Mamelodi ni Overrated, sijui ukubwa waliupataje

Super cup wamechukuwa timu gani? Tanzania imejaa mashabiki uchwara na wachambuzi mavi.
Super Cup ipi unaongelea wewe hujui mpira wa Afrika kaa utulie
Bingwa wa Super cup ni USM Alger ya Algeria walimfunga Al Ahly ya Misri.
Huyo Mamelod wako ana uhusiano gani na Super cup na yeye sio bingwa wa Africa wala shirikisho?
 
[emoji16]
 
KWahiyo toka 2016 Mamelod mafanikio pekee kwenye Caf champions league wanayoweza kujivunia ni kumfunga Al Ahly 5 na kupata matokeo Cairo?
sasa hiyo ni timu kweli yenye malengo? Yaani kila mwaka ni robo fainali kama simba au waokote kibonde robo waishie nusu shughuli imekwisha (maana nusu hakuna kibonde) unakuja
kutuambia ni timu tishio Afrika

Sasa kuna maana gani umfunge Al Ahly 5 then ukatolewe robo fainali na Petro de Luanda kwa kushindwa kushinda hata mechi moja kati ya 2

Wydad Casablanca hawajawahi kumfunga Al Ahly 5 wala kushinda mchezo cairo ila ni mabingwa wa Champions league mwaka 2022.

Hata hao Esperance wamefika Final jana na ni mabingwa 2019 sio kwa kumfunga Al Ahly 5 au kwa kushinda Cairo
Huwezi kuwa bingwa wa afrika kwa kumfunga Al Ahly pekee, ubingwa hauji kwa mechi moja
 
Basi tuseme Mamerod ni mbovu ila Yanga ni mbovu mara 3 ya Mamerody.
 
Mechi 4 bro za CAFCL toka robo hawajashinda wala kugusa nyavu.
 
Yamekuwa hayo tena jamani? Mara hii mmesahau Ubuntu Botho?
Mara hiii Mamelodi Wabovu 😅 tuliwauliza hapa waseme kabisa kabla hatujacheza nao wakasema sio wabovu...
Hakuna timu imepita miguuni kwa Yanga isijekuitwa mbovu 😃😃 Yanga inazifanya timu zisionekane bora tena
 
Timu huwa zinapanda na kushuka,

Kama ambavyo unaiona simba ndivyo ilivyo Mamelody.

Kitendo cha Simba kushuka Kwa kipindi hiki huwezi kusema ni timu ndogo bali ni upepo tu


Hivyo hivyo Kwa Mamelody.

Kumbuka Al ahly alishindwa kuchukua kombe la AFL mbele ya Mamelody.

Ukisema hivyo hata Wydad Casablanca utasema ni timu ndogo.
 
Mashindano ya vilabu ya CAF yamejaa mizengwe mitupu. Nimeyadharau kabisa, hayana tofauti na mizengwe ya championship huku kwetu. Motsepe na Waarabu ni matapeli.
 
Ubora gani? Hebu utaje .

Tukuulize kwanza uthibitishe ubora wao uliousema wao bora na hawana hata goli tangu makundi walipomfunga pyramid ..

Sasa ubora wao uko wapi?

Nj team average sawa tu na kina yanga
Oohh kwahiyo mara hii ninyi mmeshakuwa wabovu siyo bora tena
Ndio sasa kwani hayo yote ni uongo si ni ukweli yani hiyo mbinu mliyoitumia ya kupaki basi timu yoyote hata ihefu wangeitumia wasingefungwa, mshukuru hata watu walivyokuwa wanawahype hao mamelodi iliwasaidia kucheza kiuogauoga, vinginevyo mngerelax mngefunguka mngekula nyingi
 
Kwa msimu huu mamelodi wamedrop sana, mno ukilinganisha na misimu mitatu iliyopita. Bado naiona kama timu tishio kufanya kwake vibaya ni kawaida sana kwenye mpira wa miguu vilabu vingi hukumbwa na hali hiyo.
 
Kwa msimu huu mamelodi wamedrop sana, mno ukilinganisha na misimu mitatu iliyopita. Bado naiona kama timu tishio kufanya kwake vibaya ni kawaida sana kwenye mpira wa miguu vilabu vingi hukumbwa na hali hiyo.

1. Misimu wa mwaka 2024 mamelodi katolewa nusu fainali na esperence

2. Msimu wa mwaka 2023 mamelodi alitolewa nusu fainali na Waydad

3.Msimu wa mwaka 2022 mamelodi alitolewa robo fainali na Petro Atletico.

Kwa ujumla Katika miaka 10 iliyopita.

Mamelodi kafika nusu fainali mara 3.

Kafika fainali mara 1.

Na kombe amebeba mara 1 mwaka 2016.

Hiyo ndio CV ya mamelodi inatangazwa ni timu kubwa sana ya kutisha
 
Kila timu ni bora kabla ya kukutana na yanga.lkicheza na yanga tuu,tayari itaonekana ya kawaida tuu!
 
Mbona kila siku huwa tunaongea hapa, hata Simba inavyojiita kubwa kimataifa huo ukubwa unatoka wapi. Sio Simba sio Yanga inamzidi ukubwa Zamalek hata kama hatumuoni klabu bingwa.
Basi waambie mashabiki wenzio wa yanga waache kujiita wakubwa, sisi simba tunajijua kwamba ni wa kawaida sana wala hatuna ukubwa wowote, ila ninyi kutinga tu hatua ya makundi mkaanza kujiona wakubwa sana
 
Ni timu ya kutisha kama ilivyo man city ila sio timu kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…