Mambo yanayozuia mafanikio yako

Hao ni tatizo hata kabla hawajaathilika, na kama kuna kijana mpaka sasa hajajua nini atafanya iwapo atapata maambukizi na namna ya kuishi nayo basi hajajitambua pia na hajua kama anazungukwa na asilimia kubwa ya wanaoishi na virusi hivyo na maisha yanasonga kama kawa. Tukirudi kwenye point yako ya msingi, kama huna maambukizi jiepushe nayo, kama una maambukizi fuata njia za kuongeza muda wa kuishi na ukipambana kuibadili dunia. Vijana tuamke, tubadilike kifikra, kila ndoto yako ya mafanikio inawezekana kabisa.
 
Mkuu nimefurahi sana kwa mchango wako unamtazamo sawa na wangu ndio maana tunatoa ushauri nasaha (counseling) baada ya kupima maambukizi
 
Mtu yuko kijijini anaendesha bodaboda kwa siku anapata elf 6 au asipate unasema asitoke hapo alipo kwenda mjini anakoweza kupata elfu 20 au zaidi kwa siku, hii kali
Sijasema asitoke ndugu ila nimesema awe na imani kuwa hapo alipo haijalishi ni kijijini au mjini yupo mahali sahihi na sehemu ulipo ndipo fursa inapopatikana wangapi wanatoka vijijini na kuja mjini na maisha yakawashinda na kurudia kulekule?
 
Sijasema asitoke ndugu ila nimesema awe na imani kuwa hapo alipo haijalishi ni kijijini au mjini yupo mahali sahihi na sehemu ulipo ndipo fursa inapopatikana wangapi wanatoka vijijini na kuja mjini na maisha yakawashinda na kurudia kulekule?
Bado hujaeleweka, mtu yuko bongo mshahara laki8 unasema asitoke kwenda nchi za ulaya na Amerika ambako pengine 2mln ni kwa wiki
 
09. Kuwa na mtazamo hasi.
Siku zote kwenye maisha mtu mwenye mtazamo hasi hushindwa hata kwa jambo dogo. Hivyo badili mtazamo wako na uwe na mtazamo chanya kwenye malengo yako. Mtu mwenye mtazamo chanya huwa na msukumu (inspiration) wa hali ya juu kwenye kutimiza alichokusudia. Ili uwe na mtazamo chanya yakupasa uitulize akili yako na kutokuwa na shaka au wasiwasi wa aina yeyote ile. Kwakuwa sasa huna wasiwasi wa aina yeyote ile sasa unaweza kufikiri na kutimiza kile ulichokusudia. Weka kwenye ufahamu wako kuwa ukiwa na mtazamo chanya ni sawa na mtu mwenye taswira ya ubunifu ya kile ambacho unakihitaji. Usiogope kusema kile unachokitaka au kukitamani kwenye maisha yako vifanye viwe msukumo katika maisha yako ya kila siku. Mfano kwenye akili yako unatamani kuwa tajiri anza kuweka bayana kwa kusema "mimi ni tajiri" na "sio mimi nitakuwa tajiri". Mifano mingine ni I can get what I want (naweza kupata kile ninachokitaka), I am beautiful (mimi ni mzuri). Usishangae kuona wadada zetu wanajichubua au kutumia mda mwingi kwenye kioo uone ni halali hapana ni kwa sababu wanamitazamo hasi kwenye akili zao wanajiona wao ni wabaya ndio maana wanajichumbua hivyo siku zote ukiwa na mtazamo hasi utasita kufanya jambo na ndio kitu pekee kitakacho kufelisha kwenye maisha yako.
Itaendelea
 
Mkuu haturuhusu tabia ya kuweka link za kuwatoa watu JF na kuwapeleka kwenye blogu yako. Hili ni kosa kwa sheria za JF. Tafadhali usirudie.
 
Sawa mkuu nilikuwa sina uelewa na jambo hilo ila nataka kuuliza je nawezaje kufanya matangazo humu kwa kuwa mimi ni muandishi wa vitabu mbalimbali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…