Don Gorgon
Member
- Nov 21, 2024
- 35
- 68
Jeshi letu la Polisi ni jeshi zuri sana na huenda likawa ni lenye weledi na utashi kuliko yote Afrika Mashariki na Kati. IGP Wambura ni IGP Bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii. Ana historia nzuri ya kushughulikia wahalifu na askari wakengeufu kila wanapojitokeza na ametengeneza Jeshi imara ambalo halisigani na wananchi. Ndiyo maana kila raia yupo huru katika kila kona za nchi hii. Hofu iliyokuwepo enzi na enzi haipo tena.
Hakuna mtu atatekwa au kunyanyaswa kwenye nchi hii kama kuna uwepo wa polisi maeneo hayo. Ni watetezi wetu tunaopaswa kuwakumbatia vema. Tunaona kila siku watu wanavyosafiri kwa amani toka maeneo mbalimbali na wanapata msaada wa polisi kila wanapouhitaji. Kwanini wasipate msaada wakati ni wananchi halali na watiifu kwa nchi yao?
Kesi zote kama za akina Mzee Ally Kibao, Deo Bonge, Soka, n.k zimeshafanyiwa uchunguzi wa kina na majibu ya uchunguzi tumepewa. Watuhumiwa wamechukuliwa hatua na kila Mtanzania anajua hilo. Jeshi lina uwazi sana. Hawakai kimya. Hata wale waliompiga Lissu risasi polisi wamefanikiwa kuwabaini na kama tunavyojua Watanzania wote, wameshahukumiwa vifungo vya maisha.
Hata hili la Abdul Nondo nalo linashughulikiwa kwa umakini kabisa. Jeshi lipo vizuri, tutarajie weledi wao. Wambura juu, juu zaidi!
Wapo washirikina fulani wanasema eti polisi wanakamata watu wakiwa hawajavaa sare za kazi. Jamani, wapi na lini umeona wakifanya hivyo? Hao ni wahuni tu wanaolenga kulisigina jina la jeshi letu. Kwa uzoefu wangu, hicho ni kitu hakiwezi kutokea. Polisi ni ndugu zetu, marafiki zetu na majirani zetu. Tunajua fika ni watu wema.
Jeshi hili huwezi kulifananisha na kitu chochote. Tukiwa barabarani na vyombo vya moto, hawa ni ndugu zetu na marafiki zetu wakubwa. Ni nadra sana kumbugudhi Mtanzania mwenzao. Rushwa kwao ni mwiko. Ukijichanganya ukataka kumhonga kwa utovu wako wa nidhamu, unaweza kuishia gerezani kihalali kabisa.
Kusema ukweli, nina miaka zaidi ya 53 kwenye nchi hii na sijawahi kushuhudia askari akipokea rushwa ya namna yoyote ile. Nimesikia baadhi ya watu wanafiki wakisema eti huko kwenye hiyo taasisi kumetamalaki rushwa. Rushwa ipi kama si unafiki tu? Peleka ushahidi uone kama huyo askari atabaki kazini. Acheni kuongelea vichochoroni.
Maneno ya kusema eti Jeshi la Polisi linaendeshwa kwa msukumo wa chama tawala ni porojo tu hizi. Wameshasingiziwa makamanda wengi kujihusisha na chama hiki. Hata Balozi Sirro ameshawahi kueleza kuwa hizi ni porojo tu. Kwanini tusiwaamini? Hatuoni hii amani jamani, mbona hatuna shukurani? Mnataka watupe huduma gani waungwana hawa?
Ushauri wangu ni kuwa, kama kuna cheo zaidi ya IGP kwenye jeshi hilo, basi Camillus Wambura akitunukiwe.
Kwa leo maua yangu ni hayo