Mamelodi ni Overrated, sijui ukubwa waliupataje

Kucheza ulaya kitu gani?

Mbona sasa hao South walimtoa Morocco ambayo ndiyo inaongoza kuwa na wachezaji wanaocheza ulaya kwanza wao wapo karibu na ulaya?

Walimpiga ahly ahly 5 halafu wakaenda wapi? Hata msimu ule waliomfunga tena 5 wakaja kutolewa wao na petro Luanda 🤣🤣

Hiyo team ni ya mchongo hype nyingi angalia kama ahly ahly wanavyofanya wale jamaa .

Wanacheza kulingana na stage sio hao matapeli kila msimu wanaishiaga hapa nusu ...

Hakuna kitu hapo licha ya uwekezaji wao mkubwa bado output zero ..

Na wataendelea kuishia hapa hapa ..
AFL ni bonanza lililochangamka tu pale ndiyo maana watu walifuata pesa tu

Kumbuka hawa unaosema bora walifunga mara ya mwisho mechi na mazembe makundi kule hadi sasa hawafungi mpaka wametolewa hata yanga nako wameshindwa kutufunga kweli na ahly ahly alimpiga 5?
 
Caf champions league wana mafanikio gani recently?

Hao kuongoza makundi ni kawaida yao tena huongoza kwa points nyingi sana kila msimu ila wakienda sana mwisho nusu fainali na ujue walimuokota kibonde robo fainali vinginevyo robo tu shughuli yao imeisha

Timu haijawahi kucheza fainali ya klabu bingwa toka mwaka 2016 unadhani ni kwa bahati mbaya.

Al Ahly na Wydad wamegawana vikombe kwenye fainali tano za mwisho yeye hajaweza kuchallenge hata mwaka mmoja zaidi ya kumkamia Al Ahly tu kwenye makundi akipangwa nae
 

AFL ni bonanza. Ni mashindano ambayo timu 8 tu zinashiriki kwa kualikwa.

Na hizo timu ni 8 tu huwa zinaalikwa tu hakuna qualification maalumu. Mashindano ya timu 8 tu . Hayafai kuwa kigezo cha kupima ubora wa timu.

Mashindano ya caf champions league yanashirikisha timu zaidi ya 50. Na hizo timu zinapatikana kwa kigezo xha kuwa bingwa kwenye ligi zao ama kuwa mshindi wa pili. Hivyo hata timu ndogo kama biashara utd ama Tanzania prison huwa zinashirikishwa kwenye kupatikana kwa washiriki wa caf champions league
 
Kabla haijawa overrated ujue ilikuwa highly rated (kuna jambo ilifanya)

Mamelody is overrated yes. Timu ya 1996 tayari ina kombe la CAF, tayari wana Semi’s kama tatu nne hivi halafu timu za kariakoo ambazo sizo overrated hiyo Nusu wanaililia hadi kwa barua.

Kwa Soka la Africa you can’t write them off.
Yes Mamelody hii sio ile ya Motsepe’
 

Sio al ahly na waydad tu hata huyu esperence kwenye fainali 5 za mwisho na yeye ametwaa kombe mwaka 2019 na 2020
 

Acha uongo mamelodi haijaanzishwa mwaka 1996. Mamelodi ipo tangu mwaka 1960s huko.

Weka ushahidi ku prove kama mamelodi ni timu ya mwaka 1996
 
Nashangaa sana eti ubora ubora gani sasa?

Wakati ndiyo huwa wanakwama hapa. Kila mara
Yaani hawa hata yanga angefunguka vizuri angewatoa kabisa yaani

Ahly ahly pekee ndiye team kubwa kwa malengo na mipango .
Hawa huwa wanaenda enda tu hawaeleweki

Eti kutoa wachezaji wale 7 South ndiyo imekuwa dili sana?
Simple sababu jamaa wameua sana soka Lao la ndani hivyo hakuna wachezaji team zingine ndogo imagine kina gadiel Michael na majogoro huko South ndiyo tegemeo eti ...

