Mamelodi Sundowns Wanapaswa Kuthibitisha Ubora wao Dhidi ya Yanga SC

Mamelodi Sundowns Wanapaswa Kuthibitisha Ubora wao Dhidi ya Yanga SC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Pamekuwa na kelele kibao na lukuki kuhusu Ubora na Ukubwa wa Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini. Hata hivyo dhana hiyo imejengeka mno machoni pa watu kwa sababu ya Ufanisi wao wa kucheza pasi nyingi zisizo na msingi katika dakika 90 za mpira.

Sasa wamepata fursa nyadidi ya kuthibitisha ukubwa wao. Kwani mbele yao ni Dar es Salaam Young Africans SC ambao ni klabu yenye falsafa tofauti na vilabu ambavyo Mamelodi imekuwa ikicheza navyo PSL.

Wako na jukumu zito la kuuthibitishia umma wa waafrika kwamba wao ni moingoni mwa timu kubwa barani africa.

Karibu Dar es salama Mamelodi sundown. Tunawangoja kwa bashasha na matamanio mazuri mno.

Sho Sho!
 
KAZI ipo
IMG-20240312-WA0071.jpg
IMG-20240312-WA0069.jpg
 
Mamelodi jina kubwa kuliko uwezo wake juzi tu tp Mazembe mchovu katoa nae agreggate ya 1 kwa 1.. tena kwa kupewa penalty south sababu rais wa caf alikuwepo mwenye timu yake.

Timu ina miaka mingi haijawai kufika fainali wala kubeba kombe. Nusu yenyewe anafika mara chache. Ila inasifiwa kama nini.

Ingekuwa mtoano nimepangiwa kina Esperence, Al ahly ningekubali nimetolewa. Ila sio mamelodi
 
Belozdad ilikuwa hivi hivi vimaneno vya kipumbavu mkaishia kuinamisha nyuso babada ya kula chuma 4 tutunze akiba ya maneno
Al ahly alikula chuma ngapi kama mlivyojitapa? Akiba ya maneno nyinyi uto hamuwezi kutunza hadi mnawaona Mamelod ni kama CRB? Uto ndie underdog punguzeni matarajio.
 
Mamelody haisemwi kuwa timu bora kwasababu watu wamejiskia tu kutamka.

Mamelody ni timu bora based on data.

Na kuwa bora haina maana kuwa wewe ni untouchable kuwa hufungiki, ingekuwa ni hivyo basi wangepewa kwanza Kombe lao waliweke kabatini kisha ndio waanze kucheza.

Kwenye mpira kuna bahati pia l, kuna muda timu ndogo inaweza kupata matokeo dhidi ya timu kubwa unexpectedly na hili nimelishuhudia kwenye mechi yenu na Cr Belarouzidad.

Msimu jana kwani Mamelody alitokaje?

Si alitolewa kwa aggregate na Wydad, sasa nani alitegemea Wydad aliyetoa sare kwake na Mamelody ya 2-2 aje ashikilie bomba kwa Madiba na kumfanya Mamelody aage mashinda
no?

Kwa hiyo pamoja na kwamba tunajua bahati kwenye mpira zipo ila bado hatuwezi kupuuza stats za ubora na kusema Yanga ina ubora wa kumtoa Mamelody kisa tu ilimfunga Cr Belarouzidad goli 4.

NB: msimu wa 2020/21 Mamelody akiwa ugenini alimfunga Cr Belarouzidad nyumbani kwake goli 5 kwenye hatua ya makundi.

Msimu ulioisha Cr Belarouzidad alifungwa goli 4-1 na Mamelody tena akiwa nyumbani.
 
Mamelody haisemwi kuwa timu bora kwasababu watu wamejiskia tu kutamka.

Mamelody ni timu bora based on data.

Na kuwa bora haina maana kuwa wewe ni untouchable kuwa hufungiki, ingekuwa ni hivyo basi wangepewa kwanza Kombe lao waliweke kabatini kisha ndio waanze kucheza.

Kwenye mpira kuna bahati pia l, kuna muda timu ndogo inaweza kupata matokeo dhidi ya timu kubwa unexpectedly na hili nimelishuhudia kwenye mechi yenu na Cr Belarouzidad.

Msimu jana kwani Mamelody alitokaje?

Si alitolewa kwa aggregate na Wydad, sasa nani alitegemea Wydad aliyetoa sare kwake na Mamelody ya 2-2 aje ashikilie bomba kwa Madiba na kumfanya Mamelody aage mashinda
no?

Kwa hiyo pamoja na kwamba tunajua bahati kwenye mpira zipo ila bado hatuwezi kupuuza stats za ubora na kusema Yanga ina ubora wa kumtoa Mamelody kisa tu ilimfunga Cr Belarouzidad goli 4.

NB: msimu wa 2020/21 Mamelody alimfunga Cr Belarouzidad akiwa kwake goli 5 kwenye hatua ya makundi.

Msimu ulioisha Cr Belarouzidad alifungwa goli 4-1 na Mamelody tena Belouzidad akiwa nyumbani.
Sisi Yanga hatuna maneno mengi kama waimba taarabu,tunawaambia hivi tutakutana hapa hapa baada ya mechi zote mbili.
 
Yanga wanatakiwa wafanyie kazi mambo kadhaa ya muhimu

1. Yao asijisahau na kupanda sana sio kila timu ni ya kushambulia kwa kutumia wing back akirudia makosa dhidi ya Al ahly cairo na belouzidad Algeria imekula .

2. . Tackling za backline ya yanga hasa bacca na lomalisa wawe makini sana dhidi ya washambuliaji kina shalulile na maseko na kusababisha penalti, faulo au kadi , wacheze clean football wasicheze rafu .

3 . Kona na mipira ya krosi wawe makini kuna beki wao Raymond mvala anaruka sana vichwa., Huyu jamaa ndiyo mrefu zaidi Kati Yao .

4. Diara alicheza nao afcon anawajua anaweza kuchangia point chache kwa wenzake .

Nb: mamelodi ndio ilikuwa timu ya afrika kusini iliyoshika nafasi ya 3 afcon ikiwasumbua morocco na Nigeria hivyo kazini kwa young Africans kuna kazi ila siku hiyo wakicheza kwa nidhamu na ari Kama walivyocheza na simba , Al ahly Dar na belouzidad lolote linaweza kutokea .
 
Back
Top Bottom