa promoted kwa miaka kumi lakini katika uongozi huu imefanyika kila linalowezekana limefanyikakisheria wakuwa promoted.
Madarasa yamejengwa na mengine yamekuwa mentained bilashida yoyote, na ikumbukwe battle iliyokuwepo kati ya chuo naserikali mpaka ikafikia hatua wanafunzi TCU Ikawa inaletawachache ambao hata wakilipa ada haiwezi kuendesha chuoimefanyika juhudi kubwa sana ya balozi na serikali mpaka haliimerejea vizuri sana uhaba wa wanafunzi imekuwa historia namahusiano na serikali yamekuwa Chanya,
Mpaka naandika barua hiii kwako nimefatilia deni la chuonaomba kukueleza wakati uongozi wa balozi unaingia deniambalo chuo kilikuwa kinadaiwa ni bilioni 49 kwa muda huoanaeitwa mtu wa Ethiopia na makamu mkuu wamelifikisha denihilo bilioni 21 hii siyo hatua yakubeza kamwe najua wanaumiawamebanwa na huyo muethiopia hawapumui pesa inatoka kwautaratibu ili malengo na uendesheji wa chuo utimie kwaukamilifu bila mikopo.

Tujiulize kwa Pamoja imetajwa safari ya Poland hapa kuwawameenda wasiyo husika je wanajua ilikuwa inahusu nini , safari hiyo Mh Raisi wa baraza la maskofu ilidhaminiwa naErasmus fund kwa ajili ya chuo kikuu cha usafirishaji cha Poland kinaitwa international university of transport and logistics kilichopo wclavas City nchini Poland na safari hiyoimezaa matunda wanafunzi 12 na walimu 3 watafanya exchange program wataenda Poland kwa gharama za hicho chuo nawatatengeneza maabara ya transport and logistics hapo saut kwaajili ya nchi za Africa mashariki.
Mh Raisi kumekuwa na ujinga mwingi sana wa haka kakundikanakoongozwa na padre wako cretus na Dvcaa anayeitwaHosea Rwegoshora badala kutoa maoni yao kwenye proper forums wameanzisha vigenge visivyo na tija na chuo na sisiproducts za chuo hicho hatuwezi kuacha kukiokoa chuo ujingaunapofanywa na watu ambao hata uwezo wa leadership hawanamaana hata huyo dvcaa historia yake inajulikana tangu akiwaopen University mpaka anakuja Saut anadanganywa anadhanianaweza kuwa Makamu Mkuu wa Chuo.
Mh raisi juzi tu umeandikiwa na kikundi hicho hicho barua yatarehe 6 january 2025 yakukutaka umteue padre kutoka singidaanayeitwa masoy muhuri wa chuo umefojiwa na sahihiimesainiwa kwa niaba ya makamu mkuu wa chuo maanawalishindwa kuiga sahihi yake lengo lao nikutaka wapateanaeweza kupata njia yakujua operation za pesa zikoje maanawanahisi aliyepo ambaye ni padre pia hawapi taarifa pia stahikiza fedha ili waweze kuchochea chuki dhidi ya huyo muethiopiana makam mkuu wa chuo.
Mh raisi haka kakundi lazima kashughulikiwe ili chuo kiwesalama kamekuwa na mgogoro usio isha ukikutana na dvcaakazi yake ni kulalamika all the way kuonyesha kuwa boss wake hamna hanachofanya apewe yeye sasa umakam makuu wa chuoaongoze chuo tuone maana anajitanabaisha kuwa anaweza nakundi limemuahidi hivyo.
Wako katika ujenzi wa jiji la Mungu
Na mdau wa elimu Nchini Tanzania.

Cc:Secretary General of TEC,
 
Kama umeweza kuwajua waliandika barua gizani Tena kwa majina na vyeo vyao,bila shaka na wewe ni sehemu ya watuhumiwa au sehemu ya mchongo huo.
Kwa Sasa semeni matatizo tajwa hapo juu yapo au hayapo?

Watu wanapoweka mambo hayo mtandaoni ni ishara ya wazi kua mambo hayo yameshindwa kutatulika kwenye vikao au watu hawana sehemu ya kufungukia.

Nakueleza matatizo sio vita ya madaraka,au wivu bali nikutaka kua na taasi imara inayosimamia mission na vision yake.

Tumueache owner yaani Baraza la maaskofu lifanye utafiti wake, na watenge mda wa kutosha kukaa na makundi yote yaani staff na sio watawala.

"Kuruka ruka kwa maharage Ndo kuiva kwakwe " alisika mlevi mmoja akisema"
Wajibikeni
 
To: President, Bishop Wolfgang Pisa, OFM

Tanzania Episcopal Conference (TEC)

Kurasini Centre

P.O Box 2133

Dar es Salaam.

7 January 2025

Mhashamu Baba Askofu Pisa,

YAH: MAMBO YANAYOISIBU SAUT MWANZA.​

Tumsifu Yesu Kristo.

Kwanza nikupe hongera kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa TEC.

Mimi ni mdau wa SAUT Mwanza ambae nimekaa na kufanya kazi SAUT tangu inaanza na pia nimesoma hapa. Kwa hiyo ninapoandika hii barua naandika kwa uchungu kwa sababu naona mbele ya hiki chuo kuna giza sana na hakuna anaeonekana kujali. Kama usipoangalia wewe kama Mkuu wa SAUT, chuo chako ambacho zamani kilikuwa kinasifika kitakufa. Hivyo basi nimeona kama mkatoliki mkereketwa niongee na wewe kidogo kimaandishi.

Ninashukuru sana kuwa siko kwenye nafasi yoyote hapa chuoni kwa hiyo ninaangalia na kusikiliza malalamiko nikiwa nimekaa pembeni sasa naona yanazidi. Watu wengi wanajiuliza hivi hawa maaskofu na mapadre hawaoni uozo huu ulioko hapa chuoni au kuna nini? Au ni njama mahususi za kuhakikisha kwamba uongozi wa sasa, ili watu wapate cha kuongea? Watu wengi sasa tunamkumbuka Kitima enzi zake mtu ulikuwa unajisikia kuitwa mfanyakazi wa SAUT. Sio sasa. Sasa ni vilio tu na malalamiko. Kila mtu anaapply kazi hata kama ni ya chini yake ili mradi tu aondoke SAUT! Kwa kweli hamuwatendei haki wanafunzi wanaojiunga hapa pamoja na walimu wa hapa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu kuliko chuo chochote duniani! Yaani ni kama vile yatima wasio na watu wa kuwasemea. Wakati Mwenyekiti wa Council akizidi kunenepa walimu wa SAUT ambao wengi wao wana wanafunzi zaidi ya mia tano wanakonda na wana dhiki za kupitiliza. Hivi kosa la walimu hawa ni nini? Kuipenda SAUT? Walimu wenye wanafunzi zaidi ya mia tatu waliahidiwa kulipwa hela kidogo ya motisha kwa kazi kubwa wanayofanya, lakini matokeo yake hawajalipwa hata senti tano. Hivi ukiangalia kwa undani unafikiri hawa walimu wanasahihisha inavyotakiwa kweli au wanaweka tu marks. Motisha iko wapi kwa kazi kubwa wanayoifanya? Badala ya walimu hawa kusifiwa kwa kazi wanazofanya, wanasifiwa wasichana ambao wako ofisi ya makamu mkuu wa chuo au ni rafiki wa karibu wa PA wa makamu mkuu wa chuo. Makamu Mkuu wa chuo anamsifia sana Personal Assistant (PA) wake kuwa anamshauri vizuri na anafanya kazi sana, kila akikaa ana kazi ya kumsifia huyo dada, mpaka watu wanajiuliza huyu mzee kapewa nini? Kwa kweli anaudhi. Tungetegemea awasifie wafanyakazi wote wanaofanya vizuri. Mbona hafanyi hivyo.

