Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kudhibiti matumizi ya dawa za Viagra na P2

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kudhibiti matumizi ya dawa za Viagra na P2

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imesema inafanyia utafiti dawa za nguvu za kiume aina ya Viagra pamoja na kuwekea mkakati dawa zinazotumika kuzuia mimba aina ya P2 kwa lengo la kudhibiti uholela wa utumiaji wake.

Mkurugenzi wa TMDA, Adam Fimbo wakati amesema utumiaji holela wa dawa za jamii ya kuzuia mimba na za kuongeza nguvu za kiume zimekuwa zikitumika ndiyo sivyo na hivyo kuwaletea madhara watumiaji.

"Tumekuwa tukipata ripoti mbalimbali, watu wamekuwa wanapoteza maisha, wito wetu mkubwa mtu akitaka kutumia hizi dawa ni vyema apate ushauri kwa mtaalamu wa afya,' amesema Fimbo.

Aidha, ametoa tahadhari katika upande wa matumizi ya dawa za P2 ambazo zimekua zikitumiwa na watoto wa shule na wanawake kwa ajili ya kuzuia mimba ambazo zimekuwa zikileta madhara makubwa na hata vifo.

"Tumeweka mkakati wa kuhakikisha tunatoa elimu kwawatoto wetu wa kike na wanawake kuacha kutumia dawa hizi kiholela kwa sababu zinasababisha vifo visivyotarajiwa na kuelimisha jami matumizi sahihi ya kutumia," amesisitiza.
 
Upuuzi mtupu, mbona sukari inaua na haizuiliwi?
 
Gari linaua mtu mmoja barabarani mpaka zaidi ya hamsini lakini hazipigwi marufuku, Viagra inaua mtu mmoja kitandani eti iwe denjarasi! Hawa jamaa wanataka kutupora my waifu zetu kwa kudhoofisha heshima ya ndoa, tuseme hapana.
Hivi hizo Viagra na P2 kuna watu wanalazimishwa kutumia au hazilipiwi kodi? Mbona sigara na Pombe-Spirit hazizuiwi?

Apo cha kufanya ziongezewe tozo afu ziuzwe kama karanga mitaani Kimoja laki basi.
 
Back
Top Bottom