Watu wanaangalia performance yao ya hivi karibuni msifikiri wanaropoka tu, msimu uliopita tu hapo walimpiga Al Ahly goli 5 na msimu huu wamechukua kombe la AFL, huku wakimtoa Al Ahly kwenye semi finals
Bado hatujaongelea AFCON iliyoisha mwaka huu, timu ya SA ilivyoperform vizuri hasa ilipoitoa Morocco tena huku ikiondoka na clean sheet, na zaidi ya nusu ya first eleven ya SA walikuwa ni Mamelodi Sundowns
Sema basi tu kwa vile walikutana na Nigeria ambayo wachezaji karibu wote wanachezea vilabu vikubwa Ulaya, ndio wakatolewa wakaishia kuwania na kushinda nafasi ya tatu, kwahiyo siyo kwamba ni timu ndogo inawezekana labda imeanza tu kushuka viwango au kocha kuna mahali anakosea