Juzi juzi, PA wa Mkuu wa Chuo alikwenda nje ya nchi na watu wengine wawili, watu wakajiuliza amekwenda kufanya nini? Hata hatujamwona kutoa report yoyote. Kichekesho kingine, kuna M-Ethiopia ambae ndio kila mtu anasema anaendesha chuo na anakiharibu, eti yeye alikataliwa visa kwenda kwenye hiyo safari, nadhani akatetewa na Makamu mkuu wa Chuo akapata viza, wakati wenzie wanarudi, yeye ndio akaenda hiyo safari, kufanya nini? Mhashamu baba Askofu hao ndio wanaokula hela za chuo kirahisi, ila walimu ambao ndio wanafanya kazi kubwa wakiomba hela za safari wananyimwa! Kuna watu huwa wanaenda TCU kwa sababu wanakiwakilisha chuo kwenye workshop Fulani au training, wakati mwingine wanaomba pesa wananyimwa!! Wakati wameenda kwa ajili ya Chuo! Unafikiri hao viongozi watakuwa wana motisha gani ya kukifanyia chuo kazi? Kuna wakati juzi juzi Rais alikua anasafiri kwenda nje na wanataaluma kutoka idara za Kiswahili za vyuo mbali mbali. Ilikuwa safari ya kwenda Cuba kukuza Kiswahili na kujenga mahusiano na kutafutia wahadhiri wetu tonge waende wakafundishe huko. SUongozi wa AUT walimnyima hela mkuu wa idara ya Kiswahili! Jamani, kuna bahati nyingine bora kuliko kusafiri na Rais wa nchi! Tunashindwa na vyuo vidogo wao walituma wawakilishi! Halafu watu wanaenda Poland, kutafuta nini??

Kuna huyu M-Ethiopia wenu mlimuweka hapo. Huyu bwana yuko hapa kuharibu chuo. Yaani amehakikisha kwamba anajipenyeza mpaka amewekwa kwenye nafasi ambayo imetungwa ili mradi tu awe juu. Hela zote za SAUT ziko chini yake. Kama hakupendi atahakikisha anakunyanyasa na kukutungia uongo mpaka kama sio mvumilivu unahama chuo. Maprofesa wanahama kwa sababu yake (Bilame, Tibategeza, Mbasa, Beda, wote hao maprofessor wazuri tu, n.k!) na wangekuwa wengi tu kama wengine wasingekuwa wabishi kuondoka. Anakutungia uongo na ubaya wenyewe hata akikutungia uongo uulizwi unashtukia tu unapata adhabu mpaka unahama. Yeye hana nia nzuri na chuo yuko hapa kukiua. Muulize mfanyakazi yoyote wa SAUT atakwambia. Akiona tu kuna mhadhiri mahiri basi yeye atampania huyo mpaka amvunje vunje. Muulize DVCAA, DVCAF. Amehakikisha anawashusha wamekuwa wadogooo. Vitu wa academics Makamu wako anamuuliza yeye badala ya DVCAA. Mkikaa kwenye kikao (hata Seneti) mkitoa maamuzi yeye anakwenda nyuma nyuma anamfanya Makamu mkuu wa Chuo anabadilisha mnabaki mnashangaa tu. Nimeshasikia viongizi wakiuliza sasa tunakaa Vikao vya nini? Father Nkwera kidogo alikuwa anajitahidi kulinda hadhi ya vikao lakini siku hizi utakuta watu hata wasiostaili kuingia senate wanaingia ili wapate posho. Kuna msichana wa kikenya ana cheo cha Director wa international sijui kitu gani. Ukiuliza ofisi yake iko wapi huioni? Safari zote za nje anakwenda yeye peke yake, halafu makamu wako anamsifia kuwa anafanya kazi nzuri, sijui ni ipi na vigezo vya wanaofanya kazi nzuri sijui ni vipi? Tafadhali Mhashamu Baba Askofu rudisha hadhi ya chuo hiki. Kuna wafanyakazi wengine hawajalipwa gratuity hata moja, ukitaka kujua wanaofaidi ni wapi itisha list ya waliolipwa na ambao hawajalipwa, utakuwa huko administration wamelipana wote hata huyo m-ethiopia na rafiki zake, wakati huo huo kuna wafanyakazi hawajalipwa hata mara moja, kwa kisingizio cha mikopo, sasa wataishije kama hawajalipwa graituity zao si lazima wakope, basi wanakomeshwa hapo. Ila wao huko juu wamelipana wote. Sasa hichi ni chuo chA DINI kweli? Kuna walimu wanafundisha weekend, jumamosi na jumapili wakati watu wengine kama huyo m-ethiopia wako nyumbani, kulipwa nao nasikia imekuwa shida wanalalamika sidhani kama wameshalipwa, kazi wamefanya lakini M-ethiopia hataki kuwalipa anawapa sababu mbalimbali ili wakate tamaa. Wakati wa graduation picha zinazopigwa na kupostiwa ni za hao viongozi tu na wala sio wahadhiri ambao wanafanya kazi kubwa mpaka hao wanafunzi wanahitimu. Sasa hali kama ni hiyo walimu wataacha kuuza mitihani na notes? Wataacha kukimbia? Wataacha kukitukana chuo kila wanapopata fursa?

Kwenye vitivo/ndaki ndio usiseme. Viongozi hawana wanachofanya ni kukaa kwenye vikao na kula chakula na kupata posho, ila waulize wakueleze kuhusu ndaki zao, hawana habari. Kuna huyo mmoja ni msukuma na chapombe sana, ila bosi anajifanya kama hajui kuwa huyu mtu hafai. Anamlinda tu watu wamesema wamechoka. We siku njoo ghafla waite hao wakuu wa vitivo uone kama wanajua kuhusu vitivo vyao. Utashangaa sana yaani aibu hata kuwalinganisha na wakuu wa vitivo kutoka katika vyuo vingine.