Hawa hawana tofauti na bayern Munich wanachukua ligi kuu kila mara ila UEFA wanaishia nusu au robo
 
Timu ya mchongo kinoma kila mwaka wanaipa hype unaweza kudhani ni mabingwa watetezi kumbe ni timu ya kuishia robo na nusu fainali kila mwaka
Hata huo mwaka walimpiga Al Ahly 5 kwenye group stage waliishia nusu fainal wenzao wakienda kubebs ndoo
Yaani timu toka 2016 mafanikio yake makubwa champions league ni kumfunga 5 Al Ahly.
Kuliko hao wapuuzi bora hata kumwamini Wydad au Esperance au hata Mazembe wanaweza kufanya kitu sio hao timu ya mchongo na wachezaji wa gharama kubwa wenye uwezo wa kawaida.
Na kama Wydad atazidi kuyumba kwenye soka la Afrika Al Ahly atatawala sana hao Wydad kidogo wakiwa kwenye ubora wao ndio huwa wanaweza kumpa challenge angalau kwenye 5 wakaokota 2
 
Wazuri kwenye kumiliki mpira ila sio wazuri kweny kucreate nafasi. Yanga basi tu mastriker walizingua ila walipata nafasi tatu za wazi za kumaliza mchezo. Esp hawajapata nafasi nyingi ila nafasi zao chache wamezitumia vizuri.
 
Umemaliza
Yaani wydad na Al ahly ndiyo wanapokelezana tangu muda tu

Hawa wasauzi uwekezaji mkubwa sana halafu output zero kabisa

Uwekezaji ule wanaoupata kama wangepewa hata simba na yanga wakasajiri vizuri hawa wajinga wasingetamba kabisa ..

Mimi naona wydad atarudi soon angalau yeye anaweza kumchalenge kidogo Al ahly

Huyo mamelodi ni msindikizaji
 
Wazuri kwenye kumiliki mpira ila sio wazuri kweny kucreate nafasi. Yanga basi tu mastriker walizingua ila walipata nafasi tatu za wazi za kumaliza mchezo. Esp hawajapata nafasi nyingi ila nafasi zao chache wamezitumia vizuri.
Mzize ana la kujifunza hapa
 


Kama vigezo vya timu kuwa bora ni hivyo mlivyovisema ninyi tu basi hata yanga hawastahili kujiita timu bora, kwa sababu hawajafanya na wala hawajafikia hata nusu ya waliyofanya na walipofikia mamelodi, sasa kama kwa vigezo hivyo mamelodi inaitwa mbovu je yanga itaitwaje hapo

Unajua mimi nilidhani labda kitendo cha yanga kujitahidi kutofungwa na mamelodi home and away, kunaonesha kuwa yanga imeadvance na kuwa timu kubwa kwa sababu imecheza na timu kubwa na haijafungwa, lakini badala yake mnadai eti mamelodi wabovu kisa wameshindwa kuwafunga yanga je hii inamaanisha nini

Yani hii maana yake ni kwamba yanga wenyewe hawajiamini wanajijua kwamba ni timu mbovu, na hawakutegemea kutoboa kwa mamelodi ndio maana walipotoboa, wakaona kwamba kumbe mamelodi ni wabovu kama wao tu na si kwamba wao ndio wameufikia ubora wa mamelodi
 

Katika hizo 5 za mwisho. Esperence na yeye aliokota ubingwa.

Esperence Sio mnyonge kwenye kutwaa mataji ya ligi ya mabingwa Africa
 
Yanga wamezuia wasifungwe na mamelodi sawa

Na mamelodi pia wamezuia wasifungwe na yanga pia
Tunaangalia takwimu za game nanj alipata nafasi nzuri?

Yanga wamezidiwa na mamelodi kwenye uwekezaji lakini uwanjanj hawakufunga goli moja hao wasauzi

Kama mamelodi ni bora sana mbona walishindwa kuifunga yanga mbovu?

Team bora hushinda match haijalishi ni ngumu vipi? Wao walishindwa ninj kuifunga yanga mbovu?

Al ahly aliifunga yanga moja wao walishindwa ninj kuifunga yanga mbovu?

Mpira wenu wa mdomoni na ujanja ujanja
 
Katika hizo 5 za mwisho. Esperence na yeye aliokota ubingwa.

Esperence Sio mnyonge kwenye kutwaa mataji ya ligi ya mabingwa Africa
Haya huyo wa mamelodi anayelazimisha ukubwa tunamuweka wapi jamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…