Mamlaka ya Hali ya Hewa yafafanua baridi la Njombe: Kinachotokea ni Sakitu siyo theluji

Mamlaka ya Hali ya Hewa yafafanua baridi la Njombe: Kinachotokea ni Sakitu siyo theluji

Kuna video nimeiona imechukuliwa makete, Yani Ile Ni snow kabisa Kama vile uko ulaya. Snow Imejaa barabarani Halafu watoto wanaenda shule wamevaa kaptula mpaka unajiuliza hiyo baridi miguuni haiwapigi.
Washa adapt labda ndio explanation iliyopo ? Maana kama Eskimo wa eastern Siberia na Alaska wanavaa masweta ya ngozi wao ni kina nani wasivae waizoee baridi hivyo
 
Kuna video nimeiona imechukuliwa makete, Yani Ile Ni snow kabisa Kama vile uko ulaya. Snow Imejaa barabarani Halafu watoto wanaenda shule wamevaa kaptula mpaka unajiuliza hiyo baridi miguuni haiwapigi.

Mwili umekuwa ume adopt hiyo hali.

Wanyama tuna tabia ya kubadili hali ya joto la mwili kulingana na hali ya mazingira ili tuendelee kuwa hai.

Wewe ambaye hujazoea hiyo hali, kwa siku za mwanzo utapata shida sana.

Hao watoto wanahisi ni kawaida kwa sababu wamesha adopt hiyo hali
 
Sakitu 🐒
 
Wabongo bhana. Wao wamesema hio si theluji(snow) Bali ni sakitu(frost). Hawana maana kuwa Njombe hakuna baridi ipo ndio maana inagandisha hadi umande unaoleta barafu. ILA hakuna snowing.
 
Kwani Frosty ni nini? Sii ni baridi lilioganda ikimanisha barafu nyepesi...

Ila siyo barafu ya kudondoka kutokea juu...
 
Kutokana na baridi na kuonekana vitu kama barafu kwa siku za karibuni maeneo ya Njombe hali ambayo imesababisha watu wengi wawe na maswali tofauti kimefafanuliwa.

Mamlaka Hali ya Hewa Nchini (TMA) imefafanua kuwa kinachotokea maeneo ya Njombe kwa siku kadhaa ni kutokea kwa Sakitu, ambapo hiyo ni hali ya kuganda kwa umande katika eneo la uso wa ardhi kwa muonekanao inakuwa kama theluji.

Meneja TMA, Samwel Mbuya amesema: “Tumeangalia kitaalamu na kugundua kinachotokea ni Sakitu au ‘frosty’, hiyo inatokana na baridi kuwa kali na kwa kuwa kuna upepo wa kusi inasababisha maeneo mengine kuongezeka kwa baridi kutokana na upepo huo.


Chanzo: Azam TV

Sakitu ndio Frost, kweli kiswahili kimekuwa sana.🤣
 
hakuna mwenye walau kapicha ka sakitu kweli...
 
Uingereza kwa sasa kuna joto la kufa mtu hadi hali ya hatari imetangazwa.

Njombe napo huwa kuna joto kali kipindi fulani?
well, sijajua kama Njombe huwa kuna joto kali, napasikiaga kusifika kwa baridi
 
Kuna Mwalimu mmoja wakati anasoma Makete,alisema kuwa kuna kipindi maji yalikuwa hayatoki asubuhi,akiuliza anajibiwa maji yameganda subiri baadae yayeyuke kwanza.Yeye ni mtu wa Iringa lakini alisema baridi ya Makete amenyoosha mikono
 
Back
Top Bottom