Uchaguzi 2020 Mambosasa: Wagombea ubunge walioshindwa warudi majimboni mwao

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka wagombea ubunge kutoka mikoani walioshindwa katika uchaguzi, warudi majimboni mwao kwa sababu kitendo cha kukusanyika jijini humo ni uchokozi wa dhahiri kwa wakazi wa Jiji hilo.
 
Awaache! Wamekuja Dar kutafuta ajira.. Wakirudi majimboni watakufa njaa.. Pesa za ubunge wengi wamezitumia kwenye uchaguzi, anasa na miradi isiyo na tija.. Wengi akaunti ziko nyeupe.

Kama kuna ajira huko Polisi, Mambo sasa awaambie wapeleke CV.
 
Wame anza kuwapangia na sehemu za ku kaa
 
Hawaruhusiwi kukaa Dar? Hili kama tangazo la Makonda
 
Wanaruhusiwa ila sio kuandaa maandamano! Kura zipigwe Arusha na "ziibwe" Arusha alafu maandamano ufanyie Ubungu?
Umesima hilo katazo la Kulakula Mambosasa au unajibu tu sababu unadhani ni swali jepesi?
 
Haya ni maandamano yasiyokuwa na kikomo....leo ndio siku ya kwanza, aluta continua hadi Oktoba 2025. Anayedhani ataweza kuyazima maandamano haya anajichosha bure. Bora kuanzisha njia za kidiplomasia ili kupunguza makali ya maandamano siku za usoni.
 
Magufuli kaanza ukatili wake, kazi imeanza
Sasa watu wapangiwe wawe wanaishi wapi?? Au wawe wanakwenda wapi?
 
Nyie wenzetu ni wajinga sijawahi kuona. Hayo maandamano yapo wapi?
Haya ni maandamano yasiyokuwa na kikomo....leo ndio siku ya kwanza, aluta continua hadi Oktoba 2025. Anayedhani ataweza kuyazima maandamano haya anajichosha bure. Bora kuanzisha njia za kidiplomasia ili kupunguza makali ya maandamano siku za usoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…