Mamelodi Sundowns Wanapaswa Kuthibitisha Ubora wao Dhidi ya Yanga SC

Mamelodi Sundowns Wanapaswa Kuthibitisha Ubora wao Dhidi ya Yanga SC

Pamekuwa na kelele kibao na lukuki kuhusu Ubora na Ukubwa wa Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini. Hata hivyo dhana hiyo imejengeka mno machoni pa watu kwa sababu ya Ufanisi wao wa kucheza pasi nyingi zisizo na msingi katika dakika 90 za mpira.

Sasa wamepata fursa nyadidi ya kuthibitisha ukubwa wao. Kwani mbele yao ni Dar es Salaam Young Africans SC ambao ni klabu yenye falsafa tofauti na vilabu ambavyo Mamelodi imekuwa ikicheza navyo PSL.

Wako na jukumu zito la kuuthibitishia umma wa waafrika kwamba wao ni moingoni mwa timu kubwa barani africa.

Karibu Dar es salama Mamelodi sundown. Tunawangoja kwa bashasha na matamanio mazuri mno.

Sho Sho!
Kelele au siyo.
Kumbee ni kelele!!
Ujinga uki advance unakuwa upumbavu! Na upumbavu ni kipaji!
 
Sisi Yanga hatuna maneno mengi kama waimba taarabu,tunawaambia hivi tutakutana hapa hapa baada ya mechi zote mbili.
Hamuwei kuwa na maneno kwasababu mnajia hao sio Rivers.

Rivers mlivyopangiwa nao si mlipiga makofi nyie na kelele kibao?

Leo ndio kwanza nimeashangaa mmeanza ku question na mfumo wa kupanga draw eti CAF inawahujumu.
 
NB: msimu wa 2020/21 Mamelody alimfunga Cr Belarouzidad akiwa kwake goli 5 kwenye hatua ya makundi.

Msimu ulioisha Cr Belarouzidad alifungwa goli 4-1 na Mamelody tena Belouzidad akiwa nyumbani.
Kwa takwimu hizi, fungeni huu uzi
 
Upo sawa
Team zote ili kujipima ubora wao lazima wacheze na yanga
 
Hizi ni porojo za kiswaili.yaani mamelod athibitishe ubora kwa vibonde.unashida yakufikiri wewe.Mdogo ndiye anayejipima kwa mkubwa sio mkubwa kwa mdogo.
 
Mamelodi jina kubwa kuliko uwezo wake juzi tu tp Mazembe mchovu katoa nae agreggate ya 1 kwa 1.. tena kwa kupewa penalty south sababu rais wa caf alikuwepo mwenye timu yake.

Timu ina miaka mingi haijawai kufika fainali wala kubeba kombe. Nusu yenyewe anafika mara chache. Ila inasifiwa kama nini.

Ingekuwa mtoano nimepangiwa kina Esperence, Al ahly ningekubali nimetolewa. Ila sio mamelodi
Uku ni kujifariji.Endelea kuota.
 
Hivi uko sawa wewe baada yakusema uto ndiyo wakwenda kuthibitisha ubora dhidi ya mamelody hizo dharau zenu ndiyo ziliwaponza kwa al ahaly
 
Yanga wanatakiwa wafanyie kazi mambo kadhaa ya muhimu

1. Yao asijisahau na kupanda sana sio kila timu ni ya kushambulia kwa kutumia wing back akirudia makosa dhidi ya Al ahly cairo na belouzidad Algeria imekula .

2. . Tackling za backline ya yanga hasa bacca na lomalisa wawe makini sana dhidi ya washambuliaji kina shalulile na maseko na kusababisha penalti, faulo au kadi , wacheze clean football wasicheze rafu .

3 . Kona na mipira ya krosi wawe makini kuna beki wao Raymond mvala anaruka sana vichwa., Huyu jamaa ndiyo mrefu zaidi Kati Yao .

4. Diara alicheza nao afcon anawajua anaweza kuchangia point chache kwa wenzake .

Nb: mamelodi ndio ilikuwa timu ya afrika kusini iliyoshika nafasi ya 3 afcon ikiwasumbua morocco na Nigeria hivyo kazini kwa young Africans kuna kazi ila siku hiyo wakicheza kwa nidhamu na ari Kama walivyocheza na simba , Al ahly Dar na belouzidad lolote linaweza kutokea .
Ondoa neno walivyo cheza na Ahly ,mechi zote mbili ni Ahly ndio alishindwa kutoa hukumu kila kitu kuanzia shoot on target,big chances missed ,dangerous attack,chance created ,number of passes nasema kila kitu yanga alizidiwa .
 
Uku ni kujifariji.Endelea kuota.

Najua Now umemuolewa mtoa mada, maana Ulipotea sana baada ya mamelodi kupigwa na esperence nje ndani.

Nazani sasa ulielewa point yake kwa nini alimuogopa esperence kupangiwa yanga kuliko mamelodi.

Caf champions league ina timu zake za kuziogopa.

mamelodi sio mmojawao wa timu za kuziogopa
 
Back
Top Bottom