Mambo yanayopaswa/yasiyopaswa kufanya kati ya umri wa miaka 15 na 25

Mambo yanayopaswa/yasiyopaswa kufanya kati ya umri wa miaka 15 na 25

Shukrani mkuu
Monstgala ivi kufikia ndoto zangu ninahitaji vitu gani hasa vya kunipush niende where i wanna be

.made in mby city.

Mkuu, hakuna siri zaidi ya discipline. Utaona vigezo vyote vya mafanikio nguzo yake ni discipline katika kile unachokifanya. Nadhani hata njia fulani zenye kuonesha kukubalika na wengi zimejengwa juu ya discipline ya hali ya juu ambayo inakufanya ushughilike na uheshimu mambo fulani. Hakuna formula halisi ila discipline. Bahati inaweza kuibuka lakini bahati si mbinu.
 
Monstgala nikiwa kama kijana wa chuo/shule, nna malengo mengi sana..naona umegusia discline je discipline pekee ni kigezo cha kufanikiwa? kama nlivyosema nna malengo mengi tena makubwa je nini nianze kufanya ili nifikie malengo yangu hasa kwa kipindi hiki ambacho niko chuo/shule?
 
Last edited by a moderator:
Monstgala nikiwa kama kijana wa chuo/shule, nna malengo mengi sana..naona umegusia discline je discipline pekee ni kigezo cha kufanikiwa? kama nlivyosema nna malengo mengi tena makubwa je nini nianze kufanya ili nifikie malengo yangu hasa kwa kipindi hiki ambacho niko chuo/shule?
LORDVILLE Unasema una malengo mengi sana, Je huoni haja ya kuchambua malengo mengi ili uwe na malengo yale relevant alafu katika hayo uweke bidii na discipline katika kuyafikia? Malengo mengi sana ni ishara ya kwamba huna malengo yenye nguvu. Akija mtu akasema ana malengo sabini na mwingine akasema ana malengo matatu basi yule mwenye matatu inawezekana yuko focused zaidi na anajua afanye nini na yule mwenye sabini labda bado hajui afanye nini.

Ukiwa shule unaweza kupanga malengo yako unayafikiaje na hatua zake alafu ukaweka discipline katika zile hatua. Shuleni unaweza kulenga elimu itakayokusaidia katika malengo yako na ukahakikisha katika hiyo unapata grades nzuri za juu sana zinazoendana na malengo yako. No excuses katika hatua hizo ni bora uumie na kupata shida lakini malengo ya muda huo yanafikiwa. Baada ya hapo unaweza kwenda step ya pili, tatu na mwisho utaweza ukafanya tathmini kama unaenda sawa. Alternatives ni part ya malengo hivyo inatakiwa iwepo lakini isiwe kinyume kabisa na malengo yako.

Hakuna ushauri wa moja kwa moja maana situations ni tofauti lakini kama unanisoma vizuri unaweza kujenga solution kwenye situation yako.

Cheers.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom