Mamlaka 05 za waumini wa kawaida kabisa zilizoporwa na watumishi

Mamlaka 05 za waumini wa kawaida kabisa zilizoporwa na watumishi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
1: UKUHANI WA KIFALME
Kila muumini ni Kuhani na no mfalme chini ya mfalme mkuu Mungu Muumbaji. Kuhani kwa maana ya kazi ya kuwapatanisha wasiomjua Mungu na Mungu wao. Mfalme wa maana hamilikiwi na mtu au vitu ameubwa kumiliki huku anamilikiwa na Mungu tu. Viongozi wanabaki na heshima yao ya kuhakikisha hatutoki mwenye hadhi hii tukiyopewa na Baba.

Ushahidi.💥
Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu
1 Petro 2:9


2: MAMLAKA YA KUFUKUZA MAPEPO, KUDHIBITI WACHAWI NA NGUVU ZA GIZA ZOTE KWA AINA YAKE
Kimsingi kuwa mkristo ni kuwa Superior juu mbali kabisa ya kila nguvu za giza. We have superiority Complex over Satan.
Hii kazi sio ya wachungaji tu, ni kila muumini anayejitambia. Ni ukosefu wa maarifa ndio umeleta ukristo goigoi wa kutegemea watumishi kutoa mapepo na uchawi. Anza mwenyewe zima giza ofisini, nyumbani, kwenye ukoo, safarini au popote uwapo. Hii ni amri sio ushauri. Ukivunja hii umevuja amri ya Mungu kama zile 10.

Ushahidi 💥
Luka 10:19 Tazama nimewapa Amri ya kukanyaga nyoka na nge, na Nguvu zote za yule Adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

3: KUFANYA MIUJIZA

Kutoa mapepo au kuzima uchawi sio miujiza. Maana mapepo na uchawi ni giza. Na mkristo yuko kwenye mwanga. Hatutegemei mwanga kufukuza giza iwe muujiza. Ni sawa na kusema kuwasha taa kwenye chumba chenye giza ni muujiza.
Muujiza ni jambo kubwa linalovunja sheria za asili. Linalowaacha wataalam midomo wazi. Linalovunja kanuni za kidaktari, kieengineer, physics na baiolojia. Hii kazi licha hutolewa kama karama lakini kila muumini wa kawaida inapaswa kuwa taratibu za kawaida maishani mwake. Hii wasiachiwe watumishi, watumishi muda mwingi wanapaswa kutumia kufundisha na kulea waumini.

Ushahidi 💥
Waebrania 2:4
Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

4: KUFANYA KAZI YA KUWALETA WATU KWA MUNGU
Hii ni amri. Kila mkristo bila kujali anaajira au biashara fulltime, lazima ajue na yeye yuko fulltime kuokoa watu wanaopotea. Hii ni amri. Kuivunja ni sawa na kuvunja amri kumi. Hii ni kazi rahisi sana na kuna njia malaki za kuifanya kama utapenda na Mungu atakupa mbinu. Unaona ngumu kwa sababu unatafuta wasiotayari kuvunwa wakati amri ni kuvuna mavuno (waliotayari sio kila mtu maana wengine hawako tayari bado kujiunga na ufalme).

Ushahidi💥
Mathayo 28:19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,

5: KUOMBEANA

Wakristo ni familia. Familia ambayo baba ni Mungu, licha ya mgawanyiko wa majukumu katika familia, licha ya kuwepo viongozi wenye kazi ya kubariki na kuombea kundi, sisi kwa sisi wote tunapaswa kuombea. Wote tunapaswa kuombeana. Hapa kwenye kuombeana hakuna mkubwa wala mdogo. Kama Paulo aliomba aombewe hata sisi tunapaswa kuombeana. Dini ya mtu mmoja mkuubwa anaombea wengine ambao ni wadogo na watabaka la chini ni matokeo ya Lucefarian spirit. Roho ya kushusha wengine na kutaka ukuu kwa familia ya Mungu. Ombea mchungaji ombea mtume, ombea manabii, maaskofu na viongozi mbalimbali kwa aina zao.

USHAHIDI 🔥
Warumi 1:12
yaani, tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu.

1 Petro 4:10
kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
 
Back
Top Bottom