Mamelodi Sundowns FC watakuwa Mabingwa Wa CAF Champions League 2021

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari!

Nimerudi tena baada ya kimya kirefu juu ya chambuzi za soccer, twende pamoja. Hadi sasa ni hatua ya robo fainali ya CAFCL ambapo timu nane bora ndio zimebaki hadi sasa ambazo ni Wydad Casablanca, Mamelodi Sundowns, Simba Sc, Esperence, Kaizer Chiefs, Al Ahly, Mc Alger & CR Belouizdad.

Haya twende taratibu kabisa hapa maana kama ratiba inavyotarajiwa kuanza kesho na siku zinazofata.

Upande wa Mc Alger Vs Wydad Casablanca mechi hii ni nyepesi sana kwa hawa Wamorocco hivyo Wydad Casablanca atapita kutinga nusu fainali.

Kaizer Chiefs Vs Simba Sc hapa mechi wengi watampa nafasi Simba Sc kutinga nusu fainali ila ukweli ni kwamba hapa ni 50/50 yeyote anaweza kutinga nusu fainali kati ya hawa wawili.

Hivyo basi nusu fainali kwa upande huu Wydad Casablanca atakutana na Simba Sc/Kaizer Chiefs ila mambo yatakavyokuwa ni rahisi sana hapa. Wydad Casablanca kwa sasa kama umetazama mechi zake amekuwa si wakutisha sana hivyo basi kati ya Simba Sc/Kaizer Chiefs ndio ataingia Fainali huku Wydad Casablanca atakupiliwa nje ya mashindano katika hatua hiyo ya nusu.

Upande wapili wa Shilling mambo ni mepesi kwa bingwa huyu Mamelodi Sundowns Fc maana ataanza kwa kumpiga nyingi Al Ahly (Bingwa mtetezi) na kutinga nusu fainali ambapo atakutana na Esperence ambaye atakuwa amemtoa Mc Alger.

Mechi ya Mamelodi Sundowns Fc Vs Esperence itakuwa rahisi mno kwa Wasandawe hawa kutoka South Africa.

Fainali itakuwa ni Mamelodi Sundowns Fc Vs Simba Sc/Kaizer Chiefs na mambo yatakuwa mepesi zaidi na zaidi kwa Mamelodi Sundowns.

Hivyo namaliza kwa kusema pongezi kwa Mamelodi Sundowns Fc mabingwa wa CAFCL 2021.

Mtasema huyu mpiga ramli vipi tena hizi ni hesabu rahisi kabisa kwa Mamelodi Sundowns Fc japo karata zangu za uzi uliyopita ulibuma vibaya mno.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Tatizo umekariri. Ahly atamtoa mamelod sundowns. Fainali ni simba na Ahly na yeyote kati ya hao atabeba ndoo.
 
Kama ulivyoangukia pua kwenye utabiri wako kwenye Uefa champions league utaangukia pua tena kwenye utabiri wako wa caf champions league!! Wewe siyo mchambuzi bali ni mpiga ramli wa soka!! Je PSG yako iko wapi?
 
Ligi ya UEFA 2021 PSG watacheza final na timu gani vile,embu tukumbushane kidogo ndugu yangu?
 
Haujui utabiri mkuu
 
Ulianza kwa PSG. Kitu kmebuma sasa UMEKIMBILIA HUKU. Endeleeni KUTAPATAPA
 
Fainali itakuwa ni Mamelodi Sundowns Fc Vs Simba Sc/Kaizer Chiefs na mambo yatakuwa mepesi zaidi na zaidi kwa Mamelodi Sundowns.
Utabiri unatakiwa uwekwe katika raundi ya awali kabisa wakati akina Yanga wanashiriki. Mtu umeona mwelekeo halafu unajidai eti kutabiri, toa unyani na u mbwa wako hapa
 
Kama ulivyoangukia pua kwenye utabiri wako kwenye Uefa champions league utaangukia pua tena kwenye utabiri wako wa caf champions league!! Wewe siyo mchambuzi bali ni mpiga ramli wa soka!! Je PSG yako iko wapi?
Kuna mambo nilikosea hizi ramli zitakwenda kwa 100%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…