Miundo mbinu mibovu iliyochoka sana nakushauri Mhashamu Baba Askofu siku ukija usiishie tu ofisini. Pita madarasani, ofisi za walimu, vyooni, hostels, utajionea maanake walimu wanalalamika hata projectors za kugombania na ni mbovu, hazina tija. Na wanafunzi waliopita hapo chuoni zamani wanakishangaa chuo jinsi kilivyo na mazingira mabovu kabisa.

Makamu wa Chuo nae anachangia katika kukiharibu chuo. Alimwamini sana huyo M-Ethiopia na akaacha kuwasikiliza wasaidizi wake wakuu. Kuna maamuzi ambayo yanapitishwa na Senate yeye anayabadilisha pindi tu akiambiwa na M-Ethiopia. Nasikia viongozi wengine wanalalamika sasa tunapotezewa muda kwenye mikutano miingi ya nini? Aliamua kuhamisha kitengo cha admission kutoka kuwa chini ya mkuu wa taaluma wa chuo akakipeleka kwake. Sababu ni ipi? Hayo ndio matokeo ya kushauriwa na PA wake badala ya kushauriwa na watu wanaohusika. Pengine PA alimshauri kuwa “Mwamishe rafiki yangu umuweke chini yako ili aweze kuingia kwenye senate”. Hiyo ofisi nayo inatakiwa itazamwe upya ili iendane na hadhi yake. Nashauri ijulikane na iwe wazi nani anaingia kwenye Senate na nani haingii. Wajumbe kutoka vyuo shirikishi vya SAUT wanatushangaa sana. Na hili linaweza kumnalizwa kwa urahisi kwa kuangalia Rules ans regulations za Chuo.

Mtu anaitwa Director wa International Office wakati hata ofisi ya kufanyia kazi hana. Kila safari ya nje anaenda mwenyewe ila wenzie wakienda kanataka kujua. Kana kihelehele sana na bwana mkubwa anathubutu kukasimamisha mbele eti kanafanya kazi nzuri, ipi? Makama Mkuu wa Chuo kila ikitokea nafasi anamsimamisha PA wake eti anamshauri vizuri, vipi? Mbona chuo kinaoza? Where is the professionalisms? Kwa hiyo washauri wake anaowaamini ni PA wake na M-Ethiopia wengine wote wanaonekana hawafai? Projectors ni mbovu na hazitoshi kwa mahaitaji ya kufundisha. Ukiipata unakuta inaonyesha rangi ya njano. Chache sana hazizidi tano labda ndio nzima. Huyo M-Ethiopia anapelekewa maombi haya ya kununua bulb, projectors anakataa. Watu wanadai haki zao anakataa, wakati yeye safari zake zote akitaka anakwenda na anajilipa vizuri.

Mwenyekiti wa Baraza la chuo kwa kweli ameshachokwa sana. Hasaidii kitu. Yeye kila siku ni kufoka tu. M-ethiopia akishamjaza maneno basi anakuja amejitayarisha kwa vita. Kila hoja ya kukijenga chuo yeye anaipiga chini!! Mimi nawaonea huruma sana viongozi wengine wa chuo ambao wana mikutano kibao, utekelezaji zero. Huko Lavoure Centre mna mpango gani? Ukija chuoni usiku unakuta mlinzi yuko gizani, hakuna bulb kwenye jingo la taaluma. Hata bulbs zinawashinda? Karibu chuo kitapitwa na ofisi za mtaa!

Tafadhali fanya kitu kuhusu hichi chuo chetu kilichotulea. Kwa hali hii ilivyo,kitakufia na ukizingatia serikali inajenga vyuo vingine 14. Kazi ipo. Amkeni kutoka usingizini SAUT. Na muanze kuwajali wahadhiri wenu, wao hawana mahali pa kula bure na wanafamilia za kutunza.

Pole kwa hii barua ila nimekaa naangalia mambo yanavyokwenda roho inaniuma. SAUT ni chuo change kimenisomesha na kunipa kazi. Nataka kuona hadhi yake inarudi. Sikutaka kupeleka kopi ya hii barua sehemu nyingine husika ila nikaona kwanza nikuletee wewe najua utafanya marekebisho ili chuo kiendelee kukua. Wasaidie pia wanafunzi wa certificate na diploma. Hao ndio wamesahauliwa na walimu wengi wanaowafundisha hawana hata sifa za kuwa wahadhiri! Walipataje kazi hawa? Au ni kwa sababu wanafanya kazi SAUT? Angalia hii isikiponze chuo. Kuwe na mkakati mzuri wa kupata wahadhiri wazuri na wahadhiri wakiahidiwa kufanya kazi na kulipwa basi hizo ahadi zitekelezwe sio kuwafanya wajinga mnawafunja morali.

Wako katika ujenzi wa Jiji la Mungu

Mdau mkereketwa.

CC: Secretary General of TEC: Fr, Charles Kitima, Minister of Education, Chairman TCU.
Kuna mambo mengi hapo yameainishwa. Ni kweli kuna progress imepigwa kwa miaka ya hivi karibuni lakini hiyo haiondoi ukweli wa matatizo haliyoainishwa hapo na mengine mengi ambayo hayajawekwa. Ni wakati mwafaka wa taasisi hiyo kufanya tafakuri ya kina kama inaelekea kwenye malengo yake au inarudi nyuma. Suala la kutupiana lawana linaweza lisilete suluhu ya kudumu, lakini naamini kwenye majadiliano, mashirikiano, uwajibikaji kwa uwazi na kurekebishana kwa ukweli na uaminifu penye mapungufu.

Kuna watu na familia zao wanategemea SAUT ili kujipatia kipato. Ukiangalia ile Nyamalango, kwa Masha, Ngaza, Kijiweni na maeneo yote ya karibu na chuo yanategemea chuo hicho ili kujiendeshea maisha. Bila shaka hata uchumi wa jiji la Mwanza kwa kiasi unaihitaji saut kwa namna moja au nyingine. Hivyo, yeyote anayewaza kuiangamiza saut kwa kutosimama na ukweli wa mambo ulivyo anahatarisha uchumi na ustawi wa maisha ya jamii kubwa.

Ni wakati mwafaka taaluma na utaalamu wa watu walioaminiwa na kuwa sehemu ya wafanya maamuzi kuchukua hatua zenye kurejesha matumaini kwa jumuiya nzima ya chuo.
 
To: President, Bishop Wolfgang Pisa, OFM

Tanzania Episcopal Conference (TEC)

Kurasini Centre

P.O Box 2133

Dar es Salaam.

7 January 2025

Mhashamu Baba Askofu Pisa,

YAH: MAMBO YANAYOISIBU SAUT MWANZA.​

Tumsifu Yesu Kristo.

Kwanza nikupe hongera kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa TEC.

