Mamlaka husika ichunguze uthabiti wa chanjo ya kuku ya Tatu Moja

Mamlaka husika ichunguze uthabiti wa chanjo ya kuku ya Tatu Moja

Soko limekuwa holela sana mkuu kila mtu anaingiza sokoni kila kitu bila ubora wake kuthibitishwa na hatimaye kuleta hasara kwa watumiaji na wengine kwa nguvu waliyonayo wanaweza kuhakikisha bidhaa yao ndiyo itumike kuliko nyingine hata kama haina uwezo
Hii ndio shida
 
Hayo ya kufundisha usafi kwa wafugaji yaanzishie uzi wake mkuu ila leo ni kutaka kujua ufanisi wa hii chanjo ni wa uhakika kweli maana inalalamikiwa sana kuwa haifanyi vizuri kwenye kukinga
Hii ina maana kiliko hiyo chanjo
This is fact my dear
 
mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipata vifaranga 30. niliwatunza vizuri bila kutumia dawa aina yoyote. walipofikisha mwezi mmoja nimewachanja kutumia tatu moja kwa usahihi kabisa. cha ajabu haukupita mwezi mmoja baada ya chanjo. kuku wote wameshijwa ndui. Tunaomba wahusika wafwatilie kwa karibu hilo swala ijulikane tatizo liko wapi.
 
Hata mimi ni mhanga wa hiyo chanjo, niliinunua nikawapa vifaranga wangu na woote walipatwa na ndui na kufa wooote.

Tokea hapo natumia ile chanjo ya sindano, ni nzuri sana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Unafuga kuku mazingira machafuuuu maranda unabadili mara moja kwa mwezi! Unamwagamwaga maji kunanukaaaa halafu UNATAKA TATU MOJA IKUSAIDIE kukufugia kuku!?

We tafuta mlalamishi hata mmoja mwambie mwende kwake kama atakubali! Kuna wafugaji wapuuzi sana
Hii ni kweli kabisa,!
Mtu kuku wameshaugua wameanza kufa eti ndiyo anawachanja!

Kuku mazingira Safi, kama wanaugua wapewe tiba Kwanza. Wapone, wakishamaliza dozi ya siku 5, wapumzishwe siku 1, baada ya hapo wapewe chanjo.
Wafugaji wanakosea kuku wameanza kufa, ndiyo wanakimbilia chanjo!
 
mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipata vifaranga 30. niliwatunza vizuri bila kutumia dawa aina yoyote. walipofikisha mwezi mmoja nimewachanja kutumia tatu moja kwa usahihi kabisa. cha ajabu haukupita mwezi mmoja baada ya chanjo. kuku wote wameshijwa ndui. Tunaomba wahusika wafwatilie kwa karibu hilo swala ijulikane tatizo liko wapi.
KABISA!TATU MOJA CHANJO NI YA UONGO,MWENYEWE KUKU ZANGU WALIISHA WOTEKABISA
 
Binafsi hiyo chanjo haijanisumbua,
Naitunza kwenye ubaridi, nafikiri hii ya kutunza at all temperatures Sisi tuna joto na fukuto Hadi 35°C, nikitumia inayobaki naitupa!

Na kabla ya kuwapa chanjo nawapa tiba za coccidiosis na mafua, siku5, ya 6 nawapa maji tu, hata kama hawaugui maana hatujui wanapooanza kuumwa! Ufugaji ni Vita!
 
hivi hii chanjo ya tatu moja inu ujazo wa mil ngapi nimejaribu kuangalia walipoandika ujazo sioni nimeona tu wameandika 200dose ..
mana leo nimenunua hii chanjo imefungwa kwene kinailoni chenye barafu nimefika nayo nyumbani nikasema niiangalie vzr nakuta kichupa kipo nusu yani nusu kabisa,kwakuwa nilipoinunua sio mbali na nyumbani ikanilazimu kuirudisha muuzaji akaniambia ndio ujazo wanaoweka vichupa vyote vipo nusu amenitolea na vichupa vingine vilivyopo kwene friza lake nikajiridhisha kuwa vyote vipo nusu
 
Nimetumia chanjo hiyo kuwachanja kuku nilichogungua hii tatu moja unapoinunua hakikisha hipotezi ubaridi hata kidogo hadi inafika nyumbani na wakati wa kuwachanja iwe na ubari haswa pili usiwachanje mchana wa jua kali wacje usiku nasikia dawa hii haipatani na mionzi ya jua kabisa mwisho matumizi ni mara moja ukirudia mara mbili ni bahati nasibu nimejaribu hivyo na nimefanikiwa japo bado sijaiamini kwa asilimia mia.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom