Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro: Shughuli za utalii bado zinaendelea licha ya taarifa za Maandamano

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro: Shughuli za utalii bado zinaendelea licha ya taarifa za Maandamano

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
photo_2024-08-18_22-21-13.jpg
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa taarifa kwa Umma juu ya shughuli za utalii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwamba zinaendelea vizuri pamoja na uwepo wa baadhi ya wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo kuandamana leo tarehe 18.08.2024.

NCAA katika taarifa yao hiyo, imesema kuwa, Watalii kutoka ndani na nje ya nchi wameendelea na safari zao za kushuhudia vivutio vya utalii ndani ya Hifadhi na Serikali inaendelea kuwahakikishia usalama wao.

"Maandamano yaliyoripotiwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii yanaidhihirishia dunia na jumuiya za kimataifa, vyombo vya habari na asasi za kimataifa kwamba ndani ya Hifadhi hiyo hakuna ukiukwaji wa haki za binadamu na unyanyasaji wa wananchi.

Mamlaka inawahakikishia watalii wote waliopanga safari za kuja Ngorongoro kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wao wakati wote watakapokuwa ndani ya hifadhi." Imebainisha taarifa hiyo iliyotolewa na Hamis Dambaya, Kaimu Meneja , Kitengo cha Uhusiano kwa Umma wa NCAA.

Pia soma ~ Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
 
Back
Top Bottom