Mimi ni mdau wa SAUT Mwanza ambae nimekaa na kufanya kazi SAUT tangu inaanza na pia nimesoma hapa. Kwa hiyo ninapoandika hii barua naandika kwa uchungu kwa sababu naona mbele ya hiki chuo kuna giza sana na hakuna anaeonekana kujali. Kama usipoangalia wewe kama Mkuu wa SAUT, chuo chako ambacho zamani kilikuwa kinasifika kitakufa. Hivyo basi nimeona kama mkatoliki mkereketwa niongee na wewe kidogo kimaandishi.

Ninashukuru sana kuwa siko kwenye nafasi yoyote hapa chuoni kwa hiyo ninaangalia na kusikiliza malalamiko nikiwa nimekaa pembeni sasa naona yanazidi. Watu wengi wanajiuliza hivi hawa maaskofu na mapadre hawaoni uozo huu ulioko hapa chuoni au kuna nini? Au ni njama mahususi za kuhakikisha kwamba uongozi wa sasa, ili watu wapate cha kuongea? Watu wengi sasa tunamkumbuka Kitima enzi zake mtu ulikuwa unajisikia kuitwa mfanyakazi wa SAUT. Sio sasa. Sasa ni vilio tu na malalamiko. Kila mtu anaapply kazi hata kama ni ya chini yake ili mradi tu aondoke SAUT! Kwa kweli hamuwatendei haki wanafunzi wanaojiunga hapa pamoja na walimu wa hapa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu kuliko chuo chochote duniani! Yaani ni kama vile yatima wasio na watu wa kuwasemea. Wakati Mwenyekiti wa Council akizidi kunenepa walimu wa SAUT ambao wengi wao wana wanafunzi zaidi ya mia tano wanakonda na wana dhiki za kupitiliza. Hivi kosa la walimu hawa ni nini? Kuipenda SAUT? Walimu wenye wanafunzi zaidi ya mia tatu waliahidiwa kulipwa hela kidogo ya motisha kwa kazi kubwa wanayofanya, lakini matokeo yake hawajalipwa hata senti tano. Hivi ukiangalia kwa undani unafikiri hawa walimu wanasahihisha inavyotakiwa kweli au wanaweka tu marks. Motisha iko wapi kwa kazi kubwa wanayoifanya? Badala ya walimu hawa kusifiwa kwa kazi wanazofanya, wanasifiwa wasichana ambao wako ofisi ya makamu mkuu wa chuo au ni rafiki wa karibu wa PA wa makamu mkuu wa chuo. Makamu Mkuu wa chuo anamsifia sana Personal Assistant (PA) wake kuwa anamshauri vizuri na anafanya kazi sana, kila akikaa ana kazi ya kumsifia huyo dada, mpaka watu wanajiuliza huyu mzee kapewa nini? Kwa kweli anaudhi. Tungetegemea awasifie wafanyakazi wote wanaofanya vizuri. Mbona hafanyi hivyo.

Juzi juzi, PA wa Mkuu wa Chuo alikwenda nje ya nchi na watu wengine wawili, watu wakajiuliza amekwenda kufanya nini? Hata hatujamwona kutoa report yoyote. Kichekesho kingine, kuna M-Ethiopia ambae ndio kila mtu anasema anaendesha chuo na anakiharibu, eti yeye alikataliwa visa kwenda kwenye hiyo safari, nadhani akatetewa na Makamu mkuu wa Chuo akapata viza, wakati wenzie wanarudi, yeye ndio akaenda hiyo safari, kufanya nini? Mhashamu baba Askofu hao ndio wanaokula hela za chuo kirahisi, ila walimu ambao ndio wanafanya kazi kubwa wakiomba hela za safari wananyimwa! Kuna watu huwa wanaenda TCU kwa sababu wanakiwakilisha chuo kwenye workshop Fulani au training, wakati mwingine wanaomba pesa wananyimwa!! Wakati wameenda kwa ajili ya Chuo! Unafikiri hao viongozi watakuwa wana motisha gani ya kukifanyia chuo kazi? Kuna wakati juzi juzi Rais alikua anasafiri kwenda nje na wanataaluma kutoka idara za Kiswahili za vyuo mbali mbali. Ilikuwa safari ya kwenda Cuba kukuza Kiswahili na kujenga mahusiano na kutafutia wahadhiri wetu tonge waende wakafundishe huko. SUongozi wa AUT walimnyima hela mkuu wa idara ya Kiswahili! Jamani, kuna bahati nyingine bora kuliko kusafiri na Rais wa nchi! Tunashindwa na vyuo vidogo wao walituma wawakilishi! Halafu watu wanaenda Poland, kutafuta nini??

Kuna huyu M-Ethiopia wenu mlimuweka hapo. Huyu bwana yuko hapa kuharibu chuo. Yaani amehakikisha kwamba anajipenyeza mpaka amewekwa kwenye nafasi ambayo imetungwa ili mradi tu awe juu. Hela zote za SAUT ziko chini yake. Kama hakupendi atahakikisha anakunyanyasa na kukutungia uongo mpaka kama sio mvumilivu unahama chuo. Maprofesa wanahama kwa sababu yake (Bilame, Tibategeza, Mbasa, Beda, wote hao maprofessor wazuri tu, n.k!) na wangekuwa wengi tu kama wengine wasingekuwa wabishi kuondoka. Anakutungia uongo na ubaya wenyewe hata akikutungia uongo uulizwi unashtukia tu unapata adhabu mpaka unahama. Yeye hana nia nzuri na chuo yuko hapa kukiua. Muulize mfanyakazi yoyote wa SAUT atakwambia. Akiona tu kuna mhadhiri mahiri basi yeye atampania huyo mpaka amvunje vunje. Muulize DVCAA, DVCAF. Amehakikisha anawashusha wamekuwa wadogooo. Vitu wa academics Makamu wako anamuuliza yeye badala ya DVCAA. Mkikaa kwenye kikao (hata Seneti) mkitoa maamuzi yeye anakwenda nyuma nyuma anamfanya Makamu mkuu wa Chuo anabadilisha mnabaki mnashangaa tu. Nimeshasikia viongizi wakiuliza sasa tunakaa Vikao vya nini? Father Nkwera kidogo alikuwa anajitahidi kulinda hadhi ya vikao lakini siku hizi utakuta watu hata wasiostaili kuingia senate wanaingia ili wapate posho. Kuna msichana wa kikenya ana cheo cha Director wa international sijui kitu gani. Ukiuliza ofisi yake iko wapi huioni? Safari zote za nje anakwenda yeye peke yake, halafu makamu wako anamsifia kuwa anafanya kazi nzuri, sijui ni ipi na vigezo vya wanaofanya kazi nzuri sijui ni vipi? Tafadhali Mhashamu Baba Askofu rudisha hadhi ya chuo hiki. Kuna wafanyakazi wengine hawajalipwa gratuity hata moja, ukitaka kujua wanaofaidi ni wapi itisha list ya waliolipwa na ambao hawajalipwa, utakuwa huko administration wamelipana wote hata huyo m-ethiopia na rafiki zake, wakati huo huo kuna wafanyakazi hawajalipwa hata mara moja, kwa kisingizio cha mikopo, sasa wataishije kama hawajalipwa graituity zao si lazima wakope, basi wanakomeshwa hapo. Ila wao huko juu wamelipana wote. Sasa hichi ni chuo chA DINI kweli? Kuna walimu wanafundisha weekend, jumamosi na jumapili wakati watu wengine kama huyo m-ethiopia wako nyumbani, kulipwa nao nasikia imekuwa shida wanalalamika sidhani kama wameshalipwa, kazi wamefanya lakini M-ethiopia hataki kuwalipa anawapa sababu mbalimbali ili wakate tamaa. Wakati wa graduation picha zinazopigwa na kupostiwa ni za hao viongozi tu na wala sio wahadhiri ambao wanafanya kazi kubwa mpaka hao wanafunzi wanahitimu. Sasa hali kama ni hiyo walimu wataacha kuuza mitihani na notes? Wataacha kukimbia? Wataacha kukitukana chuo kila wanapopata fursa?

