09. Kuwa na mtazamo hasi.
Siku zote kwenye maisha mtu mwenye mtazamo hasi hushindwa hata kwa jambo dogo. Hivyo badili mtazamo wako na uwe na mtazamo chanya kwenye malengo yako. Mtu mwenye mtazamo chanya huwa na msukumu (inspiration) wa hali ya juu kwenye kutimiza alichokusudia. Ili uwe na mtazamo chanya yakupasa uitulize akili yako na kutokuwa na shaka au wasiwasi wa aina yeyote ile. Kwakuwa sasa huna wasiwasi wa aina yeyote ile sasa unaweza kufikiri na kutimiza kile ulichokusudia. Weka kwenye ufahamu wako kuwa ukiwa na mtazamo chanya ni sawa na mtu mwenye taswira ya ubunifu ya kile ambacho unakihitaji. Usiogope kusema kile unachokitaka au kukitamani kwenye maisha yako vifanye viwe msukumo katika maisha yako ya kila siku. Mfano kwenye akili yako unatamani kuwa tajiri anza kuweka bayana kwa kusema "mimi ni tajiri" na "sio mimi nitakuwa tajiri". Mifano mingine ni I can get what I want (naweza kupata kile ninachokitaka), I am beautiful (mimi ni mzuri). Usishangae kuona wadada zetu wanajichubua au kutumia mda mwingi kwenye kioo uone ni halali hapana ni kwa sababu wanamitazamo hasi kwenye akili zao wanajiona wao ni wabaya ndio maana wanajichumbua hivyo siku zote ukiwa na mtazamo hasi utasita kufanya jambo na ndio kitu pekee kitakacho kufelisha kwenye maisha yako.
Itaendelea unaweza kusoma pia...
Mambo yanayozuia mafanikio yako 03.