Mambo yanayoisibu SAUT Mwanza

Mambo yanayoisibu SAUT Mwanza

Mambo ya aibu kabisa haya.
Wahusika hapo TEC hili mlifanyie KAZI.
Probably wanafanyia kazi. Hivi Mshahara wa yule Mhebeshi umepitishwa na nani? Analipa Kodi Ya serikali yetu Tukufua ya MAma Samia Suluhu Hassan? Ni kweli unamstahili? Ana qualifications za kuwa Financial Controller? Ina maana yeye ana uwezo zaidi ya DVC (PFA)? Hivi hili linajulikana? Inawezekanma wapoi mtu mgeni akaje Tanzania na mu manupulate watu? Yaani vyombo vyote ya TEC wameshindwa kuligundua hili?
 
Inakuaje mtu mmoja anajifanya Mungu mtu kwa kauli mbovu na lugha zisizo rafiki za kuambiwa binadamu nikisikia hivyo nakumbuka mambo ya Mwalimu Simba wa Tabora polytechnic college 😁
 
Duh aiseee ndoaana hawafundishi vizuri kumbe wana stress
 
To: President, Bishop Wolfgang Pisa, OFM

Tanzania Episcopal Conference (TEC)

Kurasini Centre

P.O Box 2133

Dar es Salaam.

7 January 2025

Mhashamu Baba Askofu Pisa,



YAH: MAMBO YANAYOISIBU SAUT MWANZA.​

Tumsifu Yesu Kristo.

Kwanza nikupe hongera kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa TEC.

Mimi ni mdau wa SAUT Mwanza ambae nimekaa na kufanya kazi SAUT tangu inaanza na pia nimesoma hapa. Kwa hiyo ninapoandika hii barua naandika kwa uchungu kwa sababu naona mbele ya hiki chuo kuna giza sana na hakuna anaeonekana kujali. Kama usipoangalia wewe kama Mkuu wa SAUT, chuo chako ambacho zamani kilikuwa kinasifika kitakufa. Hivyo basi nimeona kama mkatoliki mkereketwa niongee na wewe kidogo kimaandishi.

Ninashukuru sana kuwa siko kwenye nafasi yoyote hapa chuoni kwa hiyo ninaangalia na kusikiliza malalamiko nikiwa nimekaa pembeni sasa naona yanazidi. Watu wengi wanajiuliza hivi hawa maaskofu na mapadre hawaoni uozo huu ulioko hapa chuoni au kuna nini? Au ni njama mahususi za kuhakikisha kwamba uongozi wa sasa, ili watu wapate cha kuongea? Watu wengi sasa tunamkumbuka Kitima enzi zake mtu ulikuwa unajisikia kuitwa mfanyakazi wa SAUT. Sio sasa.

Sasa ni vilio tu na malalamiko. Kila mtu anaapply kazi hata kama ni ya chini yake ili mradi tu aondoke SAUT! Kwa kweli hamuwatendei haki wanafunzi wanaojiunga hapa pamoja na walimu wa hapa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu kuliko chuo chochote duniani! Yaani ni kama vile yatima wasio na watu wa kuwasemea. Wakati Mwenyekiti wa Council akizidi kunenepa walimu wa SAUT ambao wengi wao wana wanafunzi zaidi ya mia tano wanakonda na wana dhiki za kupitiliza. Hivi kosa la walimu hawa ni nini? Kuipenda SAUT?

Walimu wenye wanafunzi zaidi ya mia tatu waliahidiwa kulipwa hela kidogo ya motisha kwa kazi kubwa wanayofanya, lakini matokeo yake hawajalipwa hata senti tano. Hivi ukiangalia kwa undani unafikiri hawa walimu wanasahihisha inavyotakiwa kweli au wanaweka tu marks. Motisha iko wapi kwa kazi kubwa wanayoifanya? Badala ya walimu hawa kusifiwa kwa kazi wanazofanya, wanasifiwa wasichana ambao wako ofisi ya makamu mkuu wa chuo au ni rafiki wa karibu wa PA wa makamu mkuu wa chuo. Makamu Mkuu wa chuo anamsifia sana Personal Assistant (PA) wake kuwa anamshauri vizuri na anafanya kazi sana, kila akikaa ana kazi ya kumsifia huyo dada, mpaka watu wanajiuliza huyu mzee kapewa nini? Kwa kweli anaudhi. Tungetegemea awasifie wafanyakazi wote wanaofanya vizuri. Mbona hafanyi hivyo.

