Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu uwepo na mwenendo wa Kimbunga Kikali “CHENGE” ambacho kwa sasa kipo katika Bahari ya Hindi, upande wa kaskazini mashariki mwa Madagascar, takribani kilomita 2,400 mashariki mwa pwani ya Mtwara
Kimbunga Kikali “CHENGE” kilianza kuunda katika eneo la mashariki mwa Bahari ya Hindi tarehe 17 Oktoba 2025 na kimeendelea kupata nguvu kadri muda unavyopita
Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonyesha kuwa Kimbunga hiki kinatarajiwa kuendelea kusogea magharibi kupitia Bahari ya Hindi kuelekea pwani ya nchi yetu ndani ya siku nne hadi tano zijazo (kati ya tarehe 26 na 27 Oktoba 2025), huku kikitarajiwa kupungua nguvu
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Kimbunga Kikali “CHENGE” na athari zake kwenye mifumo ya hali ya hewa nchini, na itaendelea kutoa taarifa na masasisho pale inapohitajika
Mamlaka Watumiaji wa bahari na umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri na taarifa mpya za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, pamoja na kupata ushauri na maelekezo kutoka kwa wataalamu wa sekta husika
Chanzo: Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA)