Mambo yote Polisi huwa wanasingiziwa tu. IGP Wambura anapaswa kupongezwa kwa amani tunayoifurahia

Mkuu msome vizuri utaelewa zimetumika akili kubwa hapo.
Bado sana tutaongelea tukio dogo tu, kuna wale madogo walilipiga mawe treni la SGR wakapotelea makwao wale madogo siku ile ile walidakwa si ndio? Sasa hawa washenzi wanaoteka watu na ushahidi upo kwanini hawakamatwi? Hapo ndipo linapokuja suala kwamba wanaohusika na huo ushenzi ni wao wenyewe, nini kifanyike?

Sheria ya ukamataji watu washukiwa na watuhumiwa inabidi ifanyiwe marekebisho au maboresho kuanzia CPA, Penal Code mpaka PGO na polisi wanaotumia loophole zilizopo kwenye sheria zinazowapa wao fursa ya kukamata watu washukiwa/watuhumiwa na kuwatesa na kuwaweka kizuizini kinyume cha sheria waweze kushughulikiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mfano mwingine ni suala la Deo mpaka sura za watekaji wale zinafahamika na mpaka wengine wanafahamika majina yao kabisa hao polisi mpaka sasa wamechukua hatua gani na huyu mleta mada anakuja kuongea jambo gani hapa? Hakuna popote uliposikia kwamba wale waliofanya lile tukio wamechukuliwa hatua yoyote ya kisheria.

Hivi anataka tumuelewe kwa mawazo yake mgando suala la polisi linafahamika wazi sio suala la kusimuliwa, ukweli ya kua kuna polisi waovu na polisi wema hilo pia lipo wazi ila polisi walio wengi hawatendi haki hususani linapokuja suala la Chama A na upinzani polisi wanaegemea upande wa Chama A, polisi wote wanapokea order kutoka kwa Chama A hilo halina uongo wowote ndio maana watu wanafika hatua na kusema polisi wapo kwa ajili kukilinda Chama A na maslahi yake ya kiutawala.

Tuje kwenye mfano mwingine wale polisi waliohusika na mauaji wa George kule kwa kumpiga risasi 4 mpaka kupelekea kifo chake wamefikishwa wapi mpaka muda huu?

Hapo hakuna majibu yoyote yenye mashiko kwa kuzingatia hilo unagundua kwamba polisi wanafanya kazi yao sio kwa ajili ya Wananchi wote na sio kwa ajili ya kuwalinda Wananchi bali kwa ajili ya kuwalinda Chama A tu na watawala wa Chama A na ukionekana unaenda kinyume na Chama A basi polisi huchukua hatua ya kukuabgamiza kivyovyote maana yake ni kwamba polisi wameajiriwa na Chama A sio na Wananchi na hawapo kwa ajili ya ulinzi wa Wananchi bali ni kwa ajili ya kuwalinda Chama A

Mfano mwingine wapo wanachama wa Chama A wanaotamka vibaya dhidi ya wanachama wa Chama B kiasi cha kutishia uhai wao ila polisi hawawachukulii hatua yoyote ya kisheria ila wanaponyanyuka wanachama wa Chama B au C na kufanya vilevile wafanyavyo wanachama wa Chama A basi hapo polisi wananyanyuka na kuanza kuwateka na kuwatesa na kuwaua, sasa unaponyanyuka na kuja kusema polisi wanatenda haki sio kweli polisi hawatendi haki, tuzungumzie kuhusu wale wanachama wa Chama A waliotamka hadharani kwamba wakiwapoteza wanachama wa vyama vingine basi polisi wasiingilie hapo unagundua kabisa polisi wanapokea order kutoka kwa Chama A maana yake polisi ni chombo kilichopo chini ya Chama A na wanafanya kazi zao kwa amri kutoka Chama A polisi hutowakuta katu kamwe wakiwaita wanachama wa Chama A kwa matamshi yao.

Mfano kauli ya 'kifo ni kifo tu' hii kauli angeitamka mwanachama wa Chama kingine huyo mtu angetekwa angewekwa kizuizini na kupotezwa au ikiwezekana kuuawa kabisa huko huko asionekane popote ila kwa kua imetamkwa na mwanachama wa Chama A basi polisi wameishia kunywea na imekua km amri kwao kwamba wamepewa ruhusa ya kuua yoyote ambae hayupo Chama A na anakipinga Chama A kwa utendaji wake usio na haki kwa Wananchi wote wawe wa upande pinzani au wa Chama A

Mleta mada nenda umuulize Wambura kwanini matukio yote yanayoendelea anayakalia kimya km hayaoni na utendaji wa kisheria juu ya matukio hayo hayaonekani? Utakuta kwamba hata yeye hana majibu ya hayo maswali utakayo muuliza kwa hio hakuna haja ya kumkingia kifua sababu utendaji wake akiwa mkuu wa Jeshi la polisi ni chini ya kiwango kiufupi hio nafasi haimfahi

..............
 
Nilivyoona kichwa cha habari nilitaka nikurukie kama mwewe, baada ya kusoma kumbe unawakejeli hawa majambazi wanaovaa uniform.
 
Sawa mkuu. Ila mimi sijawahi kumilikiwa na chama kimawazo na hata kinyaraka - sina hata kadi. Hapa nalipa tu jeshi letu maua yake.
Sawa.gari lililombeba nondo lilikuwa linafanya Nini kituoni gogoni?
 
Jf ya sasa wachangiaji wengi vichwa havijiongezi. Yaani mleta uzi kawapeleka chaka wamejaa, angalia koment zao hawajamwelewa. Ingekuwa ile jf ya miaka ya 2014 kurudi nyuma koment nyingi zingekuwa ni kukazia hoja ama emoji za vicheko. Ndio hivyo tena kila zama na....
 
Mkuu umeua.
 
Kwenye ku control issue ya ujambazi wapewe maua yao hatusikii hbr za ujambazi mara kwa mara ila hii issue ya utekaji inawachafua sn waangalie namna ya kurekebisha hapo.
 
Nimegundua JF members wa siku hizi hawana thinking capacity kubwa.
Hawajamuelewa mtoa mada.
Mtoa mada anaongea the opposite
Nilidhani ni chawa lakini sio chawa
 

Attachments

  • Screenshot 2024-12-04 083841.png
    210.5 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…