Mamia ya wanafunzi wa Namibia wakutwa na Corona

Mamia ya wanafunzi wa Namibia wakutwa na Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Namibia imethibitisha visa 11,373 vya coronavirus


Namibia imethibitisha visa 11,373 vya coronaImage caption: Namibia imethibitisha visa 11,373 vya corona. Zaidi ya wanafunzi 300 nchini Namibia wameambukizwa virusi vya corona baada ya shule kufunguliwa.

Wizara ya Afya imesema wanafunzi walioambukizwa wengi wao wanasoma shule za mabweni. Waziri wa Afya Kalumbi Shangula amesema muongozo uliowewa kuzuia kusambaa kwa maambukizi unastahili kuzingatiwa hasa katika maeneo ya shule.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti mlipuko wa virusi vya corona katika moja shule iliyoko eneo la Oshikoto inayosadikiwa kuwa na idadi ya juu ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Namibia ilifunga shule mwezi Machi lakini zikafunguliwa tena mwezi Juni baada ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19
 
Back
Top Bottom