Juzi juzi, PA wa Mkuu wa Chuo alikwenda nje ya nchi na watu wengine wawili, watu wakajiuliza amekwenda kufanya nini? Hata hatujamwona kutoa report yoyote. Kichekesho kingine, kuna M-Ethiopia ambae ndio kila mtu anasema anaendesha chuo na anakiharibu, eti yeye alikataliwa visa kwenda kwenye hiyo safari, nadhani akatetewa na Makamu mkuu wa Chuo akapata viza, wakati wenzie wanarudi, yeye ndio akaenda hiyo safari, kufanya nini?

Mhashamu baba Askofu hao ndio wanaokula hela za chuo kirahisi, ila walimu ambao ndio wanafanya kazi kubwa wakiomba hela za safari wananyimwa! Kuna watu huwa wanaenda TCU kwa sababu wanakiwakilisha chuo kwenye workshop Fulani au training, wakati mwingine wanaomba pesa wananyimwa!! Wakati wameenda kwa ajili ya Chuo!

Unafikiri hao viongozi watakuwa wana motisha gani ya kukifanyia chuo kazi? Kuna wakati juzi juzi Rais alikua anasafiri kwenda nje na wanataaluma kutoka idara za Kiswahili za vyuo mbali mbali. Ilikuwa safari ya kwenda Cuba kukuza Kiswahili na kujenga mahusiano na kutafutia wahadhiri wetu tonge waende wakafundishe huko. SUongozi wa AUT walimnyima hela mkuu wa idara ya Kiswahili! Jamani, kuna bahati nyingine bora kuliko kusafiri na Rais wa nchi! Tunashindwa na vyuo vidogo wao walituma wawakilishi! Halafu watu wanaenda Poland, kutafuta nini??

Kuna huyu M-Ethiopia wenu mlimuweka hapo. Huyu bwana yuko hapa kuharibu chuo. Yaani amehakikisha kwamba anajipenyeza mpaka amewekwa kwenye nafasi ambayo imetungwa ili mradi tu awe juu. Hela zote za SAUT ziko chini yake.

Kama hakupendi atahakikisha anakunyanyasa na kukutungia uongo mpaka kama sio mvumilivu unahama chuo. Maprofesa wanahama kwa sababu yake (Bilame, Tibategeza, Mbasa, Beda, wote hao maprofessor wazuri tu, n.k!) na wangekuwa wengi tu kama wengine wasingekuwa wabishi kuondoka. Anakutungia uongo na ubaya wenyewe hata akikutungia uongo uulizwi unashtukia tu unapata adhabu mpaka unahama.

Yeye hana nia nzuri na chuo yuko hapa kukiua. Muulize mfanyakazi yoyote wa SAUT atakwambia. Akiona tu kuna mhadhiri mahiri basi yeye atampania huyo mpaka amvunje vunje. Muulize DVCAA, DVCAF. Amehakikisha anawashusha wamekuwa wadogooo. Vitu wa academics Makamu wako anamuuliza yeye badala ya DVCAA.

Mkikaa kwenye kikao (hata Seneti) mkitoa maamuzi yeye anakwenda nyuma nyuma anamfanya Makamu mkuu wa Chuo anabadilisha mnabaki mnashangaa tu. Nimeshasikia viongizi wakiuliza sasa tunakaa Vikao vya nini? Father Nkwera kidogo alikuwa anajitahidi kulinda hadhi ya vikao lakini siku hizi utakuta watu hata wasiostaili kuingia senate wanaingia ili wapate posho.

Kuna msichana wa kikenya ana cheo cha Director wa international sijui kitu gani. Ukiuliza ofisi yake iko wapi huioni? Safari zote za nje anakwenda yeye peke yake, halafu makamu wako anamsifia kuwa anafanya kazi nzuri, sijui ni ipi na vigezo vya wanaofanya kazi nzuri sijui ni vipi? Tafadhali Mhashamu Baba Askofu rudisha hadhi ya chuo hiki. Kuna wafanyakazi wengine hawajalipwa gratuity hata moja, ukitaka kujua wanaofaidi ni wapi itisha list ya waliolipwa na ambao hawajalipwa, utakuwa huko administration wamelipana wote hata huyo m-ethiopia na rafiki zake, wakati huo huo kuna wafanyakazi hawajalipwa hata mara moja, kwa kisingizio cha mikopo, sasa wataishije kama hawajalipwa graituity zao si lazima wakope, basi wanakomeshwa hapo. Ila wao huko juu wamelipana wote.

