Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Veronica Matikila akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Nchini Tanzania (DCEA), Gerald Kusaya, amesema leo Disemba 21, 2022 wameteketeza kilo 584.55 za dawa za kulevya zinazojumuisha kilo 569.25 za Heroin, Cocaine kilo 15.3 na Tani mbili za bangi na mirungi.
Uteketezaji huu umefanyika kufuatia kumalizika kwa mashauri ya dawa za kulevya katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, na Mahakama za Hakimu Mkazi za Kisutu na Kibaha Pwani pamoja na Mahakama za Wilaya ya Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni.
Dawa za kulevya zilizoteketezwa zimehusisha mashauri ya kuanzia mwaka 2009 hadi 2022.
Hii ni mara ya pili kwa mwaka 2022 uteketezaji wa dawa za kulevya unafanyika. Uteketezaji wa kwanza ulifanyika mwezi Februari ambapo jumla ya kilo 250.7 ziliteketezwa katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote mkoani Mtwara. Kwa mwaka 2021, uteketezaji ulifanyika mkoani Mtwara ukihusisha kilo 355 za dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.
Aidha, hekari 41 za mashamba ya bangi na mirungi ziliteketezwa katika mikoa ya Pwani, Arusha na Kilimanjaro.
Tangu kuanzishwa kwa Mamlaka mwaka 2017, hii ni mara ya tatu kufanya uteketezaji katika kiwanda hiki cha Twiga. Mara ya kwanza uteketezaji ulifanyika tarehe 8 Oktoba 2019 ambapo kilo 120.91 za heroin, kilo 70.96 za cocaine ziliteketezwa.
Amesema mara ya pili ulifanyika 12 Novemba 2020 ambapo kilo 118.174 za heroin, kilo 3.932 za cocaine na kilo 120 za bangi ziliteketezwa.
Uteketezaji wa dawa za kulevya hufanyika kwa namna ambayo hulinda afya na kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira. Zoezi hili hushuhudiwa na Mahakama pamoja na Taasisi nyingine zinazojihusisha na Udhibiti wa dawa za kulevya ambazo zimeainishwa kwenye Kanuni za Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Wadau hao ni Hakimu au Jaji, Kamishna Jenerali, Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkemia Mkuu wa Serikali, Idara ya Usalama wa Taifa, Baraza la Taifa la Mazingira na wadau wengine watakaoalikwa na Kamishna Jenerali.
Aidha, Uteketezaji wa dawa za kulevya ni zoezi endelevu ambalo hufanyika pale inapohitajika. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya itaendelea kutoa
taarifa kwa Umma juu ya zoezi la uteketezaji wa dawa za kulevya ili kuwapa taarifa wananchi kuhusu hatua hii muhimu katika mapambano dhidi a dawa za kulevya.
Kipekee shukrani ziwaendee Majaji na Mahakimu, Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkemia Mkuu wa Serikali, Idara ya Usalama wa Taifa, Baraza la Taifa la Mazingira, Waandishi wa Habari na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha zoezi hili muhimu la uteketezaji.
Aidha, shukrani zimwendee mwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga kwa kuendelea kutupatia ushirikiano na kuruhusu zoezi hili kufanyika kiwandani kwake.