Mamlaka kanuni zinaua sekta ya maziwa nchini

Mamlaka kanuni zinaua sekta ya maziwa nchini

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Wana JF kwa muda mrefu sasa, wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakilalamika kwamba kanuni lukuki na kodi kubwa zimekuwa zikichangia kudumaa kwa biashara na kuwavunja moyo wajasirimali.

Malalamiko yao yanatokana na ukweli kuwa ili mtu asajili biashara yake anatakiwa kupitia kwa mamlaka zaidi ya 11 ambazo zinatoa vibali na leseni za biashara na mchakato huo unaweza kuchukua mwezi mzima bila usajili kukamilika.

Kutokana na mlolongo huo mrefu, wadau wanapendekeza kwamba iwepo mamlaka moja ambayo itashughulikia utoaji wa vibali ili kuokoa muda na kupunguza au kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.

Hivi karibuni malalamiko mengine yalitolewa na wasindikaji wa maziwa ambao nao wanaamini mamlaka zaidi ya 11 kwa mfano, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika sekta ya maziwa zinasababisha gharama za biashara kuwa kubwa.

Nimeelewa kuwa hawasemi kwamba kusiwapo na wadhibiti la, wanachohitaji ni wadhibiti wachache ambao watawasaidia wafanyabiashara wadogo kujiimarisha pia kusajili biashara zao,

Ninachoamini;

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wasindika Maziwa nchini (TAMPA) unaweza kuwasaidia wanachama wenzako ambao hawawezi kuzifikia mamlaka husika kwa haraka na urahis plz tusaidiane katika hili.
 
Back
Top Bottom