Mambo yanayokatisha tamaa kuwapa lifti baadhi ya watu

Mambo yanayokatisha tamaa kuwapa lifti baadhi ya watu

Wewe dada niliekupakia Dodoma na ukashukia chalinze na kuiba vocha zangu za mitandao mbalimbali. UTAKUFA NAKUHAKIKISHIA, Nitafute upone, unajijua. Jinga sana.
 
pole sana mkuu, ilikuwaje hii episode kama hutajali imwage hapa unaweza kusaidika. maduu kumbe nao hawajambo.
Natoka zangu Dodoma pale stendi ya karibu na Bungeni, nikasema hili jini kuliko kulitembeza kigavo gavo hadi Dar acha nilambe vichwa. Nikapakia nginja kaa 4 hivi mixer duuh mmoja alikaa siti ya mbele. Sasa kwenye daily ilikuwa kwenye dashboard nikawa nimeweka vocha za Voda, Yas na Airtel kama za 100k hivi almost. Huyo du alishukia Chalinze kumbe alishuka nazo muda tumeenda kuchimba dawa ye alibaki garini ndo muda nilojua alizibeba nafika Dar kuzisaka sizioni...nikawawakia sana wanangu wa Car wash Kuja kukumbuka kumbe ni Dada jizi alishuka nazo Chalinze...naenda kuweka tego Mufindi wiki ijayo. Akipona ndagu zake kali!
 
Unapotoa lifti kwa baadhi ya watu tegemea mambo haya,

- Wizi/ukwapuaji - si ajabu umempakiza mkaka mtanashati au mdada mlimbwende lakini anaposhuka akaondoka na kitu chako hasa hivi vitu vya thamani mfano laptop. Umefika unakoenda unachungulia kitu chako ukawajibike unakuta holaah hamna kitu! kumbe yule mwamba au mlimbwende uliyempa lifti alishashuka nacho.

- Uharibifu - unaweza kukuta hapo kabla milango ya gari ilikuwa inafunga vizuri tu lakn baada ya kutoa lifti au kuazimisha chombo, milango haifungi au haifunguki kama mwanzo. mwingine unakuta amejining'iniza kwenye ile support hanger ya juu [pale unapoweka suti zako] hadi ameivunja hadi unashangaa sasa huyu alikuwa anabembea hapo juu au alikuwa anafanya nini hadi kavunja?

- Harufu - mwingine upo naye mnapiga stori kumbe mwenzio katoka zake huko bila kuoga au ana fangasi zake zinatema vibaya mno unajaribu kuongeza kiyoyozi unakuta hakifui dafu unaamua kuacha wazi madirisha labda hali itakaa sawa lakini wapi. hapo sasa unakuta huyo mhusika mwenyewe hana wasiwasi anakupigisheni stori tu utafikiri hakuna kinachokera humo ndani.

- Kubeba watu mishikaki - Unamsimama kumpa mtu lifti nayeye anaamua kumwita mwenzake au wenzake kadhaa ili waingie wote kwenye huo usafiri wako. mambo ya ajabu kabisa haya. yaani mimi nimekupa ofa ya usafiri wewe hlf nawew unaita washkaji zako wengine. daah!

- Kujipa u-DJ - wewe umepewa lifti tu lakn sasa umeshajigeuza umejifanya wewe sasa ndo DJ kwenye gari hata isiyo yako. unaweka mamiziki yako kwa sauti ya vipimo vyako bila hata kujali kama unakera wenzio.

- Kupakia mizigo - wewe umepewa hisani ya lifti lakini sasa bwana wewe au bi wewe umegeuza gari kama ya kwako kila unachokiona huko barabarani unataka kukinunua kiingie kwenye gari. haya sasa unataka kuchoma gari ya watu na magunia ya huko mkaa wako ulionunua huko mabarabarani.

Kwakweli kuna mambo yanafanywa na baadhi ya watu unaweza kuyaona ni madogomadogo lakini kiukweli yana maudhi yake.

Mtaongezea....
Shida yako una asili ya uchoyo na ulitaka tujue unamiliki gari
 
Sisi wengine tuna gari zenye ground clearance ndogo.. unasimama umpe lift mtu mmoja, yanakuja majitu manne zaidi, na hawaoni aibu kwamba wapo wengi kuliko ukubwa wa gari yatajiminya yaenee yote.

Kuna Mmoja nilimpa lift, siti ya mbele huw naweka sim yeye akafungua mlango bila kuangalia akaikalia, ikabid nimuulize hujahis kitu umekalia akasema hapana.. bado kdg nimwambie ningeweka kidole hapo ungekalia? Alinipa hasira sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wawili ofisini yaliwakuta haya. Wa kwanza aliwapa lift wanafunzi wa sekondari, wakashuka na laptop yake. Wa pili aliwapa lift watu tu barabarani. Akafika mahali akaingia dukani mara 1. Aliyekuwa kakaa 'siti' mbele akabeba simu ya aliyewapa lift. Kuna mmoja nilikuwa nampa lift, akishuka anabamiza mlango balaa hadi motor ya kupandisha/kushusha kioo ikapata changamoto. Sijui km milango ya gari yake huwa anaibamiza hivyohivyo baada ya kununua ndinga yake.
 
Huyu wa kubamiza mlango, huenda alikua hajui namna ya kufunga.
Msamehe.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom