Mambo yanayonikasirisha Kanisani

Mambo yanayonikasirisha Kanisani

Me kero yangu ni kuona mtu amefunga Safari kutoka kwao kwenda kanisani na nguo zinazobana makalio hatari, mwishowe kutufanya wanaume kutenda dhambi kwa kuwaza.

Wito wangu, kanisani watu wavae kwa heshima ikiwa ni ishara wamehudhuria sehemu takatifu.
Kuna tofauti gani na wakivaa hivyo mtaani?. Madhara ni yale yale tu.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Wasalaam wana JF,

Kesho jamii nzima ya kikristo au sisi wakatoliki tunaanza kwaresma siku 40 za kufunga na kufanya ibada nyingi.

Pamoja na zoezi hilo, naomba niorodheshe mambo yanayonikera kanisani kama yafuatayo:

1. Kwaya kuimba nyimbo ambazo waumini hawazijui. Yaani wanaimba wenyewe tu mavitu ambayo hatuelewi na hatushiriki;

2. Wingi wa matangazo, makanisa yanakua kama platforms za matangazo, yanapoteza muda na kurefusha ibada;

3. Urefu wa mahubiri, mapadre wanaongea sana, waongee kwa kiasi ujumbe utafika tu;

4. Sadaka za kushtukiza, watu wapewe taarifa mapema watatoa tu; na

5. Kushindwa kufuata ratiba za ibada. Hii ni mikoani zaidi, unakaa zaidi ya nusu saa ibada haijatoka tofauti na ilivyoandikwa kwenye time table.

Nawatakia kwaresma njema.
Mkuu kuchelewa nusu saa ibadani unaona ni nyingi hebu jumapili ya wiki hii ukasali kanisa lolote la kilokole lilipo karibu yako then utuletee mrejesho hapa jukwaani
 
Nop, kuna kitu inaitwa Mtaguso, taratibu huwa zinabadirika baadhi, usiooohudhuria misa kwa muda mrefu utakereka tu na mabadliko hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu ni mimi kabisa 🤣 leo sipati picha nitakavyokuwa mgeni huko RC, maana kwa karibia mwaka mzima wa 2021+22 Nilikuwa mbali sana na kanisa la katoliki, ikabidi niwe nasali KKKT 😁
 
Naunga mkono 100%. Mfano Kwaya nyingi zina kigagasi (egocentrism) mara nyingi huwa wanaambiwa na kuonywa waimbe zile nyimbo zinazofahamika na wengi na kama ni lazima basi wimbo mpya uwe ni 1 au 2 tu na wimbo huo urudiwe-rudiwe mara nyingi kadri iwezekanavyo ili na waumini wengine waujue. Lakini wapi!! hawaambiliki.... Wata-surf kwenye Swahili music notes na kukusanya nyimbo mpya huko na kuziimba bila kujali kwamba wao wanachangia tu kukoleza Ibada ili washiriki waweze kushiriki kikamilifu(Active participation) na kwamba pale sio mahali/jukwaa la maonesho au mbwembwe. Aidha nyimbo nyingine haziko kama ni sala na hivyo zinapigwa marufuku.
Tunaingia kwenye kwaresma, nyimbo ni zile zile hazibadilikagi…
Natumaini hii active participation itakuwa kwa kiwango cha 100%
 
Huku unalalamika misa inachukua muda mrefu at the same time unataka upate nafasi ya kuuliza. Hivi wakiruhusu maswali Misa utachukua masaa mangapi
Kwan unaona mm kuna sehemu nimelalamika juu ya mda?
Mm mda sio kero kwangu
 
Wasalaam wana JF,

Kesho jamii nzima ya kikristo au sisi wakatoliki tunaanza kwaresma siku 40 za kufunga na kufanya ibada nyingi.

Pamoja na zoezi hilo, naomba niorodheshe mambo yanayonikera kanisani kama yafuatayo:

1. Kwaya kuimba nyimbo ambazo waumini hawazijui. Yaani wanaimba wenyewe tu mavitu ambayo hatuelewi na hatushiriki;

2. Wingi wa matangazo, makanisa yanakua kama platforms za matangazo, yanapoteza muda na kurefusha ibada;

3. Urefu wa mahubiri, mapadre wanaongea sana, waongee kwa kiasi ujumbe utafika tu;

4. Sadaka za kushtukiza, watu wapewe taarifa mapema watatoa tu; na

5. Kushindwa kufuata ratiba za ibada. Hii ni mikoani zaidi, unakaa zaidi ya nusu saa ibada haijatoka tofauti na ilivyoandikwa kwenye time table.

Nawatakia kwaresma njema.
6. Kufanya mnada wakati wa ibada (hii kwa makanisa yetu haya)
 
Hasa hapo kwenye kwaya, Wanaimba nyimbo zilizotungwa kisasa, ukutane mpiga kinanda anatacheza kinanda makelele yaani unapoteza utulivu kabisa.

Baraza la walei wapige marufuku kwaya zinazoimba nyimbo zisizokuwepo kwenye liturujia.maana wanakwaya wengine wanafikiri pale ni jukwaa la kuonyesha mbwe mbwe zao.

Waimbe nyinmbo za rohoni ambazo kila muumini anaweza kuimba zile zina uburudisha moyo na utukufu unakujieni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni mimi kabisa 🤣 leo sipati picha nitakavyokuwa mgeni huko RC, maana kwa karibia mwaka mzima wa 2021+22 Nilikuwa mbali sana na kanisa la katoliki, ikabidi niwe nasali KKKT 😁
Usiogope. Jipe moyo! tuko wengi wa aina yako na bado watakuwepo. Kanisa katoliki....🤣🤣
 
Hasa hapo kwenye kwaya, Wanaimba nyimbo zilizotungwa kisasa, ukutane mpiga kinanda anatacheza kinanda makelele yaani unapoteza utulivu kabisa.

Baraza la walei wapige marufuku kwaya zinazoimba nyimbo zisizokuwepo kwenye liturujia.maana wanakwaya wengine wanafikiri pale ni jukwaa la kuonyesha mbwe mbwe zao. Waimbe nyinmbo za rohoni ambazo kila muumini anaweza kuimba zile zina uburudisha moyo na utukufu unakujieni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Bro. Sijui hilo linawashinda vp. Kamani mbwembwe si wangoje siku za harusi? Aidha Paroko/Padri, Baraza (Kamati tendaji)/kamati ya Liturjia ni kama wanaunga mkono jambo hilo kwa ukimya wao. Kwaya (Wengi ni vijana) hawajakulia malezi ya Sala -hata ile kauli isemayo Kuimba ni kusali mara mbili hawakumbushwi au hawaikumbuki au wanaipuuzia.
 
Back
Top Bottom