KERO Mamlaka husika chukueni hatua juu ya ujenzi holela maeneo ya barabara, sehemu za kupita kwa miguu zimekuwa finyu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
2,805
Reaction score
3,640
Ewe Waziri wa Ardhi, Halmashauri, Tanroads na tarura.

Tunaomba sana watu wote wanaojenga ovyo magenge mitaani, vibanda vya mkaa na wale waliojenga road reserve hata kama ni wakubwa wabomolewe haraka.

Sehemu za kupita zimekuwa finyu. Fujo na uswahili umezidi. Piteni mitaa yote Dar mvunje hivi vigenge.

Msisahau hata baa maarufu ya Rose garden imejengwa kwenye road reserve . Kusiwe na exceptions.

Maeneo kama Magomeni Mikumi watu wote wamezidisha kujenga mbele ya mawe yao ya viwanja. Mpaka waenda kwa miguu hawana pa kupita.

Nawasilisha
 
Mkuu umeishauri na kuikumbusha mamlaka husika wajibu wao ni jambo jema. Rose garden imekukosea nini mkuu? Mbona una nongwa nayo?

Uwepo wa bustani ya Rose pale Kuna umuhimu sana na unasaidia sana wakazi wanaoishi maeneo yale. Wanaoijua na kufahamu Ile bustani umuhimu wake hawatakubaliana na wewe.
 
Ni mwaka wa uchaguzi huu.. Hawataondolewa
 
Khahahahahahha,maiti zinazotembea mojawapo ni hii🤔.
Mpaka umemtaja unaemlenga shubamiti wewe.
Uzao WA CCM matokeo ndo haya sasa.
Watu wanashida,ila ni tofauti na uliyoiadres
 
Sina shida na bustani ya rose lakini watakaposafisha mji mkubwa asionewe huruma haitakuwa haki. Yaani ma car wash.yamezidi road reserve. Kiusalama wa watembea kwa miguu na vipofu ni mdogo sana.

Kwa rose garden najua hawatabomolewa sababu hata jiwe magufuli alibariki wawepo pale. Na sina nia wabomolewe. Ila thinking in bigger picture
 
Kwa mfano eneo la mwenge kijijini lilitakiwa libomolewe wote waliojiunganishia vyumba zaidi ya.maeneo yao wengine wameziba.mpaka barabara.

Sisi waswahili nani katuloga hata maeneo ya kupanda miti hakuna na tunaachia taasisi zingine zinajenga mafremu ya maduka mpaka kwenye road reserve. Tukajifunze zimbabwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…