Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA, kujiendesha kidigitali kwa ufadhili wa TradeMark East Africa, TMEA

Mamlaka ya Chakula na Dawa, TFDA, kujiendesha kidigitali kwa ufadhili wa TradeMark East Africa, TMEA

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Niko hapa Serena Hotel DSM kuwaletea uzinduzi wa ON Line Porta ya TFDA ambao utawezesha mambo yote ya TFDA kuendeshwa kidigitali!.

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania, (TFDA) kwa ushirikiano na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) imezindua mfumo wa taarifa za kiutendaji, e-portal ambayo itawezesha TFDA kuhudumia wateja wake kwa mfumo wa kidigitali kwa kutumia mtandao wa internet ambapo sasa huduma za TFDA zitatolewa moja kwa moja kupitia mtandao wa internet hivyo kuleta ufanisi zaidi .

Mfumo unaozinduliwa leo umegharim TFDA takriban Tsh. 300 Milion na kutoka Taasisi ya TMEA imetumia Dola za Marekani $ 250,000 kwa lengo la kuboresha mfumo huo. Uzinduzi huu unahitimisha maboresho yaliyoanza mwaka 2012. Taasisi ya TMEA imeahidi kuendelea kusaidia TFDA kuboresha mifumo yake ya usimamizi wa huduma za kimaabara. Msaada wa ziada utaelekezwa kwenye kuinganisha TFDA na Tasisi za kifedha ili kuboresha mifumo ya malipo kwa njia ya mtandao. Na hatua ya mwisho ni TMEA itasaidia kuuingiza TFDA kwenye mfumo wa malipo yote nchini Tanzania, kupitia dirisha moja la kitaifa (National Single Window), mradi ambao uko kwenye maandalizi.

Akizungumza katika uzinduzi Dkt. Donan Mmbando, Katibu Mkuu Wizara ya Afya alisema,
“Mfumo huu unaozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kiudhibiti kwa maeneo ya utoaji wa vibali ya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya nchi kwa kuwa muda wa kuandaa vibali utafupishwa. Hata hivyo mfumo huu utasaidia katika kuhudumia wateja kwa ufasaha katika kusajili na ufuatialiaji wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. Ubunifu huu utasaidia kuongeza idadi ya wateja kufuata na kukidhi matakwa ya kisheria katika udhibiti hivyo kuimarisha usalama na ubora wa bidhaa zilizopo katika soko”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti B. Sillo aliongeza,
"TFDA inaishukuru sana TMEA kwa msaada wake kwa TFDA katika uanzishwaji wa e- portal, ambayo itarahisisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za vyakula, madawa, vipodozi, vifaa tiba na kuyafuatilia maduka ya dawa nchini Tanzania. Hii itaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na itarahisisha muda wa kazi na kurahisisha kufikia maamuzi.”

Mkurugenzi wa TradeMark East Africa Tawi la Tanzania Dk Josephat Kweka aliongeza,
"Portal hii inatarajiwa kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kupeleka bidhaa nje ya nchi, hivyo kuboresha mazingira ya kufanya biashara!. TMEA Tumefurahi kushirikiana na TFDA shirika ambalo kiungo katika kulinda na kuboresha bidhaa za afya ya umma wa Watanzania, huku ikihakikisha ufanisi wa viwango vya ubora na usalama wa bidhaa za vyakula, madawa, vipodozi na vifaa tiba. "


Umuhimu wa hii e-portal ya TFDA, itawezesha wafanyabiashara kuomba na kupata vibali vyote muhimu, kwa njia ya mtandao, bila kulazimika kufika TFDA, na wakati huo huo, pia utawawezesha maafisa wa TFDA, kupitia maombi hayo, kuyakagua na kuyaidhinisha kidigitali, kwa njia ya mtandao, ambapo huduma sasa zitatolewa usiku na mchana, sasa 24 kwa siku zikiwemo Jumamosi, Jumapili na sikukuu. (24/7) . Huduma hizi zitaunganishwa na mtandao wa Mfumo wa Taifa wa Malipo kupitia Dirisha Moja (National Electronic Single Window) ambao uko kwenye maandalizi.

Mfumo huu mpya wa kidigitali unaojiendesha wenyewe, utaboresha kasi ya utoaji wa vibali vya TFDA kuagiza, kuingiza na kusafirisha nje ya nchi, bidhaa za vyakula, madawa, vipodozi na vifaa tiba, hivyo kuimarisha uwezeshaji wa biashara.

