Mambo yanayotupunguzia umri wa kuishi

Mambo yanayotupunguzia umri wa kuishi

Goodrich

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
2,091
Reaction score
1,178
Kimsingi sababu kubwa inayotupunguzia umri wa kuishi na kututengenezea magonjwa sugu ni tabia yetu ya kuthamini vitu vilivyotengenezwa na wanadamu badala ya vile tulivyowekewa na Muumba wetu.

Mtu yupo tayari kununua juisi ya TShs 3500 badala ya embe la 500.

Mtu yupo tayari kutumia daladala mwendo wa hatua chache badala ya miguu yake.

Mtu yupo tayari kuweka mabati ili apate kivuli badala kupanda miti nk.

Tumeendekeza;

1. Matumizi ya bidhaa za viwandani eg mafuta ya kupikia, dawa za meno, soda, juisi, vipodozi, perfume etc (Tumeacha vitu vya asili tulivyowekewa na Muumba wetu)

2. Hatufanyi mazoezi (Miili yetu iliumbwa kufanya kazi/physical kwa kiwango fulani)

3. Mawazo na/au kukata tamaa (Hii husababishwa na changamoto za Dunia ya sasa ikiwamo kumiliki vitu, kudhulumiwa haki nk)

4. Hewa ukaa kutoka kwenye magari, viwanda nk

5. Kukosa mazingira tulivu ya kuishi, yenye hewa ya kutosha.

Ukiangalia afya za watu wanaoishi vijijini utagundua ni bora na imara kuliko wale wanaoishi mijini.

Ni vema kubadili lifestyle
 
Acha kwanza tumalizane na huyu aliyehamisha mpaka. 'Amelaaniwa mtu ahimishaye mpaka na jirani yake kwa lengo la kujiongezea ukubwa wa eneo lake' tafadhali mwenye kujua hii verse naomba airushe.
 
Acha kwanza tumalizane na huyu aliyehamisha mpaka. 'Amelaaniwa mtu ahimishaye mpaka na jirani yake kwa lengo la kujiongezea ukubwa wa eneo lake' tafadhali mwenye kujua hii verse naomba airushe.

N kweli ni JFK WA BONGO unawaza kibongobongo, si yule wa asili.
 
uko sahihi sana mtoa mada na kuna mengi ambayo hujayaorodhesha hapo lakini nayo ni chanzo cha matatizo yanayotukumba kwa mfano

1. Mwanaume kuacha mke wake na kwenda KUZINI nje ya ndoa
2. Mwanamke kuacha mumewe na kwenda KUCHEPUKA nje ya mahusiano

3. Uvivu wa kujifunza kupitia usomaji na kuishia kupata madhara ambayo tungeyaepuka kwa kusoma
4. Kupanda pikipiki mtindo wa mshikaki
5. Kunywa pombe kupita kiasi
 
Sawa mkuu, ila wazo kuu la mleta mada lilikuwa ni ile tabia ya kuacha kutumia tulivyopewa na Mungu na kuendekeza vinavyotengenezwa na binadamu, eg, kutumia magari na pikipiki kwa safari fupi badala ya miguu, kuacha mke/mume uliyepewa na Mungu na kuchepuka, kunywa bia, gongo, dadi nk badala ya maji etc.Anyway,wewe mtoa post umeweka kina kizuri kwenye thread.
 
Mambo mengine yanayopunguza umri wa kuishi ni kumchukia Lowassa tu
 
uko sahihi sana mtoa mada na kuna mengi ambayo hujayaorodhesha hapo lakini nayo ni chanzo cha matatizo yanayotukumba kwa mfano

1. Mwanaume kuacha mke wake na kwenda KUZINI nje ya ndoa
2. Mwanamke kuacha mumewe na kwenda KUCHEPUKA nje ya mahusiano

3. Uvivu wa kujifunza kupitia usomaji na kuishia kupata madhara ambayo tungeyaepuka kwa kusoma
4. Kupanda pikipiki mtindo wa mshikaki
5. Kunywa pombe kupita kiasi
Mleta thread umenena kweli tupu! Nilimtembelea rafiki yangu msomi mmoja mzuri sana anayeishi Dar.Nakumbuka ilikuwa ni msimu wa matunda mengi sana maembe na machungwa kwawingi.Ile nimekaa kwenye kochi sebuleni namwona anafungua friji na kuniuliza, "bro, nikupe juisi gani? Kuna ya embe, mapera nk"
Alipotaja embe nikakumbuka maembe dodo mengi niliyoyaona Mombo nikiwa njiani kuja Dar.

Nikamwambia nipe ya embe. Mara akatoa paketi na kunipa akisema,"hizi juisi safi sana!"
Akaleta glasi nikainywa lakini sikuwa na raha kwa sababu nilikuwa nakunywa juisi ya kiwandani iliyotengenezwa
na kuhifadhiwa kwa madawa kemkem yanayodhuru miili yetu.

Pamoja na usomi wake aliona juisi ya kiwandani ni bora kuliko kununua tunda na kutengeneza juisi! Hii ni tabia ya watu wengi waishio kwenye miji mikubwa hapa tz.
 
Hata ukigonga sana-kale ka mchezo tupendao sote ...basi nasikia nako kanafupisha umri wa kuishi.!
 
Unamaanisha miswaki tuwe tunatumia ile ya miti? duh! hatariiiii
 
Back
Top Bottom