Mamelodi ni Overrated, sijui ukubwa waliupataje

Mamelodi mtoto mdogo sana .

Hata ENYIMBA tu hamfikii.. unaanzia wapi kumuweka level za wakubwa
Eti ni team tishio
Tishio la wapi sasa?
Ujue wabongo tunapenda sana kukuza vitu vya nje bila sababu

Ukiangalia huyo mamelodi kama ni makombe kaachwa hata na mazembe amebeba mara 5
 
Tunazungumzia Champios League michuano inayotoa bingwa wa Afrika anayekwenda kuwakilisha bara zima kwenye Fifa club world cup michuano inayomfanya Mamelod kila mwaka asotee robo fainali ama nusu kutokana na vigogo anaokutana nao tena wakiwa serious kuna kitu wanatafuta, sasa unakuja unazungumzia AFL michuano ambayo ukitoa hela ya mshindi hamna purpose wala heshima yoyote kwa timu iliyoshinda ulitaka Al Ahly na Wydad watoe macho kihivyo?
We hujiulizi why ikiwa champions League Ahly lazima umkute fainali?

Caf waipandishe hadhi hiyo AFL iwe michuano namba moja inayotoa bingwa wa Afrika uone huyo Mamelod aliyechukua hii mara moja wakati wa majaribio kama hajarudi kwenye default mode yake ya robo na nusu kila mwaka

Ahly wanataka heshima ya Afrika siyo kuweka kombe tu bila malengo unakuwa bingwa hueleweki bingwa wa nini huongezi points wala huna kwa kuwakilisha na huo ubingwa wako sasa hilo si sawa na MAPINDUZI CUP lenye hela nyingi.
 
Katika hizo 5 za mwisho. Esperence na yeye aliokota ubingwa.

Esperence Sio mnyonge kwenye kutwaa mataji ya ligi ya mabingwa Africa
Yeah kwenye 5 za mwisho
Esperance 01
Wydad 01
Al Ahly 03
Atleast tuongelee hao sio tuzungumzie timu kwenye miaka mitano ya mwisho sio tu kubeba hata kunusa fainali moja hakuna.
 
Nakiri kwamba Hersi alizingua kusema fainal ni Al ahly na Mameloids
Tuweke akiba ya maneno! Ningekua ni mimi ningejibu
' Timu yoyote iliyojipanga vyema inaweza kucheza fainal inaweza ikasa ni Al ahly, Yanga, Mamelod hata TPM'

Hersi pia alichangia kuwakuza sana wale Simba B
 
Si ndio maana nikasema mamelodi kushindwa kuwafunga yanga maana yake yanga wamefikia ubora wa mamelodi, sasa mbona hamueleweki amueni moja basi ninyi ni bora au wabovu maana ninyi mnajiita timu bora ilihali hamjafikia walipofikia mamelodi ambao mnawaita wabovu, yani yanga ni kama mna vigezo vyenu wenyewe vya kurate ubora na ubovu wa timu
 
ninyi mnajiita timu bora ilihali hamjafikia walipofikia mamelodi
Ubora gani? Hebu utaje .

Tukuulize kwanza uthibitishe ubora wao uliousema wao bora na hawana hata goli tangu makundi walipomfunga pyramid ..

Sasa ubora wao uko wapi?

Nj team average sawa tu na kina yanga
 
yanga ni kama mna vigezo vyenu wenyewe vya kurate ubora au ubovu wa timu
Nadhani nyie ndiyo mna vigezo vyenu ila ukweli upo wazi
Mnahype sana vitu kuliko uhalisia.

Tukumbuke kabla yanga hawajakutana na mamelodi.
Kauli zenu zilikuwa

"Alliende thamanj yake unapata kikosi kizima yanga"

"Yanga akitoboa sana anakula 5"

"Mamelodi walishampiga Al ahly 5"

"Kuna mokoena pale kati yanga watajjta"

"Pale Loftus stadium huwaga hatoki mtu"

Wakati hawakupata hata goli moja wajameni ni penati zikawaokoa sababu ya sisi kushindwa kutumia nafasi za wazi kabisa ambazo wao hawakupata ..

Wakubwa wako final kama unavyoona haya hao mamelodi unaodai wakubwa wako wapi????
 
Aliongea kama raisi wa vilabu Africa sio kama rais wa yanga


Jamaa mjanja mjanja sana huyu injjnia anataka yanga isifuatiliwe sana huku anapiga progress kimya kimya

Wakishtuka tupo mbali tayari
 
Timu kutolewa sio ubovu sometimes football ina wonders juzi tu hapo Madrid kamtoa Man city ki ajabu ajabu
 
Kibonde huyu anaetupiga kila siku?
 
Simba alipigwa nje ndani mkachonga sana, ohh tumebaki mabingwa watupu Sasa huyo bingwa wako nae kapigwa nje ndani
 
Takwimu zinaonesha kuwa Mamelodi ndiyo vibonde ukiangalia timu hizi nne zilizoingia nusu fainali.

Bila shaka Hersi na wachambuzi uchwara wataelewa kuwa uwekezaji pekee haukubebi kwenye football.
 
Sio hersi tu...watanzania karibu wote mliwatukuza kabla

Ila uzuri watanzania huwa wanafiki ..unafiki unawasaidia sana
 
Simba alipigwa nje ndani mkachonga sana, ohh tumebaki mabingwa watupu Sasa huyo bingwa wako nae kapigwa nje ndani
Wanaopigwa nje ndani wanajulikana..
Unapigwa nje ndani kimataifa cafcl
Unapigwa nje ndani kitaifa nbcpl
 

Haina tofauti na SSC

Kila mwaka ni robo fainal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…