Kwenye vitivo/ndaki ndio usiseme. Viongozi hawana wanachofanya ni kukaa kwenye vikao na kula chakula na kupata posho, ila waulize wakueleze kuhusu ndaki zao, hawana habari. Kuna huyo mmoja ni msukuma na chapombe sana, ila bosi anajifanya kama hajui kuwa huyu mtu hafai. Anamlinda tu watu wamesema wamechoka. We siku njoo ghafla waite hao wakuu wa vitivo uone kama wanajua kuhusu vitivo vyao. Utashangaa sana yaani aibu hata kuwalinganisha na wakuu wa vitivo kutoka katika vyuo vingine.

Miundo mbinu mibovu iliyochoka sana nakushauri Mhashamu Baba Askofu siku ukija usiishie tu ofisini. Pita madarasani, ofisi za walimu, vyooni, hostels, utajionea maanake walimu wanalalamika hata projectors za kugombania na ni mbovu, hazina tija. Na wanafunzi waliopita hapo chuoni zamani wanakishangaa chuo jinsi kilivyo na mazingira mabovu kabisa.

Makamu wa Chuo nae anachangia katika kukiharibu chuo. Alimwamini sana huyo M-Ethiopia na akaacha kuwasikiliza wasaidizi wake wakuu. Kuna maamuzi ambayo yanapitishwa na Senate yeye anayabadilisha pindi tu akiambiwa na M-Ethiopia. Nasikia viongozi wengine wanalalamika sasa tunapotezewa muda kwenye mikutano miingi ya nini? Aliamua kuhamisha kitengo cha admission kutoka kuwa chini ya mkuu wa taaluma wa chuo akakipeleka kwake. Sababu ni ipi? Hayo ndio matokeo ya kushauriwa na PA wake badala ya kushauriwa na watu wanaohusika. Pengine PA alimshauri kuwa “Mwamishe rafiki yangu umuweke chini yako ili aweze kuingia kwenye senate”. Hiyo ofisi nayo inatakiwa itazamwe upya ili iendane na hadhi yake. Nashauri ijulikane na iwe wazi nani anaingia kwenye Senate na nani haingii. Wajumbe kutoka vyuo shirikishi vya SAUT wanatushangaa sana. Na hili linaweza kumnalizwa kwa urahisi kwa kuangalia Rules ans regulations za Chuo.

Mtu anaitwa Director wa International Office wakati hata ofisi ya kufanyia kazi hana. Kila safari ya nje anaenda mwenyewe ila wenzie wakienda kanataka kujua. Kana kihelehele sana na bwana mkubwa anathubutu kukasimamisha mbele eti kanafanya kazi nzuri, ipi? Makama Mkuu wa Chuo kila ikitokea nafasi anamsimamisha PA wake eti anamshauri vizuri, vipi? Mbona chuo kinaoza? Where is the professionalisms? Kwa hiyo washauri wake anaowaamini ni PA wake na M-Ethiopia wengine wote wanaonekana hawafai? Projectors ni mbovu na hazitoshi kwa mahaitaji ya kufundisha. Ukiipata unakuta inaonyesha rangi ya njano. Chache sana hazizidi tano labda ndio nzima. Huyo M-Ethiopia anapelekewa maombi haya ya kununua bulb, projectors anakataa. Watu wanadai haki zao anakataa, wakati yeye safari zake zote akitaka anakwenda na anajilipa vizuri.

Mwenyekiti wa Baraza la chuo kwa kweli ameshachokwa sana. Hasaidii kitu. Yeye kila siku ni kufoka tu. M-ethiopia akishamjaza maneno basi anakuja amejitayarisha kwa vita. Kila hoja ya kukijenga chuo yeye anaipiga chini!! Mimi nawaonea huruma sana viongozi wengine wa chuo ambao wana mikutano kibao, utekelezaji zero. Huko Lavoure Centre mna mpango gani? Ukija chuoni usiku unakuta mlinzi yuko gizani, hakuna bulb kwenye jingo la taaluma. Hata bulbs zinawashinda? Karibu chuo kitapitwa na ofisi za mtaa!

Tafadhali fanya kitu kuhusu hichi chuo chetu kilichotulea. Kwa hali hii ilivyo,kitakufia na ukizingatia serikali inajenga vyuo vingine 14. Kazi ipo. Amkeni kutoka usingizini SAUT. Na muanze kuwajali wahadhiri wenu, wao hawana mahali pa kula bure na wanafamilia za kutunza.

Pole kwa hii barua ila nimekaa naangalia mambo yanavyokwenda roho inaniuma. SAUT ni chuo change kimenisomesha na kunipa kazi. Nataka kuona hadhi yake inarudi. Sikutaka kupeleka kopi ya hii barua sehemu nyingine husika ila nikaona kwanza nikuletee wewe najua utafanya marekebisho ili chuo kiendelee kukua. Wasaidie pia wanafunzi wa certificate na diploma. Hao ndio wamesahauliwa na walimu wengi wanaowafundisha hawana hata sifa za kuwa wahadhiri! Walipataje kazi hawa? Au ni kwa sababu wanafanya kazi SAUT? Angalia hii isikiponze chuo. Kuwe na mkakati mzuri wa kupata wahadhiri wazuri na wahadhiri wakiahidiwa kufanya kazi na kulipwa basi hizo ahadi zitekelezwe sio kuwafanya wajinga mnawafunja morali.

Wako katika ujenzi wa Jiji la Mungu

Mdau mkereketwa.

CC: Secretary General of TEC: Fr, Charles Kitima, Minister of Education, Chairman TCU.
 
Hakuna haja ya kujitetea hapa kwa kuonyesha kwamba kuna watu wanagombea madaraka. This is very low and poor. Kwani haya mambo yanayolalamikiwa hayapo? tui akichukua time kuandika a well written story kama hii, bado unaweza kujitetea hapa? Very poor. THios is Kwa mfano mambo 2

1. Linalolalamikiwa kuhus PA wa VC ni kweli au sio kweli? Ni kweli alisafiri kwenda nje na nchi? Kufanya nini? Anastahili?