Portal hii imewezeshwa na TMEA kama sehemu ya majukumu yake ya kukuza biashara ya kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

e-Portal hii ya TFDA ni mtandao unaotumia Teknolojia ya Habari na Mwasiliano (ICT) na inajumuisha ya Mfumo wa Management Information System (MIS) kwa watoa huduma, na Trade Portal kwa wapokea huduma ambao ni wafanya biashara.

Uwezeshaji huu kwa TFDA, kwa msaada wa TradeMark East Africa (TMEA), unalenga kuwezesha TFDA kuwahudumia wateja wake kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi.

TFDA imeanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Kiutendaji kutumika kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu, uhifadhi na uchambuzi wa taarifa kuhusu usajili, kanuni na ufuatiliaji wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na maduka ya dawa nchini Tanzania. Mfumo huu, utaongeza ufanisi katika utoaji wa maamuz na urahisishaji kazi ya usimamizi. Aidha, e- portal itashughulikia maombi ya leseni za kuagiza na kuuza bidhaa kwa njia ya mtandao, (online).

Matokeo yanayotarajiwa kutokana na e- portal hii ya TFDA ni online ni pamoja na:
• Kuongezeka kwa ufanisi kwa njia ya kuokoa muda wa kufanya biashana na kupunguza gharama kwa kwa wadau, kufuatia kuthitajika uwepo wa mtu wala hati katika ofisi za TFDA.
• upatikanaji wa taarifa na nyaraka kwa urahisi kwa kuingia mara moja tuu kwenye mtandao.
• Kuongezeka kwa viwango vya ufuatiliaji.
• Kuongezeka kwa ubora wa huduma, uwazi na uwajibikaji katika huduma zinazotolewa na TFDA

1. Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA)Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.

TFDA imeanzishwa chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura 219 na ilianza kutekeleza rasmi makujumu yake tarehe 1 Julai, 2003.
Dhima ya TFDA ni Kulinda afya ya Jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

Dira ya TFDA ni kuwa Mamlaka inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora, na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba kwa wote.


Majukumu ya TFDA ni kutoa leseni na utoaji wa vibali kwa ajili ya kuagiza na kuuza nje ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ndani na nje ya Tanzania.
• Udhibiti wa kuagiza na kuingiza nchini bidhaa .
• Uchambuzi wa maabara kudhibiti ubora, usalama na ufanisi.
• Kufanya uchambuzi wa masoko ya bidhaa hatarishi.
• Udhibiti na Ukuzaji Masoko ya bidhaa

Ili kujua zaidi kuhusu TFDA, tafadhali tembelea tovuti TFDA katika www.tfda.or.tz

2. TradeMark East Africa


TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani.
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.


TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.

Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www.
www.trademarkea.com


Paskali
TFDA NA TAASISI YA TRADEMARK EAST AFRICA (TMEA) WAZINDUA MFUMO WA UTOAJI VIBALI KWA MFUMO WA KIELEKITRONIKI,SOMA HAPO KUJUA


Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi (kulia), akibonyeza kituvye Dar es Salaam leo asubuhi, kuashiria uzinduzi wa mfumo wa utoaji vibali kwa njia ya kielekitroniki (e-portal) ambao utawezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuhudumia wateja wake kwa kutumia mtandao wa intaneti. Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa TFDA na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA)
Viongozi wakiwa meza kuu wakifuatilia uzinduzi huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Viongozi wakiwa tayari kuzungumza na wanahabari. Kutoka kulia ni Meneja wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA), Josephat Kweka, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo.
Maofisa Habari kutoka Kampuni ya PR ya PPR, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo (kushoto), akizungumza na wanahabari.





MAMLAKA ya Chakula na dawa nchini (TFDA), imezindua mfumo mpya wa utoaji vibali kwa mfumo wa kielektroniki ujulikanao kama 'e-portal'.

Mfumo huo uliogharimu kiasi cha sh. milioni 300 kwa ushirikiano wa taasisi ya Trademark East Afrika(TMEA) kwa kutoa dola za marekani 250,000 lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao.

