Mamelod sundowns vs Yanga Afrika

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Ushawahi kulifikiria hili pambano? Uenda ndio itakuwa mechi bora kuwahi kuchezwa kwa karne hii hapa Afrika. Nilitamani sana wakutane kwenye super cup ila waarabu walitibua msimu jana.

Ndizo timu za kibantu zinazocheza mpira mziri barani Afrika kwa sasa. Wanafanana style za uchezaji. Wote wanamiliki mpira, wote wanashambulia kama nyuki pale wanapohitaji goli, wote wanakabia kwenye nusu ya mpinzani, kubwa zaidi wote wana stamina na pumzi ya kumpelekea moto mpinzani dakika 90 kwa kasi ile ile.

Toumbe hii miamba ikutane hatua za mbele kwenye CAF champions league. Mpira utakaopigwa hautasahaulika.
 
Mashabiki wa yanga tuache kulalamika na kutaka kufika mahali ambapo hatujapapambania... Kama tunataka kucheza na mamelodi tujitahidi Kila mwaka kufika angalau robo caf... Sasa miaka 25 hatujacheza caf hao mamelodi tutakutana nao wapi sasa???
 
Kwanza tumalizane na Al Ahly,tutaona huko mbeleni

Ila tukikutana itakuwa ni amsha popo
 
Siku ya mwananchi ijayo waalikwe
 
Hebu acha taarifa za comedy na wewe watu tuko serious bhna na umenichekesha kweli 🤣🤣🤣🤣😅😅
 
Hatua za mbele zipi hizo, we si umeshatoka hapohapo makundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…