Sasa hichi ni chuo chA DINI kweli? Kuna walimu wanafundisha weekend, jumamosi na jumapili wakati watu wengine kama huyo m-ethiopia wako nyumbani, kulipwa nao nasikia imekuwa shida wanalalamika sidhani kama wameshalipwa, kazi wamefanya lakini M-ethiopia hataki kuwalipa anawapa sababu mbalimbali ili wakate tamaa. Wakati wa graduation picha zinazopigwa na kupostiwa ni za hao viongozi tu na wala sio wahadhiri ambao wanafanya kazi kubwa mpaka hao wanafunzi wanahitimu. Sasa hali kama ni hiyo walimu wataacha kuuza mitihani na notes? Wataacha kukimbia? Wataacha kukitukana chuo kila wanapopata fursa?

Kwenye vitivo/ndaki ndio usiseme. Viongozi hawana wanachofanya ni kukaa kwenye vikao na kula chakula na kupata posho, ila waulize wakueleze kuhusu ndaki zao, hawana habari. Kuna huyo mmoja ni msukuma na chapombe sana, ila bosi anajifanya kama hajui kuwa huyu mtu hafai. Anamlinda tu watu wamesema wamechoka. We siku njoo ghafla waite hao wakuu wa vitivo uone kama wanajua kuhusu vitivo vyao. Utashangaa sana yaani aibu hata kuwalinganisha na wakuu wa vitivo kutoka katika vyuo vingine.

Miundo mbinu mibovu iliyochoka sana nakushauri Mhashamu Baba Askofu siku ukija usiishie tu ofisini. Pita madarasani, ofisi za walimu, vyooni, hostels, utajionea maanake walimu wanalalamika hata projectors za kugombania na ni mbovu, hazina tija. Na wanafunzi waliopita hapo chuoni zamani wanakishangaa chuo jinsi kilivyo na mazingira mabovu kabisa.

Makamu wa Chuo nae anachangia katika kukiharibu chuo. Alimwamini sana huyo M-Ethiopia na akaacha kuwasikiliza wasaidizi wake wakuu. Kuna maamuzi ambayo yanapitishwa na Senate yeye anayabadilisha pindi tu akiambiwa na M-Ethiopia. Nasikia viongozi wengine wanalalamika sasa tunapotezewa muda kwenye mikutano miingi ya nini?

Aliamua kuhamisha kitengo cha admission kutoka kuwa chini ya mkuu wa taaluma wa chuo akakipeleka kwake. Sababu ni ipi? Hayo ndio matokeo ya kushauriwa na PA wake badala ya kushauriwa na watu wanaohusika. Pengine PA alimshauri kuwa “Mwamishe rafiki yangu umuweke chini yako ili aweze kuingia kwenye senate”. Hiyo ofisi nayo inatakiwa itazamwe upya ili iendane na hadhi yake. Nashauri ijulikane na iwe wazi nani anaingia kwenye Senate na nani haingii. Wajumbe kutoka vyuo shirikishi vya SAUT wanatushangaa sana. Na hili linaweza kumnalizwa kwa urahisi kwa kuangalia Rules ans regulations za Chuo.

Mtu anaitwa Director wa International Office wakati hata ofisi ya kufanyia kazi hana. Kila safari ya nje anaenda mwenyewe ila wenzie wakienda kanataka kujua. Kana kihelehele sana na bwana mkubwa anathubutu kukasimamisha mbele eti kanafanya kazi nzuri, ipi? Makama Mkuu wa Chuo kila ikitokea nafasi anamsimamisha PA wake eti anamshauri vizuri, vipi? Mbona chuo kinaoza? Where is the professionalisms? Kwa hiyo washauri wake anaowaamini ni PA wake na M-Ethiopia wengine wote wanaonekana hawafai? Projectors ni mbovu na hazitoshi kwa mahaitaji ya kufundisha. Ukiipata unakuta inaonyesha rangi ya njano. Chache sana hazizidi tano labda ndio nzima. Huyo M-Ethiopia anapelekewa maombi haya ya kununua bulb, projectors anakataa. Watu wanadai haki zao anakataa, wakati yeye safari zake zote akitaka anakwenda na anajilipa vizuri.