Akizungumza Dar es Salaam leo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, Dk.Mkuu wa Serikali Muhammad Kambi alisema mfumo huo uliozinduliwa umekuja wakati muafaka kwani utasaiduia kuboresha huduma katika sekta ya afya kwa kuongeza uwazi, ukweli na kwa uharaka zaidi.

"Mfumo huu uliozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kudhibiti katika utoaji wa vibali vya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya nchi kwa kuwa wa kuandaa vibali utafupishwa na utaongeza faida katika mamlaka hiyo,"alisema.

Alisema mfumo huo utasaidia kuhudumia wateja na katika kusajili na kufuatilia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula,dawa, vipodozi na vifaa tiba sokoni sanjari na kuongeza kiwango cha wateja katika kuzingatia matakwa ya kisheria.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo alisema mfumo huo mpya unatumiwa na watu takribani 300 ambao wamethibitisha kuwa hauna matatizo yeyote kwani lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanapunguza muda wa wateja wao katika kuomba vibali ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za huduma hiyo.

"TFDA inatambua mchango wa TMEA katika kuendeleza mfumo wa e-portal ambao utarahisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za ubora na usalama wa vyakula dawa, vipodozi, vifaa tiba nchini,"alisema.

Mkurugenzi wa TradeMark East Afrika Tawi la Tanzania, Dk. Josephat Kweka alisema mfumo huo utasaidia kuweka mazingira mazuri ya kibiashara hasa katika kuingiza na kutoa bidhaa katika soko la ushindani.

"Portal inatarajia kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Tumewawezesha portal hiyo ili kukuza biashara ya kikanda na ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za jumuia za Afrika Mashariki,"alisema.


Aidha uzinduzi huo ni hitimisho la maboresho ya mfumo huo ulioanza mwaka 2011 ambapo utawawezesha wafanya biashara kuomba na kupata vibali vyote muhimu kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisi za mamlaka hiyo.

TFDA yabadili na Kuzindua Mfumo mpya wa Kuagiza na kutoa bidhaa nchini kumlinda mlaji

Posted By Fikra Pevu - October, 21st 2015 (13)
Views

Mkurugenzi-Mkuu-wa-TFDA-akizungumza-katika-uzinduzi-wa-mfumo-huo-750x350.jpg

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imebadili mfumo wa kuagiza bidhaa nje ya nchi, baada ya kuzindua mfumo mpya unaowezesha wateja wake kutuma maombi kwa njia ya mtandao ili kupata vibali vya kuingiza nchini na kutoa nje ya nchi bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaatiba zilizosajiliwa na mamlaka hiyo.
Maombi hayo yatakuwa wanawasilishwa TFDA kwa njia ya mtandao (Online Import and Export Permits Application) baada ya (TFDA) kwa kushirikiana na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) kuzindua mfumo wa taarifa za kiutendaji, E-portal ambayo itawezesha TFDA kuhudumia wateja wake kwa mfumo wa kidigitali kwa kutumia mtandao wa Internet ambapo sasa huduma za TFDA zitatolewa moja kwa moja kupitia mtandao ili kuleta uwazi na uwajibikaji.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari, akizungumza katika uzinduzi wa mfumo huo unaozinduliwa leo Oktoba 21, 2015 amesema TFDA pamoja na kuwa chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na kwamba kilichofanywa na mamlaka hiyo ni utekelezaji wa sera ya Wizara yake ya utoaji wa huduma za afya na mambo yanayohusiana na afya kwa njia ya mtandao.
Njia hiyo ni moja ya mkakati wa kuendesha Serikali kwa kutumia mtandao hivyo TFDA imetekeleza mkakati huo. Kundi la watu ambao wamekuwa wakijaribu kuingiza bidhaa zisizo halali ‘feki’ kwa sasa watakuwa wamefikia kikomo.
Kutokana na mfumo huo na TFDA wameapa kuendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa mitaani ili kuziba mianya ya matumizi ya bidhaa zisizosajili.
Uzinduzi-wa-mfumo-huo-uliofanywa-na-Mganda-Mkuu-wa-Serikali.jpg