2. Ethjiopian": Ni kweli Yupo? anapataje visa, vya kufanya kazi Tanzania? Hakuna watanzania wenye uwezo wa kufanya kazi yake? Ni kweli anahonga kupata visa? Hili linamuhusu Kamishan mkuu wa Migration.

. Ma Professor waliiondoka kwa fitina. Huoni kwamba hii itaangusha credibility ya SAUT University? Na ni kweli waliondoka kwa Fitina? In cases committee ikiundwa, haya yate yatakuwa wazi. Ni mategemeo kwamba, SAUT kama flagship ya Christianity Education in Tanzania, haiuwezi kufa hivi hivi, TEC watalifanyia kazi. Ila kwa kuwa limegusa quality of educationb, TCU linawahusu. Na kwa kuwa limehusu Idara ya Uhamiaji kumfuga Raia wa Ethiopia, Idara ya UHAMIAJI linawahusu. Let us wait and see
 
Aliyeandika Iyo Barua ni PETER KAFUMU, DVCAA Na CREUTUS,
pale Chuo kuna vita ya madaraka, kuna genge la watu Wanataka madaraka Kwa hali na mali, wameamua kuwachafua wenzao ili wao wachukue madraka yao, kabla ya huu utawala wa sasa kuingia madarakani chuo kilikua kinaenda kufa kabisa kilikua hakilipi mishahara ata kwa miezi mitatu walimu wanadai tu, walimu hawakua promoted kwa 10 wote walikua assistance lecturers tu, majengo yalikua yale yale ya mwaka 47, ila toka uongozi huu uingie walimu wanalipwa kwa wakati, idadi ya wanafunzi kusajiliwa imeongezeka, kuna majengo yameongezeka, chuo kimejengewa uzio ambao maduka ambayo yanatumika kama kitega uchumi cha chuo, na mengineyo mazuri, shida iliyopo pale chuo kwamba nafasi zote kubwa wanataka zishikwe na mapadri tu, iligenge la watu watatu ndio lina injinia Ili jambo.
This is very poor. Hakuna haja ya kujitetea hapa. Acha comitees (TEC, TCU, Uhamiaji) zifanyie kazi hizi tuhuma. Kama sio kweli au ni kweli itajulikana.
 
Aliyeandika Iyo Barua ni PETER KAFUMU, DVCAA Na CREUTUS,
pale Chuo kuna vita ya madaraka, kuna genge la watu Wanataka madaraka Kwa hali na mali, wameamua kuwachafua wenzao ili wao wachukue madraka yao, kabla ya huu utawala wa sasa kuingia madarakani chuo kilikua kinaenda kufa kabisa kilikua hakilipi mishahara ata kwa miezi mitatu walimu wanadai tu, walimu hawakua promoted kwa 10 wote walikua assistance lecturers tu, majengo yalikua yale yale ya mwaka 47, ila toka uongozi huu uingie walimu wanalipwa kwa wakati, idadi ya wanafunzi kusajiliwa imeongezeka, kuna majengo yameongezeka, chuo kimejengewa uzio ambao maduka ambayo yanatumika kama kitega uchumi cha chuo, na mengineyo mazuri, shida iliyopo pale chuo kwamba nafasi zote kubwa wanataka zishikwe na mapadri tu, iligenge la watu watatu ndio lina injinia Ili jambo.
Sijui watanzania tumerogwa na nani tu. Wewe u mmoja kati ya walamba makalio ya muethiopia, na ndiyo maana unaropoka hayo.

Tena umechochea moto kwa kuongeza petrol. Wengine hatukuwa na muda wa kupambana na huu uzandiki unaonendelea hapa SAUT maana kwa umri wangu 27yrs nipo busy kusaka ajira serikalini, si leo wala kesho Mungu atafungua njia nitatoka SAUT

Ila uko sahihi, nyie walamba makalio ya muethiopia hamdai hata senti moja ya gratuity ila wapo wanaodai gratuity hadi za mikataba minne na zaidi.

Watu wamebadilishiwa mikataba kuwa 13th cheque ambapo sheria inataka walipwe madai yao ya nyuma ndo wabadilishiwe terms, wakalipa wachache wengine robo, wengine nusu, wengine hamna kabisa... full double standards... haya na hili njoo ubishe ewe mnufaika usodai hata senti tano.

Anayesimamia VC ni mwanasheria ila anavunja sheria. Njoo ubishee

Ushahidi tunao, haya ww tupe ushahidi wako juu ya kumtuhumu DVCAA, PETER NA CRETUS... Tupeee

Kisa wewe umelipwa gratuity na advance hadi mkataba ambao hujaumaliza ndo unakuja kutudharau sisi kwa kejeli?

Nani katuroga watanzania???

Hakuna foreigner SAUT anayedai gratuity, ushahidi tunao, vipi wewe, mwenzetu... unadai eti alotuma ujumbe hana adabu hata kwa Askofu kansela ... kweli? Sisi watanzania kutukanwa na muethiopia ni adabu, ila wadau kutoa maoni yao ni ukosefu wa nidhamu,

watanzania tumerogwa na nani? Anatukana wafanyakazi hadharani huyo muethiopia... hayo n manukato ndugu mlamba makalio yake, au siyo?

Saizi kuna foreigner mmoja kaja juzi na kupewa ubosi saizi anapiga makofi wanafunzi... hayo ni manukato siyo???

Huyo PA anayesemwa anafanyia jeuri watu, hafanyi kazi, akikumbushwa majukumu yake anashtaki kwa VC, kisha wanaitwa na VC na kutukanwa kuwa wamwache maana anafanya kazi kubwa sana... kweli???

Mie nina imani na experience yangu ya six years hapa one day serikalini nitapata tu.

Kama haya yanayosemwa hayapo kama unavyodai, ulikuwepo kwenye kikao kilichofanyika M15 wahadhiri walivyolalamika na double standards za SAUT? Ulimuona muethiopia alivyovuja jasho kisha kuanza kumuomba Noel amteteee??? Watanzania tumerogwa na nani???

Bora ukae tu kimya, maana u kati ya walamba makalio, endelea na kazi yako hiyo usipinge ukweli uliopo SAUT. Waache wenye chuo waone cha kufanya, japo nahisi watapotezea tu maana muethiopia huwa anawajaza maokoto ya hatari, ndo maana hata hawajisumbui na hali za wahadhiri na chuo kwa ujumla.

Sasa endelea kuchochea, sisi tuombe interviews bbc kabisa, tuyaweke hadharani.

