Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara - Tanganyika Law Society(TLS) iliandaa Warsha kwa Wanahabari Jijini Dodoma Tarehe 4 Juni 2024 kuhusu Uhuru wa kujieleza. Hapa chini ni andiko la Mwanahabari Mkongwe mbaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Mabaraza ya Habari Afrika Mashariki (East Africa Press Councils - EAPC), Kajubi D. Mukajanga alilolitoa kwa Wanahabari hao kuhusu Uhuru wa kujieleza.
Mikataba mbalimbali ya Kimataifa inalinda haki ya kujieleza
Mikataba hiyo ni pamoja na; Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UNDHR) la Mwaka 1948 Ibara ya 19, Agano la Kimataifa Kuhusu Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) lililopitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) 16 Desemba 1966. Tanzania ilitia saini (ratify) ICCPR mwaka 1976.
Declaration of Principles of Freedom of Expression in Africa – Azimio la Kanuni za Uhuru wa Kujieleza Afrika lililopitishwa na Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) mwaka 2002;
African Charter of Human and Peoples’ Rights iliyopitishwa 1982.
Uhuru wa kujieleza unatambulika kama haki ya binadamu ambayo ni msingi na nguzo ya uwezeshaji wa haki nyingine na iko katika katiba za nchi mbalimbali Afrika na Duniani.
Hapa Tanzania haki ya kujieleza imo katika katiba za JMT, 1977 ya Ibara ya 18 ya katiba ya Zanzibar, 1984 Ibara ya 18 pia.
Hata hivyo, serikali mbali mbali duniani zimekuwa hazizingatii matakwa ya mikataba na maagano ya kimataifa kikamilifu.
Wakati mwingine matakwa haya huzingatiwa kwa baadhi ya watu tu – double standards; k.m. watu wenye asili fulani katika mataifa yenye ubaguzi wa rangi, watu wa daraja la juu, n.k.
Kuna mazingira ambayo uhuru wa kujieleza huminywa kihalali na mazingira hayo yamefafanuliwa kimataifa katika Ibara ya 19 ya ICCPR, na Ibara ya 30 ya Katiba ya JMT hapa nchini.
Uminyaji mwingine nje ya maelekezo ya ICCPR au hata Katiba ya JMT sio halali. Mambo na mazingira yaliyo nje ya maelekezo hayo ni pamoja na haya yafuatayo:
Leseni au rukhsa maalum kwa wanahabari
Sharti hili, ambalo hutolewa kwa kisingizio cha kuhakikisha wanaoandika habari wana “uwezo stahiki”, linaweza kutumika vibaya kuwanyima baadhi ya watu haki ya kujieleza, kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kibiashara, kisiasa, kibinafsi, n.k. Hivyo linakiuka haki ya msingi ya kujieleza na hivyo kutokidhi vigezo vya sheria nzuri.
Baadhi ya mamlaka zilizoainisha hivyo ni Inter-American Court of Human Rights mnamo 1985 katika ushauri uliotolewa na mahakama hiyo kwa Costa Rica; Mahakama Kuu ya Zambia mwaka 1997 katika shauri la Kasoma v. Attorney General; na tamko la pamoja la UN Special Rapporteur on Freedom of Opinion and Expression, OSCE (Organisation for Security and Co-operation in Europe) Representative on Freedom of the Media na OAS Special Rapporteur on Freedom of Expression mwaka 2004.
Kashfa kufanywa jinai
Viwango vya sheria vya kimataifa havitambui kashfa kuwa kosa la jinai, bali la madai. Kuifanya kashfa kuwa jinai husababisha woga kwa watu kutoa maoni yao wazi wazi, hasa kuhusu viongozi na hata katika masuala ya tuhuma za ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Pia huathiri utendaji wa kazi ya uandishi kwa kuwatia hofu wanahabari (libel chill), lakini pia kunakiuka kanuni ya ulinganifu wa kosa na adhabu (proportionality test).
Kuwalinda viongozi na watumishi wa umma dhidi ya ukosoaji
Mahakama ya Afrika iliamua katika kesi ya Media Rights Agenda and Others vs. Nigeria – 2000 kuwa watu wanaochukua nafasi za uongozi zenye maslahi makubwa kwa umma hawawezi kuepuka ukosoaji na kufuatiliwa kama ilivyo kwa raia wa kawaida, vinginevyo hata mijadala yenye maslahi kwa umma itauwawa katika jamii. Hii ina maana sheria haipashwi kuweka ulinzi maalum kwa watu hawa.