Mwenyekiti wa Baraza la chuo kwa kweli ameshachokwa sana. Hasaidii kitu. Yeye kila siku ni kufoka tu. M-ethiopia akishamjaza maneno basi anakuja amejitayarisha kwa vita. Kila hoja ya kukijenga chuo yeye anaipiga chini!! Mimi nawaonea huruma sana viongozi wengine wa chuo ambao wana mikutano kibao, utekelezaji zero. Huko Lavoure Centre mna mpango gani? Ukija chuoni usiku unakuta mlinzi yuko gizani, hakuna bulb kwenye jingo la taaluma. Hata bulbs zinawashinda? Karibu chuo kitapitwa na ofisi za mtaa!

Tafadhali fanya kitu kuhusu hichi chuo chetu kilichotulea. Kwa hali hii ilivyo,kitakufia na ukizingatia serikali inajenga vyuo vingine 14. Kazi ipo. Amkeni kutoka usingizini SAUT. Na muanze kuwajali wahadhiri wenu, wao hawana mahali pa kula bure na wanafamilia za kutunza.

Pole kwa hii barua ila nimekaa naangalia mambo yanavyokwenda roho inaniuma. SAUT ni chuo change kimenisomesha na kunipa kazi. Nataka kuona hadhi yake inarudi. Sikutaka kupeleka kopi ya hii barua sehemu nyingine husika ila nikaona kwanza nikuletee wewe najua utafanya marekebisho ili chuo kiendelee kukua. Wasaidie pia wanafunzi wa certificate na diploma. Hao ndio wamesahauliwa na walimu wengi wanaowafundisha hawana hata sifa za kuwa wahadhiri! Walipataje kazi hawa? Au ni kwa sababu wanafanya kazi SAUT? Angalia hii isikiponze chuo. Kuwe na mkakati mzuri wa kupata wahadhiri wazuri na wahadhiri wakiahidiwa kufanya kazi na kulipwa basi hizo ahadi zitekelezwe sio kuwafanya wajinga mnawafunja morali.

Wako katika ujenzi wa Jiji la Mungu

Mdau mkereketwa.

CC: Secretary General of TEC: Fr, Charles Kitima, Minister of Education, Chairman TCU.
Umesagia watu kunguni vibaya mno kama sio majungu basi apo Chuo kinaenda kujifia tu.
Inaelekea watu wameendekeza mapenzi kwenye kazi.
Naamini watalifanyia kazi
 
Mm nikili, nime soma SAUT na nimefanya kazi SAUT hapo awali. NIKA ONDOKA. Anae haribu chuo cha SAUT, ni Dr. Andre Negussie tu. Huyo m-Ehiopia.
Alimfukuza Prof. Mbassa kutoka SUA. Huyu Prof , alikuwa na maono makubwa kwa SAUT. Ila alipigwa vita sanaaa..aka ondoka.
Huyo mu ethiopia, ali undiwa cheo ambacho hakipo ktk muundo wa uongozi wa chuo wa SAUT, FINANCIAL CONTROLLER (FC). Licha ya cheo hicho cha Fedha, ila Dr. Negussie hana elimu yoyote ya Biashara wala uhasibu, yeye ni wa Theology tu. Hata mwaka jana kazawadiwa u professor wa kugaiwa na Prof. Mahalu, japo hana publications zozote wala zenye hadhi ya u professor.
SAUT chini ya Prof. Costa Rick Mahalu, haina jipya ni Retired and tired.

Watanzania wenzangu naomba tuwe makini na Wageni tunao wa ajiri ktk taasisi zetu. Wengine siyo wazuri.

Toka 2021 hadi 2023 SAUT ime poteza vijana, walio bakizwa na Rev. Fr. Charles Kitima kama tutorials na kusomeshwa na kuwa wahadhiri, wenye uzoefu wa miaka 5 hadi 9, wame ondoka woteeeee karibu stafu 50. Idara ya Civil Engineering ime bidi warudishe wa staafu walio kuwa wame wafukuza. Kisa kuondoka vijana.

Walimu wanadai Gratuity za kuanzia mwaka 2014 hadi leo bado hajalipwa. Walimu wote walio acha kazi SAUT, wanadai SAUT. NSSSF huyo mu-ethiopia hapeleki michango ya staff. Hawa NSSSF pia ni JIPU. Hawafustilii michango ya staffs wa SAUT. Kazi ya NSSSF ni kula bata tu.

Kifupi SAUT ina uliuwa na Dr. Negussie, rafiki na classmate wa Askofu Kasala wa Geita.
 
Nimekimbuka chuo changu Pendwa.

Tulikuwa na mwalimu anaitwa Acran John Mtalaamu wa History.

Poleni sana
Wasalimie watu wa Malimbe
 
Back
Top Bottom