Nani katuroga watanzania???
Aliyeandika Iyo Barua ni PETER KAFUMU, DVCAA Na CREUTUS,
pale Chuo kuna vita ya madaraka, kuna genge la watu Wanataka madaraka Kwa hali na mali, wameamua kuwachafua wenzao ili wao wachukue madraka yao, kabla ya huu utawala wa sasa kuingia madarakani chuo kilikua kinaenda kufa kabisa kilikua hakilipi mishahara ata kwa miezi mitatu walimu wanadai tu, walimu hawakua promoted kwa 10 wote walikua assistance lecturers tu, majengo yalikua yale yale ya mwaka 47, ila toka uongozi huu uingie walimu wanalipwa kwa wakati, idadi ya wanafunzi kusajiliwa imeongezeka, kuna majengo yameongezeka, chuo kimejengewa uzio ambao maduka ambayo yanatumika kama kitega uchumi cha chuo, na mengineyo mazuri, shida iliyopo pale chuo kwamba nafasi zote kubwa wanataka zishikwe na mapadri tu, iligenge la watu watatu ndio lina injinia Ili jambo.
Sijui watanzania tumerogwa na nani tu. Wewe u mmoja kati ya walamba makalio ya muethiopia, na ndiyo maana unaropoka hayo.

Tena umechochea moto kwa kuongeza petrol. Wengine hatukuwa na muda wa kupambana na huu uzandiki unaonendelea hapa SAUT maana kwa umri wangu 27yrs nipo busy kusaka ajira serikalini, si leo wala kesho Mungu atafungua njia nitatoka SAUT

Ila uko sahihi, nyie walamba makalio ya muethiopia hamdai hata senti moja ya gratuity ila wapo wanaodai gratuity hadi za mikataba minne na zaidi.

Watu wamebadilishiwa mikataba kuwa 13th cheque ambapo sheria inataka walipwe madai yao ya nyuma ndo wabadilishiwe terms, wakalipa wachache wengine robo, wengine nusu, wengine hamna kabisa... full double standards... haya na hili njoo ubishe ewe mnufaika usodai hata senti tano.

Anayesimamia VC ni mwanasheria ila anavunja sheria. Njoo ubishee

Ushahidi tunao, haya ww tupe ushahidi wako juu ya kumtuhumu DVCAA, PETER NA CRETUS... Tupeee

Kisa wewe umelipwa gratuity na advance hadi mkataba ambao hujaumaliza ndo unakuja kutudharau sisi kwa kejeli?

Nani katuroga watanzania???

Hakuna foreigner SAUT anayedai gratuity, ushahidi tunao, vipi wewe, mwenzetu... unadai eti alotuma ujumbe hana adabu hata kwa Askofu kansela ... kweli? Sisi watanzania kutukanwa na muethiopia ni adabu, ila wadau kutoa maoni yao ni ukosefu wa nidhamu,

watanzania tumerogwa na nani? Anatukana wafanyakazi hadharani huyo muethiopia... hayo n manukato ndugu mlamba makalio yake, au siyo?

Saizi kuna foreigner mmoja kaja juzi na kupewa ubosi saizi anapiga makofi wanafunzi... hayo ni manukato siyo???

Huyo PA anayesemwa anafanyia jeuri watu, hafanyi kazi, akikumbushwa majukumu yake anashtaki kwa VC, kisha wanaitwa na VC na kutukanwa kuwa wamwache maana anafanya kazi kubwa sana... kweli???

Mie nina imani na experience yangu ya six years hapa one day serikalini nitapata tu.

Kama haya yanayosemwa hayapo kama unavyodai, ulikuwepo kwenye kikao kilichofanyika M15 wahadhiri walivyolalamika na double standards za SAUT? Ulimuona muethiopia alivyovuja jasho kisha kuanza kumuomba Noel amteteee??? Watanzania tumerogwa na nani???

Bora ukae tu kimya, maana u kati ya walamba makalio, endelea na kazi yako hiyo usipinge ukweli uliopo SAUT. Waache wenye chuo waone cha kufanya, japo nahisi watapotezea tu maana muethiopia huwa anawajaza maokoto ya hatari, ndo maana hata hawajisumbui na hali za wahadhiri na chuo kwa ujumla.

Sasa endelea kuchochea, sisi tuombe interviews bbc kabisa, tuyaweke hadharani.

Nani katuroga watanzania???
 
To.President ,Bishop Wolfgang Pisa
Tanzania Episcopal Conference(TEC)
Kurasini Center
P.O.BOX 2133
Dar Es Salaam.
12/1/2025
YAH:TUNAOMBA UINGILIE KATI SAUT MWANZA.
Kwako Mkuu wa chuo ,pole na majukumu,nimeangalia andikokwenye jukwaa la jamii forums kuhusu chuo cha Saut,nimeamua kufatilia Sakata hilo kwa ukaribu kama mpenzi wachuo maana nimesoma hapo miaka kadhaa iliyopita kwanza nikabaini kuna mgogoro wa kiuongozi kuna kundi linahitajiumakamu mkuu wa chuo na cheo cha financial controller ambacho kuna mtu ametajwa kama mtu wa Ethiopia ,
Nimesikitishwa na watu wazima hawa wasiyokuwa na adabuhata kidogo kufikia hatua yakumuita askofu ambaye nimwenyekiti wa counsel ya chuo kuwa anajinenepea hidhi nidharau na utovu mkubwa sana wa kimaadili kwa kundi hililinalosaka Madaraka kwa nguvu na mapadre kuwemonimefedheheka sana .
Mh Raisi wa TEC Chuo hichi cha saut kabla ya uongozi huu waBalozi mwaka 2018 kilikuwa kikiongozwa na padri nadhaniwewe unajua chuo watumishi hata mshahara tu ulishindikanampaka miezi mitatu hujalipwa walimu walikata tamaa kabisa ilatangu uongozi huu uingie madeni yote yalilipwa na mishaharainalipwa kwa wakati ya kila mwezi.
Walimu hawakuwahi kuwa promoted kwa miaka kumi lakini katika uongozi huu imefanyika kila linalowezekana limefanyikakisheria wakuwa promoted.
Madarasa yamejengwa na mengine yamekuwa mentained bilashida yoyote, na ikumbukwe battle iliyokuwepo kati ya chuo naserikali mpaka ikafikia hatua wanafunzi TCU Ikawa inaletawachache ambao hata wakilipa ada haiwezi kuendesha chuoimefanyika juhudi kubwa sana ya balozi na serikali mpaka haliimerejea vizuri sana uhaba wa wanafunzi imekuwa historia namahusiano na serikali yamekuwa Chanya,
Mpaka naandika barua hiii kwako nimefatilia deni la chuonaomba kukueleza wakati uongozi wa balozi unaingia deniambalo chuo kilikuwa kinadaiwa ni bilioni 49 kwa muda huoanaeitwa mtu wa Ethiopia na makamu mkuu wamelifikisha denihilo bilioni 21 hii siyo hatua yakubeza kamwe najua wanaumiawamebanwa na huyo muethiopia hawapumui pesa inatoka kwautaratibu ili malengo na uendesheji wa chuo utimie kwaukamilifu bila mikopo.