Utaratibu wa vibali kwa wanahabari
Haki ya kujieleza inajumuisha haki ya kutafuta na kupokea taarifa na maoni. Serikali kwa kawaida huzuia waandishi na watu wengine kuingia katika baadhi ya maeneo ambayo ni nyeti, kama vile ya kijeshi. Hii ni sahihi mradi vigezo vimezingatiwa.
Wakati mwingine, kwa sababu ya ufinyu wa nafasi, mamlaka hutoa vibali vya kuingia ili kuepusha msongamano. Tume ya Kimataifa ya Haki za Binadamu imeeleza kuwa ili kupata uhalali, utoaji wa vibali shurti usifanywe kisiasa (Gauthier v. Canada, 7 April 1999).
Utaratibu wa vibali kwa wanahabari
Mamlaka nyingine zikiwamo Umoja wa Mataifa, OSCE (Organisation for Security and Cooperation in Europe) na OAS (Organisation of American States) zimesisitiza msimamo huu na kusema utaratibu wa vibali kwa wanahabari unafaa tu pale ambapo unawawezesha kuingia mahala au kuhudhuria matukio fulani (privileged access to certain places and/or events) na lazima usimamiwe na mamlaka huru na uwe wa haki na uwazi huku vigezo vikijulikana mapema. Kwa hiyo utaratibu wa vibali uwawezeshe waandishi badala ya kuminya uhuru wao.
Kukosekana ulinzi wa vyanzo vya habari
Kuna wakati ambapo vyanzo vya habari huhitaji kulindwa kwa kutotajwa. Hii hutokea pale vinapotoa taarifa nyeti zinazoweza kuhatarisha usalama au kazi zao, mathalan, taarifa dhidi ya magenge ya kihalifu, au za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Ulinzi wa vyanzo umesisitizwa na mahakama na mamlaka mbalimbali duniani zilizosema amri ya kutaja vyanzo itolewe tu katika mazingira maalum na sio kiholela. Hii ni kwa kutambua kwamba ulinzi wa vyanzo ni ulinzi wa haki ya kujieleza na haki ya kupata habari, kwani vyanzo visipolindwa kuna hatari ya kutopata taarifa muhimu kwa maslahi ya umma.
Mashambulio dhidi ya watendaji wa vyombo vya habari
Mashambulio dhidi ya watendaji wa vyombo vya habari ili kuwanyamazisha ni jambo lisilokubalika. Serikali zinazonyamazia au hata kushajiisha mashambulizi haya zinavunja si haki ya kujieleza tu, bali hata haki ya uhuru na hata haki ya kuishi.
Azimio la Tume ya Afrika la Misingi ya Haki ya Kujieleza linatamka bayana wajibu wa serkali kuwalinda wanahabari na vyombo vyao dhidi ya mauaji, utekaji, unyanyasaji, uharibifu wa vifaa vya kazi, n.k.
Sheria mbaya za makosa ya mtandaoni, ugaidi, usalama
Serikali nyingi zimekuwa zikitumia sheria za makosa ya mtandaoni kunyima watu uhuru wa kujieleza. Mara nyingi sheria hizi hazifuati viwango vinavyokubalika kimataifa.
Sheria nyingine ambazo zimekuwa zikitumika ni sheria za kuzuia ugaidi. Uhuru wa kujieleza umekuwa pia ukiminywa kupitia sheria za usalama wa taifa.
Vita
Mazingira ya vita yanajulikana duniani kote kuwa huwa sio rafiki kwa habari za kweli. Kuna msemo kuwa majeruhi wa kwanza wa vita huwa ni UKWELI.
Wakati wa vita dola huweka udhibiti mkubwa wa kujieleza kuhusiana na mwenendo wa vita. Dola pia hudhibiti habari zinazotolewa. Lengo huwa ni kulinda morali wa wapiganaji, lakini pia hamasa ya wananchi na kupunguza uwezekano wa adui kupata taarifa zinazohusu upande wenu.
Msaada
Kuna taasisi kadhaa ambazo zinaweza kumsaidia mtu ambaye haki yake ya kujieleza imevunjwa. Ni vizuri kuwasiliana nazo na kuona zinaweza kutoa msaada gani ikiwa umepatwa na kadhia hiyo. Baadhi ta asasi hizo ni:
Tanganyika Law Society (TLS) : Hawa wana jukumu la kuishauri serikali na Bunge kuhusu maswala ya kisheria.
Kituo cha Msaada wa Kisheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Msaada
Nyingine ni pamoja na:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)
Baraza la Habari Tanzania (MCT) hususan kwa wanahabari
Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) – kwa wanahabari
Tanzania Network of Legal Aid Providers
Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA)
Nyingine ni:
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG)
WILDAF, na Registrar of Legal Aid Providers, Ministry of Constitution and Legal Affairs.