Mambo yanayopaswa/yasiyopaswa kufanya kati ya umri wa miaka 15 na 25

Mambo yanayopaswa/yasiyopaswa kufanya kati ya umri wa miaka 15 na 25

NICOLAX

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2014
Posts
250
Reaction score
138
Habarini maGT wa hapa jukwaani,

Leo nimeona niombe msaada wa mawazo kwa watu waliopevuka kiakili.

Ni muda mrefu sasa nimekua nikisikia kua ujana hivi mara ujana vile mara ujana maji ya chumri, kuna wadau wamekua wakizungumzia mambo yanayopaswa kufanywa au yasiyopaswa kufanywa kati ya umri wa miaka 15 na 25, mimi kama kijana ambaye umri wangu una range hapo kati natambua uwepo wa wadau wa rika zote hapa JF.

Hivyo basi kwa niaba ya vijana wote ningependa kuleta maada ambayo nina uhakika itatubadilisha sana sisi kama vijana kama tutafuata mashauri, mawazo, mawaidha, maonyo, na kila changizo ambalo litatolewa na maGT wa hapa jukwaani

Natanguliza shukrani

.made in mby city.
 
kama unasoma: soma sana
kama unakazi kujiajiri : fanya kwa juhudi sana
achana na magenge ya ajabu ajabu.mana yatakupeleka kubaya ,ucje juta ukifikia uzeee kama ukifanikiwa kuwepo
 
Jijengee uwezo wa kuweza kujitegemea kuanzia kiakili
 
Mtegemee MUNGU sana maana usipomtegemea Mungu utakuwa mtumwa wa shetani
 
kama unasoma: soma sana
kama unakazi kujiajiri : fanya kwa juhudi sana
achana na magenge ya ajabu ajabu.mana yatakupeleka kubaya ,ucje juta ukifikia uzeee kama ukifanikiwa kuwepo

Umenena vyema mkuu
shukrani

.made in mby city.
 
NICOLAX , naomba nichangie kidogo kwenye mada yako hii kwa style ya kulinganisha.

Kizazi cha vijana waliozaliwa miaka ya kati ya 70s 80s mpaka kati ya 1990s katika dunia nzima wamekuwa na common culture. Baadhi ya vijana katika group hili hawana furaha. Hii imeonekana kwa tafiti zenye kulinganisha vijana waliozaliwa katika miaka ya nyuma zaidi na ujana wao ulikuwaje. Kwa kutokuwa na furaha basi mbinu tofauti zimetumika kujaribu kuleta furaha ya kujitengenezea (artificial happiness) baadhi ya mbinu zikiwa hatari sana kwa mwili, akili na mahusiano kwa jamii nzima.

Furaha ni matokeo ya Uhalisia kutoa Mategemeo au unaweza kuweka katika hisabati;

Furaha = Uhalisia wa mambo – Mategemeo yako.

Ni wazi kwamba Mategemeo yako yakiwa zaidi ya Uhalisia wa mambo basi utakuwa na furaha sana na kama Mategemeo yako yasipofikia uhalisia wa mambo basi hautakuwa na furaha.

Watu waliozaliwa kabla ya miaka hiyo niliotaja labda tuseme wazazi wa hawa vijana "wengi" mategemeo yao yamevuka uhalisia na ujana wao ulikwa na furaha. Sehemu nyingi za ulimwengu mambo hayakuwa kama yalivyo sasa. Miaka ya 70s, 80s ,90s dunia iliingia katika kipindi cha ukuaji wa chumi na technolojia. Watu wakasoma na kukuta kazi zipo tu moja kwa moja kutoka shuleni. Wale ambao hawakusoma wakakutana na viwanda vingi tu unafundishwa kazi taratibu unaendelea. Hawakutegemea haya kwa kuwa utoto wao ulikuwa hauna matarajio haya. Kwa hiyo kipindi hiki kwa duniani ujumla kinajulikana kama kipindi cha neema ya uchumi. Uhalisia wa kipindi hiki ni mzuri zaidi ya mategemeo ya vijana wale wa kabla ya 70s.

Sasa waliozaliwa kuanzia katikati ya 70s mpaka 90s hawa wamezaliwa katika kipindi cha neema ya uchumi na matarajio yao yamekuwa makubwa kuliko uhalisia wa mambo. Vijana wana matarajio makubwa tu asome apate kazi kubwa sana awe na mali nyingi lakini uhalisia kazi hizi nyingi kwa kila kijana hazipo. Biashara pia si rahisi kama jinsi ilivyotarajiwa. Infact uhalisia ni hauendani na matarajio hivyo kunakuwa hamna furaha.

Kwa hiyo utatuzi hapa ni kujiangalia vizuri jinsi gani furaha itapatikana. Matarajio yaendane na uhalisia au yasizidi uhalisia wa mambo. Kazi ni kazi na bidii ndio inaleta matokeo tofauti. Kudhani kwamba utakuwa na hali nzuri by default ni kuwa na expectations nje ya uhalisia. Na vijana wengi wanadhani wao ni special kwamba ni zaidi ya kawaida sasa hii inaondoa ile bidii binafsi ambayo ndiyo hasa siri ya furaha. Hawatafuti bali wanasubiri kuonwa jinsi walivyo na kipaji.

Ushauri wangu kwa kijana.

  1. Stay ambitious
  2. Acha kudhani wewe ni special.
  3. Achana na maneno ya watu ya kukatisha tamaa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu MONSTGALA/MGALANJUKA nimefarijika kukuona hapa jukwaani,
Sasa mkuu matarajio yangu yawe chini ya uhalisia au niwe na matarajio pande nyingi ambazo zitakua sawa na uhalisia(multipurpose)??

.made in mby city.
 
Kuwa makini sana na chama cha ccm, husikubali kuwa mtumwa wa siasa,
 
Miaka 15 mpaka 25 wengi bado KKB wachache sana wanajitegemea!!

Shukrani mkuu kwa mchango wako
Naomba nikuulize kaswali kadogo hapa
muda sahihi wa kuanza kujitegemea ni upi hasa(umri gani)?

.made in mby city.
 
Mkuu MONSTGALA/MGALANJUKA nimefarijika kukuona hapa jukwaani,
Sasa mkuu matarajio yangu yawe chini ya uhalisia au niwe na matarajio pande nyingi ambazo zitakua sawa na uhalisia(multipurpose)??

.made in mby city.

I could break down my last 3 tips as below:

Moja, Ulimwengu wa sasa unafunguka na opportunities nyingi kwa mtu kijana ambaye ni ambitious hakika utajizawadia mafanikio. Specific direction haiko clear, lakini panaendeka na unaweza kwenda. Mbili, Lakini kudhani kwamba wewe kama kijana ni special mmmh! Hiyo ni wrong unless you are really special. Ukijiona kama mtu wa kawaida ambaye anahitaji experience na bado hana cha kujivunia bado then unaweza kuwa "special" baadae na ni baada ya kufanya kazi au malengo yako kwa muda wa kutosha.

Tatu, Usisikilize au kudhani wengine wanafanya vizuri bila ya kutoka jasho hapana! Hata wenye biashara haramu wanasota sana na wana risk kubwa zaidi hivyo hamna mtu hatoki jasho kama yupo basi kuna wanaotoka jasho kwa niaba yake. If you just do your thing, you'll never have any reason to envy others.
 
Shukrani mkuu
Monstgala ivi kufikia ndoto zangu ninahitaji vitu gani hasa vya kunipush niende where i wanna be

.made in mby city.
 
Back
Top Bottom