Tujiulize kwa Pamoja imetajwa safari ya Poland hapa kuwawameenda wasiyo husika je wanajua ilikuwa inahusu nini , safari hiyo Mh Raisi wa baraza la maskofu ilidhaminiwa naErasmus fund kwa ajili ya chuo kikuu cha usafirishaji cha Poland kinaitwa international university of transport and logistics kilichopo wclavas City nchini Poland na safari hiyoimezaa matunda wanafunzi 12 na walimu 3 watafanya exchange program wataenda Poland kwa gharama za hicho chuo nawatatengeneza maabara ya transport and logistics hapo saut kwaajili ya nchi za Africa mashariki.
Mh Raisi kumekuwa na ujinga mwingi sana wa haka kakundikanakoongozwa na padre wako cretus na Dvcaa anayeitwaHosea Rwegoshora badala kutoa maoni yao kwenye proper forums wameanzisha vigenge visivyo na tija na chuo na sisiproducts za chuo hicho hatuwezi kuacha kukiokoa chuo ujingaunapofanywa na watu ambao hata uwezo wa leadership hawanamaana hata huyo dvcaa historia yake inajulikana tangu akiwaopen University mpaka anakuja Saut anadanganywa anadhanianaweza kuwa Makamu Mkuu wa Chuo.
Mh raisi juzi tu umeandikiwa na kikundi hicho hicho barua yatarehe 6 january 2025 yakukutaka umteue padre kutoka singidaanayeitwa masoy muhuri wa chuo umefojiwa na sahihiimesainiwa kwa niaba ya makamu mkuu wa chuo maanawalishindwa kuiga sahihi yake lengo lao nikutaka wapateanaeweza kupata njia yakujua operation za pesa zikoje maanawanahisi aliyepo ambaye ni padre pia hawapi taarifa pia stahikiza fedha ili waweze kuchochea chuki dhidi ya huyo muethiopiana makam mkuu wa chuo.
Mh raisi haka kakundi lazima kashughulikiwe ili chuo kiwesalama kamekuwa na mgogoro usio isha ukikutana na dvcaakazi yake ni kulalamika all the way kuonyesha kuwa boss wake hamna hanachofanya apewe yeye sasa umakam makuu wa chuoaongoze chuo tuone maana anajitanabaisha kuwa anaweza nakundi limemuahidi hivyo.
Wako katika ujenzi wa jiji la Mungu
Na mdau wa elimu Nchini Tanzania.

Cc:Secretary General of TEC
Jibu Hoja msingi! Acha kutudanya hapa.

Unapo sema mapadri wananganaia vyeo ,Je hii ni Taasisi Yao au ni Taasisi ya nani?
Je wanahaki ya kuhoji wakiona mambo yanenda mrama au hawana haki? Ulitaka wao wasiwe na haki ndani ya chuo chao?
Na hao mapadri ni wangapi?

Deni ni shida? analipa deni kwa hela zake au hela tunazo tolea Jasho wote?

Taasisi yoyote haikosi madeni madeni ni ishara ya uhai wa Taasisi husika, madharani deni haliwezi kuweka na kuupuza ustawi wa watu. Hata nchi zinadaiwa je hazifanyi maendeleo? Haziongezi mishahara?

Tangu Kitima aondoke miaka 10 hatujakngezewa mishahara na unasifiwa kwa sababu mnapata marupu na posho wewe na jamaa zako.

Wewe hujawahi kopa? Je ulipo kopa uliacha kula ? Acheni uozo uonekane

Poland ,Je wewe Ndo ulistahili kwenda au alipaswa kwenda mtu husika wa fani ulizo taja?

Je unapo sema muhuri umefojiwa , askofu mwenye huyo mtumishi alimruhusu kuondoka bila kudhibitishwa na mamlaka husika?

Achana na propaganda za zamani , acha kujitetea , wajibika chukua hatua stahiki.

Niukweli Balozi kwa namna Moja mmemuingiza kwenye shida kwa sababu ya mambo yenu! Upole wake mmeutumia vibaya, wema wake mmeutumia ndivyo sivyo.

Alisikika mlevi mmoja akisema Acha inyeshe tujue panapo vuja na akakazia mfa maji haachi kutapatapa.

Ni hili halihusiani na mtu yoyote bali linamuhusu mmliki muacheni achunguze ajue ukweli ni ipi na akitaka ushaidi atuulize sisi tulio Fanya kazi kwa miaka takribani 15 hapa saut tangu enzi za Fr Kitima.
Msimpangie majibu nyingi.

Nawe Baba Mkuu Wa chuo usikubali kuwaisikiliza wao tu unda tume au njoo ziara na wekeza nguvu isio punguza wiki Moja kaa na Kila kundi utapata majibu sahii.

Kutumia neno ujenzi wa Jiji la Mungu wakati manalibomoa niaibu na fedheha mbele za Mungu. Ongopeni na badilikeni.

Cc TEC secretariete & Idara ya Elimu Baraza la maaskofu, na walio kua watangulizi yaani wakuu wa vyuo wote.
 
Kweli Balozi VC ni mpole sana, na upole wake ndo unaomponza.

Huyu muEthiopia aliwahi kumdharirisha Professor mmoja akaenda Immigration kuhoji juu yake, wakamwambia office ya Immigration Tanzania wanazo kesi zake nyingi za kudharirisha wafanyakazi wa SAUT walipoanza fuatilia undani, Balozi Mpole akawa anajisomba Uhamiaji kila siku kumtetea...

Hii inaitwaje kitaalamu? Naye ni mmoja wa wanaojazwa maokoto na Muethiopia (maokoto ya ada na mapato ya chuo - hazitoi Ethiopia, ni za watanzania) ndo maana malalamiko ya watu wa chini si shida zake?

Watanzania tumerogwa na nani?

Halafu mnakuja na kusema uongozi huu umejenga majengo mapya, majengo which? majengo what? Majengo where?

Tukiachana na Majengo ya Rev. Dr. Fr. Kitima, M14 na M15 ni project za Professor Mbassa.

Ukweli mchungueee... bishaaa.

Bado nauliza.... Je ni nani katuroga watanzania????
Na yupo mkuu waidara mmoja mnaijeria ambae taarifa zake zipo anavyo nyayasa wanafunzi na walimu SAUT. Kuna ushahidi wakutosha kutoka kwa wanafunzi na walimu kwa vitendo vyake vya unyanyasaji je unabisha na hilo. Taarifa zipo zakutosha sana .
 
Kwa maana hii, huyu mu Ethiopia kuna namna ambavyo anaweza kuendelea kuishi Tanzania na kuweza kudharirisha Walimu na wafanyakazi wa Kitanzania atakavyo. Ni matumaini kuwa Serikali sikivu na yenye Busara kubwa iunayoongozwa na Mama yetu mmpendwa, amelisoma hilo na atalifanyia kazi kupitia kwa Mkuu wa Uhamiaji
 
Back
Top Bottom