Mamlaka na nguvu ya Rais iendelee kubaki kama ilivyo kwenye Katiba

Mamlaka na nguvu ya Rais iendelee kubaki kama ilivyo kwenye Katiba

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
379
Reaction score
603
Kamwe mtu ambaye hana nguvu wala mamlaka hawezi kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa wale anaowaongoza.

Pia kinga ya Rais ibaki kama ilivyosasa kumtoa wasiwasi wa kufanya maamuzi na kutoa amri. Unapokuwa na wasiwasi pamoja na uoga wa kukosea huwezi kufanya kazi kwa ufanisi na uhuru.

Kitu pekee cha kuzingatia ni namna ya upatikana wa Rais ambae ni mwerevu na mwenye busara nyingi kuliongoza taifa kwa weledi na uzalendo.
 
Kukiwa na mihimili na taasisi imara huhitaji kumrundikia rais mamlaka makubwa, ndo maana baadhi ya nchi rais ni non-executive head of state, anamteua waziri mkuu ambaye ndo anakuwa na mamlaka ya kiutendaji.
 
Kumrundikia rais power kubwa ni hatari, ni kumfanya kuwa na maamuzi ya kifalme badala ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria.

Katiba inayompa mamlaka makubwa rais ni ya kidikteta, mahakama na bunge haviwezi Kuwa huru kutimiza Majukumu yake ipasavyo,

Mfano mzuri ni awamu ya tano namna rais alivyoingilia bunge na mahakama kwa kigezo kuwa yeye ndiye anayewateua.

Huu ni uenda wazimu
 
Back
Top Bottom