Kibumbula
JF-Expert Member
- Mar 26, 2018
- 3,683
- 3,349
We acha tu[emoji16][emoji16][emoji16] hii ndiyo Africa......
Sent from my TA-1024 using Tapatalk
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We acha tu[emoji16][emoji16][emoji16] hii ndiyo Africa......
YawezekanaLabda Kenya kuna UDHAIFU wa utunzaji wa mazingira.
Wanataka kuchakaaaaaLugha waliyotumia inalenga kuleta mgawanyiko kwenye jamii!
Tena ni uchochezi wa hali ya juu kutaka jamii isitawalike!
Naomba mamlaka husika ziwachukulie hatua kali haraka iwezekanavyo!
Cc @magufuli [emoji23][emoji23]
Only themselves know.But how???
Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
HakikaHiyo mvua tunaiuza hatuachii bure
Inawezekana huyu afisa ni wa hapa mtandaoni...Katika hali isiyo ya kawaida, mamlaka ya hali ya hewa ya Kenya imesema kuwa mawingu yenye mvua yamekwama Tanzania.Habari zaidi tembelea Bbcswahili.View attachment 1068769
Sent from my TA-1024 using Tapatalk
=====
Idara ya hali ya hewa Kenya: Mvua imekwama Tanzania
Idara ya hali ya anga nchini Kenya inasema kuwa kiangazi kitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu huku upepo wa mvua ukisalia nchini Tanzania kutokana na kiwango cha chini cha upepo.
Mvua ndefu itaanza kunyesha katika maeneo mengi ya Kenya ifikiapo miwsho wa mwezi huu, wataalam wa hali ya anga wamesema.
Kaimu mkurugenzi wa shirika la hali ya anga nchini Kenya Stella Aura alielezea kwamba upepo wenye mvua umekwama nchini Tanzania kutokana na shinikizo ya kiwango cha chini ambayo haiwezi kuisukuma mvua hiyo kuelekea kaskazini mwa Kenya.
Mwezi Aprili ndio mwezi wa mvua ndefu nchini Kenya na onyo limetolewa katika maeneo kadhaa ya Kenya kuhusu kuchelewa kwake.
''Mvua ya msimu husababishwa na upepo wa mvua unaoelekea kaskazini lakini kufikia sasa upepeo huo haujaelekea kaskazini'', aliambia vyomb vya habari.
''Mvua imekwama nchini Tanzania, mifumo ya upepo iliopo kusini haijashikamana kuweza kusukuma mawingu hivyobasi mvua itachelewa , lakini mvua itaanza kunyesha mwisho wa mwezi huu'', alisema.
Mvua Ndefu
Hatahivyo amesema kuwa mvua ndefu imeanza lakini kwa kiwango kidogo katika maeneo mbalimbali.
Mvua ndefu hunyesha miezi ya Machi, Aprili, na Mei hususan katika eneo la magharibi , bonde la Ufa na mkoa wa kati na ni muhimu sana katika sekta ya kilimo hatua inayosababisha kuwepo kwa chakula cha kutosha.
Idara hiyo imewashauri wakulima kupanda mimea inayokuwa kwa haraka na ile isiotegemea maji kwa kuwa mvua hiyo huenda isinyeshe kwa muda mrefu.
Mafuriko
Wale wanaoishi katika maeneo ya nyanja za chini ikiwemo miji midogo isio na mitaro ya kusafirisha maji walionywa kwamba watarajie mafuriko.
Magharibi mwa Kenya, visa vya radi vinatarajiwa kuongezeka huku maporomoko yakitarajiwa kufanyika katika maeneo ya juu ikiwemo Murang'a na Meru miongoni mwa mengine.
Maporomoko pia yanatarajiwa kuathiri maeneo ya magharibi na mkoa wa Bonde la Ufa.
''Mikakati inafaa kuwekwa ili kuzuia maafo yoyote'' ,ilishauri idara hiyo.