Mtu wa kwanza kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohammed Bakari, wakati wa uzinduzi wa mfumo huo
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, amesema mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa za bidhaa zilizosajiliwa na TFDA kwa lengo la kuzipeleka nje ya nchi au kuzipokea na kubwa zaidi ni wadau wa mamlaka hiyo ambao sasa wataweza kujaza fomu za maombi kupitia mfumo huo bila kufika katika Ofisi za TFDA.
“Unaweza kujaza fomu siku moja na kupata kibali chako siku hiyo hiyo, hivyo wamerahisisha ufanyaji wa biashara na kuwawezesha wadau waetu kufanya kazi kwa ufanisi” alikaririwa na FikraPevu.
Amesema hatua hiyo imepunguza muda wa kufanya kazi kwa wastani wa kati ya saa 48 hadi 72 na sasa kazi ambazo zilikuwa zinafanywa nadani ya muda huo zitatolewa kwa muda wa saa 24. Mteja anaweza kutuma maombi siku hiyo hiyo na kupata kibali, pia imerahisisha kazi kwa TFDA kuhudumia wateja wengi kwa wakati mmoja.
Washiriki-waliohudhuria-katika-tukio-hilo.jpg

Washiriki waliohudhuria katika uzinduzi wa mfumo huo
Mfumo huo tayari umeanza kufanya kazi kwa nchi zote za Afrika Mashariki, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi huku Zanzibar wakiwa wameanza kuufanyia kazi siku za hivi karibuni na umewawezesha kupashana taarifa kwa haraka zaidi miongoni mwa vyombo vya udhibiti.
Mkurugenzi wa TradeMark kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Josephat Kweka, amesema kazi yao kubwa ni kusaidia Serikali zilizopo katika Jumuiya hiyo katika adhma ya kuboresha na kuendeleza mtangamano ili kuwezesha biashara katika nchi wanachama.
Amesema wanafanya kazi na Bandari za Dar es Salaam na Mombasa nchini Kenya, vituo vya udhibiti mipakani na kuhakikisha mifumo hiyo inawezesha kufanyabiashara kwa kufanya kazi na mashirika yanayohusika kuthibiti biashara kwa kutoa vibali ikiwemo Mamlaka ya Mapato nchini.
"Mfumo huu unatarajiwa kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa kupeleka bidhaa nje ya nchi, hivyo kuboresha mazingira ya kufanya biashara, TMEA tumefurahi kushirikiana na TFDA, shirika ambalo ni kiungo katika kulinda na kuboresha bidhaa za afya ya umma wa Watanzania, na ufanisi wa viwango vya ubora na usalama wa bidhaa za vyakula, madawa, vipodozi na vifaatiba kwa sasa utakuwa ni wa uhakika" alisema Kweka.
Watu-mbalimbali-waliohudhuria-uzidnuzi-huo.jpg

Watu mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia mada zilizowasilishwa na watu mbalimbali.
Mfumo huo umeigharimu TFDA takriban Sh. 300 milioni na ya TMEA imetumia Dola za Marekani 250,000 kwa lengo la kuboresha mfumo huo. TMEA iko mbioni kusaidia kuiingiza TFDA kwenye mfumo wa malipo yote nchini Tanzania, kupitia Dirisha Moja la Kitaifa (National Single Window), mradi ambao uko kwenye maandalizi.
TFDA ndiyo mamlaka yenye jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaatiba ili kulinda afya ya jamii ingawa katika siku za hivi karibuni imekuwa ikilalamikiwa kutokana na kushindwa kudhibiti dawa na vyakula bandia ambavyo vimekuwa vikiingia kwa njia mbalimbali nchi bila kukaguliwa.
Moja ya majukumu ya TFDA ni pamoja na kukagua viwanda vya utengenezaji na maeneo ya kuuzia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka ili kuhahikisha viwango vilivyowekwa vinafikiwa kwa lengo la kulinda afya za walaji.
 
Hongera DG Sillo, hongera mkurugenzi Fimbo, honhera mkurugenzi Wegenge, Hongera Mkurugenzi Ngendabanka....Hongereni wafanyakazi wote TFDA bila kumsahau Meneja kanda Maalum Emmanuel Alphonce....
 
Mfumo huo umeigharimu TFDA takriban Sh. 300 milioni na ya TMEA imetumia Dola za Marekani 250,000 kwa lengo la kuboresha mfumo huo. TMEA iko mbioni kusaidia kuiingiza TFDA kwenye mfumo wa malipo yote nchini Tanzania, kupitia Dirisha Moja la Kitaifa (National Single Window), mradi ambao uko kwenye maandalizi.

Mkuu Root tumechangia kiasi cha kutosha.......
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom